Moro-Dar full 3G njia nzima, ya uhakika. Hapa naona tofauti kati ya hawa Halotel na wengine. Miongoni mwa vitu ambavyo vilikuwa vinanishangaza ni kukosekana kwa intaneti ya uhakika katika barabara kuu. Yaani kwa mitandao mingine ukishauacha mji ni shida, hata mjini kwenyewe inachagua maeneo.
Halotel wamenishawishi nitafuta dual sim smartphone na power bank nzuri tu, nikiwa njiani ni raha tu.
Hawa jamaa wako vizuri. Suala la kuchagua maeneo kama lipo basi ni kwa kiasi kidgo sana, binafsi sijawahi kukumbana nalo. Hapa 800MB za kasi kubwa zimeisha ila natazama video YouTube vizuri tu ingawa ubora wa picha umepungua kidogo.
Hebu toka hilo eneo nenda shemu tofauti, je spidi itabaki hivyo? Yaani hata huo mji uliopo ukienda mtaa mwingine unaweza ukakuta kitu tofauti. Kama kwa halotel kuna kuchagua maeneo basi ni kwa kiasi kidogo sana au hakuna, hiyo ndo tofauti.
Kwa halotel spidi ya mtaani kwako iko sawa na spidi ya mtaa mwingine.
Hawajafunga 3G minara yao yote.
Kwenye district ambayo ninaisimamia mimi tokea tunaanza kuingia mikataba na wenye maeneo hadi kumaliza ujenzi wa towers, siyo minara yote tuliyofunga 3G japo minara mingi ni ya 3G.
Muda si mrefu utawekewa 3G.
Kuna kijiji kilikuwa ndani sana tumeweka tower hapakuwa na Airtel, Voda wala tiGo. Baada ya kuiwasha tower na wahusika kuwapelekea lines mnara ulijaa subscribers ndani ya siku tatu hadi makao makuu wakashangaa. Siku hizi tukienda kule wanatushangilia.
asante kwa kutuelimisha hilo maana wao wanajinasibu kuwa wamefunga 3g minara yote.
ina wateja wachache ila kuna jamaa yangu yupo kitengo cha optmization kaniambia hilo ndio lengo lao.
Hapa naangalia ligi ya uingereza kwenye laptop yangu kwa raha zangu, Asante halotel
kwani hao kina voda na tigo pia si wameamrishwa watenganishe vifurushi vya data na mb?
hapa huwezi ulaumu mtandao wowote ule mbaya wetu ni TCRA kinachotakiwa ni kuwahimiza warudishe mfumo wa zamani
na kama walikua na nia kweli hao Halotel basi hata hivyo vya mb tupu wangetupa mb nyingi lakini na wao wanakaba koo vile vile tena vifurushi vyengine wanakaba kuliko hao wazoefu. nikipata muda nitaeka comparison ya vifurushi vya mitandao yote.
ni nouma arifuLeo niliamua ninunue laini ya hawa jamaa nijaribu ubora wao kwenye internet kusema kweli wamekidhi vigezo sijawahi fikia speed hii kwenye modemu, shida vocha zao tu zinasumbua mpaka urushiwe.
nimeshindwa ku updload picha sababu ya matatizo ya jamii forums ila speed ni above 4.76Mbps ambayo sijawahi ipata kabisa kwa mitandao mingine.
NB: nimedownload movie ya the battle of stanligrad 386MB kwa dakika 7 tu.
Mkuu umejuaje kwa KODI na SportDeavil
Jamaa wanatisha sana Niko Rufiji huku Bungu Vodacom na Airtel Network hamna,Tigo EDGE hata uwe unatumia torch Kwa Voda haupati kitu
Ila hawa jamaa ni 3G na unakamua speed mpaka ya mwisho 19Mbps sema bila Unlimited hauchelewi sikia meseji yao inaingia
Hamna mtandao wa 3G wenye Unlimited ya Ukweli.mkuu meseji huwahi kuingia kwa kuwa speed yao ipo juu. ukitaka kufaidi vzr nunua unlimited bundle.
Acha kupotosha
Simu za 4G zipo na ili Upate 4G unaitaji Sim card ya 4G na Device ya 4G(simu ya 4G au Modem yenye uwezo wa 4G)
Na wala 64k sio kigezo cha line kuwa na uwezo wa 4G kuna line ni 64K na ni za 3G
Labda haukuelewa vizurioooops! basi tigo ndio walinipotosha...kumbe hawa jamaa ni wezi sasa nimegundua au uwezo wa customer care agents wao uko chini. tigo walinipotosha kwamba ili upate 4g unapaswa kuwa na laini ya 4g au u-upgrade laini ya kawaida hadi 64k. tigo ni mafisadi wa ku2pwa.
Hamna mtandao wa 3G wenye Unlimited ya Ukweli.
Hiyo meseji nayoisema ni ya Ku Limit Speed!
Sasa Unlimited yenye Limit ya Speed hiyo ni Unlimited au niku Misuse neno
mkuu UNLIMITED ya kibongo ina maana ya "MUDA wa MATUMIZI" wa bundle uliyojiunga...sio UNLIMITED SPEED! umeelewa? maana yake kama umeambiwa ni kwa matumizi ya saa 24 utatumia ndani ya muda huo. mitandao yote baada ya kutumia kiasi fulani cha bundle hutuma meseji ya kulimit spidi. kibongobongo hiyo ndio maana ya UNLIMITED. haya sasa niambie UNLIMITED ya huko ughaibuni inatafasiriwaje?
Labda haukuelewa vizuri
Kama una Line ya 3G unaweza kui Swap ikawa ya 4G au ukasajili line mpya!
Lakini ili utumie Line ya 4G unaitaji Kifaa chako kiwe na Uwezo wa 4G i.e Hauwezi Tumia 4G kwenye simu kama Samsung Galaxy pocket
Hawa jamaa wana customer suport namba ambayo iko reachable kwa mtandao mwengine? Maana nimenunua line yao mpaka leo inasema sijasajiliwa na hapa karibu hakuna duka lao.