Playboy
JF-Expert Member
- Aug 11, 2011
- 1,170
- 945
Kama kuna mfanyakazi wa halotel humu asome ujumbe huu awafikishie sijui ndio control center sijui ndio customer service center mtajua wenyewe.
SITAKI NA SITAKI NA NINAKEREKA NA MESSAGE ZENU ZA HALO SOKA KAAAAAHHHHHH[emoji16] [emoji16] [emoji16] yaani utazani simu yangu ni kwa ajili ya kutunza text zenu yaani kila baada ya dk 3 text.
Hamna service nzuri ya mteja kukutana na muhudumu akipiga namba ya huduma kwa wateja[emoji16] [emoji16] [emoji16] na mkiendelea mpaka kesho natupa line yenu, sitaki ujinga mimi, kila saa halo s0ka, halo soka.
SITAKI NA SITAKI NA NINAKEREKA NA MESSAGE ZENU ZA HALO SOKA KAAAAAHHHHHH[emoji16] [emoji16] [emoji16] yaani utazani simu yangu ni kwa ajili ya kutunza text zenu yaani kila baada ya dk 3 text.
Hamna service nzuri ya mteja kukutana na muhudumu akipiga namba ya huduma kwa wateja[emoji16] [emoji16] [emoji16] na mkiendelea mpaka kesho natupa line yenu, sitaki ujinga mimi, kila saa halo s0ka, halo soka.
Asalaam ndugu zangu! Poleni ni harakati za kulainisha vyuma kwa grease! mungu ni mwema kwa wale wenye changamoto za kimaisha mungu yu pamoja nanyi!
Bila kupoteza muda naomba niende kwenye hoja yangu moja kwa moja...... Nimekuwa mteja mzuri sana wa haloteli tangu mwaka 2016, Baada ya kuvutiwa na huduma zao ila kwa sasa naona mimi pamoja na kundi langu kubwa nililolishawishi tumewachoka kwani huduma zenu zimeoza na zinanuka!
kwanza mmekuwa na kawaida ya kuiba MB mfano kuna siku nilijinga 1 GB na kuingia whatsupp tu ila baada ya muda nakuta MB 400 Hivi kuna whatsupp ya kutumia MB 600 bila kudownload wala kuandika kitu na whatsapp yangu autodownload ipo off! nikawapotezea!
Juzi nikaweka vocha lakini kwa sababu nilikuwa busy nikashindwa kujiunga kifurushi chochote! lakini baadae kutaka kujiunga nakuta wamepunguza Tsh 50/- Nikaona sio mbaya ngoja niwaulize huduma kwa wateja hii kitu imekaaje? Ebhanaaa eee nilikutana na dada mmoja sijui alikuwa kagombana na bwana yake ananijibu kwa ukali na wakati hata hanijui! ananiambia kuwa nimejiunga halowin nikabaki nashangaa kwa sababu mambo ya bahati nasibu huwa sishiriki kabisa! nikawa namwambia bhasi naomba unitoe na hiyo huduma maana mimi siijui! alichonijibu ni kuwa halowin huwa haijiungi yenyewe utakuwa umeunga wewe hivyo na kutoa utoe wewe! kisha akakata simu kiukweli nilijisikia vibaya sana na huduma ya yule customer care!
Sasa leo ndio maamuzi ya kuukimbia huu mtandao pamoja na jopo langu umefikia na ninaahidi kufanya kampeni ya kuichafua haloteli ni kuwa iko hivi....... jana jioni nilinunua vocha nikaweka kwenye wallet! sasa asubuhi kama unavyojua sisi wanaume wa mikoani nikawasha pikipiki yangu nikavaa mabuti yangu na kuanza safari ya shamba! Bahati mbaya wakati wa kurudi mvua kubwa ilianza kunyeesha nipo njiani hakuna hata kwa kukujikinga! vitu vyote nilivyokuwa navyo vikalowa isipokuwa simu sababu huwa sibebi simu shamba! vocha ikalowa chapa chapa pia nilivyofika home nikaikausha ikakauka lakini kila nikikwangua ili niweke namba ule ukungu wa juu ukawa unatoka na namba! ikabidi nipige huduma kwa wateja sabau serial namba zilikuwa zinaonekana vizuri! safari hii mtoa huduma kwa wateja alinijibu vizuri tu akasema kwa sasa hawana huduma hiyo hivyo nifike halotel shop wanibadilishie vocha! na kwakua duka hilo lipo mtaani kwangu sikupaa shida nilifika fasta ila nilichokikuta kilinitia hasira sana! nilimkuta kijana bishoo namueleza shida zangu ma yeye naona kama ananifokea hivi kuwa kwanini nimelowesha vocha? mimi vocha za kubadilisha sina! nimewasaidia wengi sana hahaha! sikumjibu kitu nilichofanya niliitupa ile vocha yangu kwenye dust bin na kuondoka heri nusu shari!
Hayo ndiyo yaliyonikuta katila mtando wa halotel yapo mengi ila hayo ni kwa uchache! mimi naahidi kulala na ninyi halotel mbele!