Halotel mna tabia ya ajabu mno

Tyupa

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
802
653
Likiwa ni shirika kubwa la mawasiliano hapa nchini lakini haliendani kabisa na mambo wanayowafanyia wateja wake.

Katika huduma ya nipige tafu hapo ndipo Halotel wanapoonesha udhaifu wao.

Ikumbukwe kwamba mteja anapoomba huduma ya nipige tafu hua ni swala la dhalura ambalo mteja anahitaji wakati huo tu.

Lakini mara nyingi au mara zote unapoomba huduma hii ya nipige tafu badala ya kusaidiwa unajibiwa kwa sms majibu ya kihuni na ya ajabu kabisa.

Majibu yao hua ya nasema " huwezi kupewa mkopo hadi lini yako iwe imetumika kwa zaidi ya miezi mitatu ", wakati laini yako ina miaka kadhaa.

Maneno mengine ni " lazima uwe na salio kiasi fulani," wakati wewe huna hilo salio na ndo maana unaomba nipige tafu.Maneno mengine ni "lazima uwe umetumia kiasi cha sh,kama 3000 hivi kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Baada ya hapo hupewi mkopo wa nipige tafu na unakufa na shida yako.Kipindi ambacho wewe huna shida ya nipige tafu wao ndo hutoa idhini ya huduma hii.

Lugha ya maudhi kiasi hiki sielewi maudhui yake kwa wateja yana maana gani.

Hivi hakuna lugha nzuri ambayo inaweza kutumika badala ya hii ya kukejeli wateja?

Na kwa nini mteja anapoomba huduma ya nipige tafu hapati badala yake anaambulia lugha ya dharau na kejeli.Halotel kueni wastaarabu.
 
pole kaka,,ni kweli ulichosema ila jitahidi sana uwe unajiunga sms za mwezi angalau inapotokea huna salio la kupiga uwe na uhakika hata wa sms.

Voda tsh 2000/=30'dys
Tigo tsh 1500/=30'dys
Halotel&Aitel tsh 1000/=30'dys
 
Kwenye intanet sasa ndo balaa,unajiunga wanakaa kama dakika 10 ndo wanaruhusu mambo yaendelee,mkiendelea na tabia hii kalaini kenu ntakachoma moto nihamie mtandao mwingine..
 
Back
Top Bottom