Hamad Rashid, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa ADC Kitaifa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,689
55,661
Mkutano Mkuu wa ADC Taifa umemchagua Waziri wa Kilimo, Maliasili, Uvuvi na Ufugaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Mkutano Mkuu wa ADC Taifa umefanyika hii leo katika Hotel ya Peacock jijini Dar es salaam.
3b70113f9e5bd764a4ab8dcafdea7882.jpg
4594d10f0edc9361a27858d89ff74b44.jpg
bddc1a52dbff5209703d0479c51c0096.jpg
 
Duuuuuuu huyu alishafukuzwa ila kwa kuwa kaukwaa Swazi Sasa ndio boss, kawatimua na mahasimu wake kwenye chama
 
Jamaa mmoja alimhurumia Punda wake kwa kutaka kumhifadhi ndani ya kibanda chake............mvua ilikuwa inanyesha.
Punda hakuthamini hisani ya yule Bwana.........akakibinua kibanda kile..............Jamaa akakosa pa kulala.
Masikini Said Miraraji...........punda kabinua kibanda
 
Mkutano Mkuu wa ADC Taifa umemchagua Waziri wa Kilimo, Maliasili, Uvuvi na Ufugaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Mkutano Mkuu wa ADC Taifa umefanyika hii leo katika Hotel ya Peacock jijini Dar es salaam.
3b70113f9e5bd764a4ab8dcafdea7882.jpg
4594d10f0edc9361a27858d89ff74b44.jpg
bddc1a52dbff5209703d0479c51c0096.jpg
Hivi huyu hamad rashid ndio yule aliyekuwa wa cuf akiganga njaa mwajukwaani kuiponda ccm ama
 
Mkutano Mkuu wa ADC Taifa umemchagua Waziri wa Kilimo, Maliasili, Uvuvi na Ufugaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Mkutano Mkuu wa ADC Taifa umefanyika hii leo katika Hotel ya Peacock jijini Dar es salaam.

Hujamalizia stori yako. Pia baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa ADC aliishawishi Kamati kuu kuwafukuzilia mbali wale vibaraka wa UKAWA waliotaka kumvua uanachama.

Hivyo basi Mkutano Mkuu ukaadhimia kumfukuza Rasmi uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa ADC ndugu Said Miraj, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi ndugu Jumanne Magafu na Katibu wa Ulinzi na Usalama ndugu Juma Malumbo.
 
Kuondoka madarakani kwa Mwenyekiti wa Chama cha ADC, Said Miraji Abdullah, kumetoa nafasi kwa Hamad Rashid kurithi kiti chake.

Miraji ameondoka kutokana na kutofautiana na viongozi kuhusu uamuzi wa chama hicho kushiriki uchaguzi wa marudio wa Zanzibar uliofanyika Machi 20, mwaka huu.

Chama hicho pia kimemchagua Doyo Hassan Doyo kuwa Katibu Mkuu aliyechukua nafasi ya Lydia Bendera ambaye alikuwa akimuunga mkono Abdullah kwa kutotaka chama hicho kisishiriki uchaguzi huo.

Akizungumzia hatua hiyo, makamu mwenyekiti wa ADC, Adelastella Mkilindi amesema chama hicho kimefikia uamuzi huo ili kutimiza matakwa ya kikatiba yanayotaka kuwa na uongozi kamili.

Source: Mwananchi
 
Back
Top Bottom