Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kunani?

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,096
6,106
Wilaya ya Tunduru ni mojawapo ya wilaya za mkoa wa Ruvuma ikiwa mpakani mwa nchi ya Msumbiji. Nauliza hii halmashauri ina mkurugenzi kweli? Nauliza kwa sababu wakati tunasajiliwa km walimu wapya walioajiriwa mwezi wa 6 mwishoni tulifanyiwa mambo ya hovyo kweli.

Idara yao ya utumishi na ofisi ya mwanasheria wa Halmashauri ni wanyanyasaji na wala rushwa. Hawa watu wanatafuta kosa dogo sana ktkt majina, kwa mfano jina lako ktk kitambulisho cha Taifa limeandikwa Jenipha na ktk vyeti linasomeka Jenipher.

Afisa utumishi akiona tu hiyo tofauti hataki kuongea zaidi anakuambia tu nenda ofisi ya mwanasheria wetu. Ukiendelea kutaka kuja zaidi hakujibu, wamejaa kiburi na dharau.

Sasa ukifika ofisi ya huyo mwanasheria ni km mamba aliyetegea mdomo kusubiri samaki ammeze. Anakuambia lete Tshs 82,000/ ili nikuapishe na kusajili jina moja unalotaka kutumia bila hivyo hutasajiliwa.

Ukidai risiti anakuambia hii haina risiti. Tofauti ya majina ktk kitambulisho cha Taifa na ktkt vyeti limesababishwa na ukweli kuwa kule vijijini wenyeti wa vitongoji ndio walikuwa wanajaza fomu kwa niaba ya wananchi maana wananchi wengine hawajui kusoma na kuandika, hawa wenyeviti shule zao nazo ni changamoto hawawezi kujua tofauti kati ya Jenipher na Jenipha.

Kwanini wa-rely kwenye majina ya NIDA? ndio mwongozo wa TAMISEMI? Fikiria mtu umetoka Kagera hujanunua hata bakuli achilia mbali kitanda na godoro na nyumba ya kuishi hujui iko wapi.

Bado umlipe daktari wa serikali, ulipie kitambulisho na unakamuliwa Shs 82,000/. Watanzania wenzetu tunaomba tuambieni hii ni sawa?

Kwani hawa wanasheria wanalipwa mishahara kwa kazi gani? Hawa ni makatili wasio na chembe ya huruma. Halafu mara kwa mara Afisa utumishi hachoki kwenda kuchungulia ofisi ya mwanasheria, nafikiri alikuwa anaenda kucheki amekusanya kiasi gani. Jambo la pili mpaka leo wiki ya tatu hatujapewa hela ya kujikimu, hatujui tutalipwa lini na ni kiasi gani.

Nna taarifa halmashauri zingine zimeshalipa, viwango ni kutegemeana na kiwango chako cha elimu yaani Grade A, Diploma au Degree. Na mshahara hapa tunaambiwa na waliotutangulia ni mpaka baada ya miezi mitatu wakati halmashauri zingine unalipwa mwezi huohuo ulioajiriwa.

Ndiyo maana nikauliza hapa kuna mkurugenzi kweli au anashirikiana na hawa subordinates wake kutunyanyasa? Mi nimetoka kanda ya ziwa nauliza au Tunduru haiko Tanzania?

Mama Ummy Mwalimu we ni jembe tunakufahamu tunaomba utupie jicho halmashauri hii tumeishiwa hatuna hela hata ya kula tunaishi nafuu ya wakimbizi maana wao wanasimamiwa na shirika la kimataifa la wakimbizi wanapata chakula na malazi.

Ahsanteni kwa muda wenu
 
Hongera mkuu kwa kuleta kero yako Jamvini.Subiri kitambo kidogo tu kero yako itatatuliwa.
 
Nenda TRA kanunuale stika mbili (tsh 500),then nenda mahakamani na vyeti vyako na hiko kitambulisho cha taifa,kaape kutumia majina yote,hapo utapigwa sh 10,000/=
 
Msomi gani unalalamikia Ujinga, kwanini ukae na vyeti ambayo majina yanapishana? Ina maana tangu uandikishwe NIDA mpaka umeomba ajira mpaka siku unaenda kuajiriwa ulikuwa wapi kurekebisha hizo kasoro?

Watu kama nyie mngekuwa hata hizo kazi mnafukuzwa maaana inaaashiria jinsi gani hamna umakini katika mambo yenu. Mbaya zaidi hata mshahara watakubania miezi sita kuupata wakisoma haya malalamiko yako. Mkuu nadhani wewe pia ni SHABIKI WA YANGA ettii😂😂😂
 
we ni popoma kwl ushabiki wa Yanga unatoka wapi hapa. Watu tunalilia mkate we unaongelea ushabiki umevimbiwa siyo? Nazungumzia rushwa kuliwa Shs 82,000/ bila uhalali au we ndioyule uliyechukua pesa zetu? Maana hii povu siyo ya mtanzania wa kawaida. Itakuwa ni weweeeee!!!! na utazitapika subiri muda utaongea. Shenz type
 
we ni popoma kwl ushabiki wa Yanga unatoka wapi hapa. Watu tunalilia mkate we unaongelea ushabiki umevimbiwa siyo? Nazungumzia rushwa kuliwa Shs 82,000/ bila uhalali au we ndioyule uliyechukua pesa zetu? Maana hii povu siyo ya mtanzania wa kawaida. Itakuwa ni weweeeee!!!! na utazitapika subiri muda utaongea. Shenz type
Basi basi mwalimu punguza hasira! Usije ukamlipua huyo Mwanasheria kwa petroli! Yaani mnaanza kuibiwa mapema hivi!!

Bado CWT wanasubiria tu salary slip zitoke ili waanze na wao kuwaibia zile 2% za basic salary zenu! Bado Bayport na Platinum hawajaja kuwashawishi mkope ndani ya masaa 24!!


Aisee safari ni ndefu!!
 
Back
Top Bottom