Hamad Rashid aapa kuimaliza CUF

eti tawi la chama linaitwa CHECHNIA, KOSSOVO
hamad Rashid ni mroho sana yaani huyu hastahili kuonewa huruma
 
hakika strategy za CCM ktk kuvuruga upinzani zinafanya kazi vizuri

Ndugu yangu sidhani kama hapa CCM inapaswa kulaumiwa,haya ni matatizo ya wana CUF wenyewe kwa baadhi ya viongozi kutuonyesha hulka zao halisi baada ya kukosa maulaji. Hamad Rashid na kundi lake wakiwa Bungeni wameharibu kabisa hata hiyo heshima kidogo CUF iliyokuwa imebakiza huku Bara. Sasa eti huyo ndiye anadai anataka kuifufua CUF!
 
Me nasubiri kitakachojiri,huyu hamad rashid alikuwa wapi mpaka leo akurupuke kutaka kujenga chama wakati kilishapotea kwenye ramani ya vyama vya siasa tz hasa toka walipofunga ndoa,so toka ndoa,hakuona kwamba ulikuwa ndo mwanzo wa kifo cha cuf hasa huku bara?au ni chuki binafsi dhidi ya seif kisa kula shavu kwenye hiyo s.u.k na kupotezwa mjengoni?
 
This dude called Hamad Rashid could either be a true opposition figure or a power monger who is willing to do anything, even destroying the cause he claims to be representing, to get to a top position. Am afraid I tend to believe that he falls under the latter category. I recall his war against the "official opposition" he himself had fought to create while still head of the "official opposition" in the parliament.
 
Kwa nini Hamad Rashid asitafute nafasi ya uenyekiti badala ya Katibu? Nafasi ya mwenyekiti katika kuimarisha/kufifisha chama iko wapi? Mimi nilifikiri kama chama kimepoteza mwelekeo basi uongozi wa juu unawajibika kwa maana hiyo mwenyekiti. Very strange party!
 
hakika strategy za CCM ktk kuvuruga upinzani zinafanya kazi vizuri

Hebu fikiria upya ulichokiandika. CCM haivurugi wapinzani ila inajivuruga yenyewe. Hawa CUF wanaandamwa na laana ya uroho wa madaraka. Ikumbukwe kuwa:
1. Ni uroho wa madaraka ndio umemfanya Seif Sharif Hamad kuingia ikulu ya SMZ na kuyaacha yale aliyoamini ndio sahihi hapo kabla.
2. Ni uroho wa madaraka ndio uliomfanya Hamad Rashid kuanzisha kambi yake ya upinzani bungeni akiigomea ile iliyo rasmi kwa mujibu wa katiba ili mradi tu alichukizwa kutopanda shangingi la Shadow PM.
3. Ni uroho wa madaraka tu ndio unawafanya CUF kutokuwa na utaratibu ulio wazi wa kuchagua uongozi wa juu wa chama chao
4. Ni uroho wa madaraka ndio unaofanya CUF wasiwe na mgombea urais tofauti na mnyamwezi

Kama haitoshi, CUF pia inaathiriwa na unafiki. Katika kikao cha mwisho cha bunge la kumi, maneno ya wabunge wengi wa CUF yalikuwa yakiwaambia wananchi kuwa CHADEMA ni chama cha fujo na dini. Tukio hili linakuwa jipya ktk historia za fujo za Tanzania (kwani nyingi huwa ni za kufikirika tu kufuatia intelijensia za polisi wetu) kwani CHADEMA ambao ndio wanaolalamikiwa kuwa wanaharibu amani ya nchi, hawajawahi kuonekana na fimbo wala jiwe kwenye maandamano yao achilia mbali mapanga ambayo CUF wameonesha uwezo mkubwa wa kuyatumia.

Kila mwenye ubongo wake na asome magazeti ya leo, atafakari dhana zilizotumiwa ktk fujo yao tukufu, atathmini majina ya viongozi wa CUF wanaoonekana kwenye hizo habari halafu ajipe majibu, kipi ni chama cha FUJO na DINI, CCM B au CDM?
 

CCM B nao wanafuata nyayo za partiner wao CCM A kujivua magamba
 
CUF kwishney!!!!!!!!!!!
Hamad Rashid naye ni pandikizi na mvugaji mkubwa wa upinzania alifanya jitihada kuungana na Kafulila ili kuvuruga nguvu ya upinzani bungeni, lakini CHADEMA walivyo smart wakashtukia mchezo wao mchafu. Sasa hivi CUF ni vuruvuru toka kwa Hamad Rashid na Kafulila naye anapiga vuruvuru huko NCCR Mageuzi, CCM bado wanapande la la kujivua gamba na mpasuko mwaka unaokuja tutashuhudia mengi kwenye hivi vyama vitatu yaani CCM, CUF na NCCR Mageuzi.
 
Shughuli pevu ilikuwa leo 13/12/2011 ambapo mbunge huyo wa wawi - Pemba alikuwa na ziara nyingine katika tawi la CHECHNIA lililoko kata ya mabibo. Baada ya walinzi wa taifa na wa wilaya kuzuia shughuli ya KOSOVO inaonekana hamad rashid na wenzie walijipanga zaidi na kukodi kundi kubwa la vijana wapatao 150 ili kulinda mkutano wake wa mabibo. Majira ya saa 8.00 mchana vijana kadhaa walianza kufika ukumbi wa mkutano wengine wakiwa na makoti na wengine wakiwa na kofia za mazoezi maarufu PAMA. Wengi wa vijana hao walionekana kuwa na nyuso nzito na baadhi yao walionekana kama wamepata kilaji kidogo.

Labda ni mimi nimepitwa na tarehe na siku kwamba leo Jumanne ndio 13/12/2011. Mbali na hilo Ukatibu Mkuu wa Chama ni jambo la kupita nchi nzima kufanya kampeni ???? Naomba nielimishwe.
 

umemaliza kila kitu mdogo wangu kilichokuwa ndani ya moyo wangu ubarikiwe kwa kuwa na hekima ya mfalme Suleman wa kwenye biblia.
 
Waache wahangaike na laana yao ya kutaka kutuvuruga Watanganyika, mimi si mfuasi wa CUF sioni tofauti yao na wadhalimu wengine ambao ni CCM, kama wanafanya hayo kuua upinzani wamechemka mpinzani ni CDM si CUF... walipe fadhila za kuhongwa na CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…