Hamad Rashid kuhamia ADC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamad Rashid kuhamia ADC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Mar 1, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, ameibuka na kuweka wazi dhamira yake kwamba, kama Mahakama Kuu itaridhia uamuzi uliofikiwa na Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa wa kuvuliwa uanachama hatakata rufaa na badala yake atachukua uamuzi wa kujiunga na chama kipya cha siasa cha Alliance for Democratic Change (ADC).

  Amebainisha hayo jana wakati akizungumza katika mahojiano na NIPASHE Jijini Dar es Salaam kuhusu msimamo wake iwapo Mahakama kuu itatupilia pingamizi lake la kupinga kuvuliwa uanachama.

  Mohamed alisema kwa kuwa anaheshimu utawala wa kisheria hivyo iwapo mahakama itaamua kutupilia mbali pingamizi lake hatakata rufaa katika Mahakama ya Rufaa na badala yake atajiunga katika chama kipya cha siasa cha ADC.

  "Mahakama ikikubaliana na uamuzi wa kuvuliwa uanachama wa CUF uliofanywa na baraza kuu, na kwa kuwa sasa nitakuwa nimekosa sifa ya kuwa mbunge hivyo napenda kuweka wazi kwamba sitasumbuka kukata rufaa nitajiunga na chama cha ADC," alisema Mohamed.

  Mbunge huyo alivuliwa uanachama na wenzake mapema mwezi Januari mwaka huu na hivyo kumfanya apoteze sifa ya kuwa mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Hata hivyo, Hamad Rashid alilazimika kukimbilia mahakamani na kufanikiwa kupata hati ya kuzuia kikao cha Baraza Kuu la CUF..
  Hamad na wenzake 13 walifungua shauri namba 1 la mwaka 2012, lililosomwa Januari 3, mbele ya Jaji Augustine Shangwa ambaye na Januari 4, majira saa 3:40 alitoa uamuzi wa kuzuia kufanyika kwa kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa kilichokutana mjini Zanzibar kumjadili mbunge huyo na wenzake.
   
 2. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Aache kuchezea watu akili. anahamiaje kwenye chama chake alichokianzisha? Anatufanya kuwa sisi hatujui kuwa yeye ndio muasisi wa ADC...Ni sawa na uandike "MTEI KUHAMIA CHADEMA"
   
 3. k

  kicha JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 500
  Likes Received: 519
  Trophy Points: 180
  hivi huyu hamad anadhani tuna upeo kiasi gani mpaka aseme eti ATAHAMIA
   
 4. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ameshahamia ADC, ila hataki kuziachia posho za ubunge so atakuwa anavuta mshiko wa ubunge (sh. 7,200,000/= per month) kwa mgongo wa CUF huku akiendelea kukijenga chama chake cha ADC
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Aende kwenye chama chake alichokianzisha wala asiseme kuwa atahamia.
   
 6. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ameshahamia ADC, ila hataki kuziachia posho za ubunge so atakuwa anavuta mshiko wa ubunge (sh. 7,200,000/= per month) kwa mgongo wa CUF huku akiendelea kukijenga chama chake cha ADC
   
 7. Smallfish

  Smallfish JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 222
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hamad amedhihirisha uroho wake wa madaraka.Alitakiwa astafu siasa.Hivi pamoja na uzoefu wote huo, hawezi kuanzisha consultancy ya kisiasa badala ya kuanzisha chama kipya?Fani yake ni nini?
   
Loading...