Hamadi Rashidi kufukuzwa chama cha ADC kwa Usaliti

Hamadi Rashidi kufukuzwa chama cha ADC kwa Usaliti

kuna yule mwalimu nani sijui alikua anaandika threads za AcT. Nilidhani Mwigamba ndio Mcubic
 
Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Said Miraj amemshushia tuhuma tatu mgombea urais wa chama hicho visiwani Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed, huku akisisitiza kuwa ili kukinusuru chama hicho ni lazima afukuzwe.

Miraj ambaye kabla ya kujiunga na ADC alikuwa kada wa CUF, ameyataja shutuma hizo kuwa ni; Hamad Rashid kutumiwa na CCM kushinikiza uchaguzi uliofutwa Zanzibar kurudiwa, ubadhirifu na kupanga njama za kutaka uongozi wa chama hicho kinyume na katiba na taratibu.

Hata hivyo, Hamad Rashid amejibu madai hayo akisema: “Tuhuma dhidi yangu zimeanza siku nyingi tangu nikiwa CUF. Kama mazungumzo ya CUF na CCM yanaendelea sipaswi kusema nitashiriki uchaguzi wa marudio? Labda tuwaulize hao waliopo katika mazungumzo sababu za kutovishirikisha vyama vingine vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa Zanzibar.

Kwa nini nisiamini Miraj anatumiwa na CUF. Nilieleza wazi kuwa ZEC (Tume ya Uchaguzi Zanzibar) haikutenda haki kufuta uchaguzi. Kama nia yangu ingekuwa kuwa mwenyekiti wa ADC ningegombea tangu zamani.”

Hamad Rashid ambaye alipewa kadi namba moja baada ya kujiunga na ADC Julai 23 mwaka jana, alisema yeye ndiye aliyemshinikiza Miraj kujiunga na chama hicho na kugombea uenyekiti.

Katika tuhuma zake, Miraj alisema: “Hamad alifukuzwa CCM kwa hila, akafukuzwa CUF kwa kutaka madaraka na sasa analeta hayo mambo ADC. Huku tutamfukuza pia maana anataka kukifanya chama hiki kuwa tawi la CCM.”

Akizungumza jana, Miraj alisema atatoa msimamo wake kuhusu suala hilo Januari 11 katika mkutano na waandishi wa habari akisema: “Ikiwa mimi nitang’oka katika chama nitaeleza uozo wote anaoufanya Hamad Rashid na ikiwa nitabaki katika chama nitatoa masharti yangu.”

Miraj alisema Hamad Rashid ni mlezi wa chama hicho na si kiongozi na jukumu lake ni kutoa ushauri kwa viongozi wa ADC, hivyo hapaswi kuingilia utendaji na kutoa matamko.

“Kuna njama za kutaka kuniondoa mimi niliyechaguliwa kikatiba na zinafanywa na wajumbe wa bodi ya wadhamini ya ADC akiwamo Hamad,” alisema huku akionyesha barua za malalamiko kuhusu suala hilo zilizoandikwa na wanachama 30 kwenda ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.

“Iweje (Hamad) aitishe vikao kuhoji yanayofanyika ndani ya chama? Baada ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar aliandika barua kupinga matokeo bila viongozi wa ADC kujua. Alitoa kauli uchaguzi Zanzibar urudiwe wakati akijua mazungumzo yanaendelea kati ya CCM na CUF.”

Alisema Hamad Rashid alionekana kuwa msaliti tangu mwanzo na ndiyo sababu viongozi wakuu wa ADC hawakushiriki kampeni za chama hicho visiwani Zanzibar.


Chanzo: Mwananchi
 
Mwenyekiti ADC Bwn.Miraji ameviambia vyombo vya habari kuwa Hamad Rashid ni lazima afukuzwe.

Hamad aliyekuwa mgombea wa ADC ametuhumiwa kushirikiana na CCM kuhujumu wazanzibar,Hamad ametajwa kuunga mkono uchaguzi kurudiwa!Pia anatuhumiwa kwa ubadhilifu wa pesa na kutaka madaraka kinyume na utaratibu.Bado Zito Kabwe
Ohoooooooo.. Tena???
Huyu jamaa si bure CUF walimtimua sababu ni Zitto type..
 
Hivi Hamad si ndio aliyeanzisha hiki chama cha ADC...??
Alianzisha lakini alipobugi ni pale aliposahau kujipa ufalme wa Chama kama yule mwenzake kutoka Mwandiga,yeye Hamad Rashid nguvu na akili yake yote alielekeza kwenye Urais ili Seif kura zake zipungue but mwishoni amekosa vyote na wajanja wamemshtukia.
 
Yes, point ni kumfia, siyo kufukuzwa!

Hivi hicho chama cha ADC kina hata mbunge?

Kimebahatisha kupata madiwani?

Maana vyama vingine inabidi vipunguzwe, tupunguze kuwa na utitiri wa vyama;

Huko mbele wanaona sisi tuko vizuri demokrasia kwa kuwa na mavya mengi kumbe geresha tu.
Nami nataka nianzishe changu cjui mtanisupport
 
Hamad Rashid anaweza kujiunga na ACT iligombee uraisi mwaka 2020,cc Mwalimu Kaijage,cc Dotto Rangimotto
 
Nami nataka nianzishe changu cjui mtanisupport

Hutakosa wa kukusapoti mkuu,

Inabidi uanzie home kwenu kwanza,

Maana vyama vingi base kubwa ni nyumbani kwa waanzilishi.
 
H
Mwenyekiti ADC Bwn.Miraji ameviambia vyombo vya habari kuwa Hamad Rashid ni lazima afukuzwe.

Hamad aliyekuwa mgombea wa ADC ametuhumiwa kushirikiana na CCM kuhujumu wazanzibar,Hamad ametajwa kuunga mkono uchaguzi kurudiwa!Pia anatuhumiwa kwa ubadhilifu wa pesa na kutaka madaraka kinyume na utaratibu.Bado Zito Kabwe
iki ni chama cha hamad rashid hao wengine wote kawaleta yeye na gharama zote anatoa yeye,huyo miraji hana ubavu wa kumtoa hamad ataondoka yeye
 
Back
Top Bottom