Halotel ni kiboko kwa internet speed

Hawajafunga 3G minara yao yote.

Kwenye district ambayo ninaisimamia mimi tokea tunaanza kuingia mikataba na wenye maeneo hadi kumaliza ujenzi wa towers, siyo minara yote tuliyofunga 3G japo minara mingi ni ya 3G.

asante kwa kutuelimisha hilo maana wao wanajinasibu kuwa wamefunga 3g minara yote.
 
Leo niliamua ninunue laini ya hawa jamaa nijaribu ubora wao kwenye internet kusema kweli wamekidhi vigezo sijawahi fikia speed hii kwenye modemu, shida vocha zao tu zinasumbua mpaka urushiwe.

nimeshindwa ku updload picha sababu ya matatizo ya jamii forums ila speed ni above 4.76Mbps ambayo sijawahi ipata kabisa kwa mitandao mingine.

NB: nimedownload movie ya the battle of stanligrad 386MB kwa dakika 7 tu.

Mpaka sasa inawateja wangapi?....huoni uchache wa wateja wao unachangia hilo?
 
asante kwa kutuelimisha hilo maana wao wanajinasibu kuwa wamefunga 3g minara yote.

Mkuu nasikia hawa jamaa wamewekewa speed governor ili wasithreat mafisadi ,vodacom,airtel,tigo maana haiwezekani kamponi changa inaanza na vifurushi vya gharam hivy ,mara mb 8
 
Mkuu nasikia hawa jamaa wamewekewa speed governor ili wasithreat mafisadi ,vodacom,airtel,tigo maana haiwezekani kamponi changa inaanza na vifurushi vya gharam hivy ,mara mb 8

kwani hao kina voda na tigo pia si wameamrishwa watenganishe vifurushi vya data na mb?

hapa huwezi ulaumu mtandao wowote ule mbaya wetu ni TCRA kinachotakiwa ni kuwahimiza warudishe mfumo wa zamani

na kama walikua na nia kweli hao Halotel basi hata hivyo vya mb tupu wangetupa mb nyingi lakini na wao wanakaba koo vile vile tena vifurushi vyengine wanakaba kuliko hao wazoefu. nikipata muda nitaeka comparison ya vifurushi vya mitandao yote.
 
4G ya tigo iko vizuri sana na ni affordable..kama unataka kushusha movies subiri saa 5 usiku wakikupa zile GB 15...connect Mobile Hotspot na wireless ya PC...unapata speed ya 4G kwnye computer..utadownload mpaka download yenyewe iseme download download!

hahahaha! Mkuu Sad eyes umenifurahsha sana doh! Download download??
 
Nimetumia halotel nikiwa Moshi speed yake sio mchezo! Wakijitahidi kusambaza vocha zao kila mahali watafanya vizuri sokoni! Nimedownload episode 15 zenye 75mb kwa 30minutes only.
 
Sema watu hawafuatilii...holotel anavuta ikifika muda ata drop...kwa kuwa teyari amekuza database..Voda, Airtel na tigo speed ipo ila inategemean ana kiasi unachochuku...

 
Kubali ukatae hawa jamaa wapo vizuri alafu hii ni HSPA+ tu wakilaunch 4G sijui itakuwaje.
 
Back
Top Bottom