Halmashauri ya wilaya MISSENYI yagoma kuwakopesha hata sumni walimu ajira mpya, walimu wafa njaa

MTABO

Member
Mar 6, 2014
95
57
Katika hali isiyo ya kawaida, Halmashauri ya wilaya MISSENYI imegoma kuwakopesha walimu ajira mpya pesa za kijikumu, hali inayopelekea walimu hao kulia njaa kila siku. Mwalimu wakiomba shule iwakopeshe, shule nazo kupitia kwa wakuu wa shule zinasema hazina pesa za kuwapa walimu hao, huku wakitoa sababu kua pesa za elimu bure zinakuja zikiwa zimepangiwa matumizi moja kwa moja kutoka juu.

Viongozi wa hii Halamshauri wanawaambia walimu hao kua waombe pea kwao ili wajikimu, na kwamba kama hawana namna basi waache kazi. Sasa walimu hao wameanza kuishi kwa kutegemea kwao na wale wasio na uwezo kwao, wameanza kulala au kushinda na njaa kabisa.

Tunaomba Mamlaka za juu, ziingilie kati hili swala. Haiwezekaani Halamashauri moja tu kati ya zote za Tanzania ndio ishindwe hata kuwakopesha walimu wa ajira mpya ambao kwa idadi yao ni 15 tu. Huku ni kuanya kazi kwa mazoea.

Ukiwaangalia hawa walimu wapya ni wanyonge muda wote, na sijui kama Taifa letu linafaidi mazuri yote kutoka kwa hawa walimu wanaoteswa na hii Halmashauri katili.
 
Na mshahara wa mwezi huu hakuna! Ndo mhubiri bajeti ipitishwe! Mshahara ni hadi mwishoni mwa mwezi Julai! Kazi kwelikweli
 
Back
Top Bottom