Hamas wameshapoteza

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,250
Reaction score
26,641
Mpango wa Trump wa vipengele 20 kuhusu Gaza

Rais wa Marekani Donald Trump amependekeza mpango wa amani wenye vipengele 20 ili kumaliza vita vya Gaza baada ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.

Muhtasari wa vipengele 20:

1. Gaza itakuwa “eneo lisilo na ugaidi, lililopokonywa misimamo mikali.”

2. Gaza itajengwa upya ili kuboresha maisha ya wakazi wake.

3. Vita vitakoma mara moja pande zote mbili zitakapokubaliana, Israeli ikijiondoa katika mstari uliokubaliwa na kusimamisha mapigano.

4. Mateka wote, walio hai na waliokufa, watarejeshwa ndani ya saa 72 baada ya Israeli kukubali mpango huo.

5. Israeli itawaachia huru wafungwa 250 wa Kipalestina waliohukumiwa kifungo cha maisha, wafungwa 1,700, na mabadilishano yataendelea kwa uwiano.

6. Wanachama wa Hamas watakaojisalimisha na kuachana na silaha watapewa msamaha au nafasi salama ya kuondoka kwenda nje ya nchi.

7. Misaada yote ya kibinadamu itaingia mara moja kwa ajili ya kujenga upya miundombinu muhimu.

8. Misaada itasafirishwa kwa uhuru kupitia Umoja wa Mataifa na Hilali Nyekundu, na mpaka wa Rafah utafunguliwa tena chini ya makubaliano.

9. Gaza itatawaliwa kwa muda na kamati ya Wapalestina ya kiufundi chini ya bodi ya kimataifa ikiwemo Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair na kuongozwa na Trump.

10. Mpango wa kiuchumi wa Trump utajenga upya Gaza kwa uwekezaji wa kimataifa na uundaji wa ajira.

11. Eneo maalum la kiuchumi litaanzishwa lenye masharti mazuri ya biashara.

12. Hakutakuwa na uhamisho wa kulazimishwa; watu watakuwa huru kubaki, kuondoka au kurejea.

13. Hamas itatengwa kutoka kwenye uongozi na silaha zote zitaondolewa.

14. Washirika wa kieneo watatoa dhamana ya Hamas kufuata makubaliano na kudumisha usalama.

15. Kikosi cha Kimataifa cha Kudhibiti Amani (ISF) kitapelekwa Gaza kulinda amani na kufundisha polisi.

16. Israeli haitakalia Gaza; itajiondoa kadri utulivu na upokonyaji silaha utakavyosonga mbele.

17. Iwapo Hamas itakataa mpango huo, maeneo yatakabidhiwa kutoka jeshi la Israeli kwenda ISF.

18. Mazungumzo ya kidini yataanzishwa ili kukuza “thamani za uvumilivu na kuishi kwa amani.”

19. Mageuzi yataandaa njia kwa ajili ya “kujitegemea na kuanzishwa kwa taifa la Palestina.”

20. Marekani itaongoza mazungumzo kwa ajili ya mustakabali wa kisiasa wa amani kati ya Israeli na Wapalestina.

HUU MPANGO UNAIFAIDISHA ISRAELI NA SIO HAMAS.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…