Halmashauri ya Ushetu - Kahama wastaafu wanaonewa sana

Halmashauri ya Ushetu - Kahama wastaafu wanaonewa sana

WAMGANDA

Member
Joined
Nov 19, 2016
Posts
10
Reaction score
7
Kama title inavyosomeka, katika halmashauri ya Ushetu iliyoko ndani ya Wilaya ya Kahama Wastaafu wa kada mbalimbali wamejikuta wako matatani kwa mtindo ufuatao:

Baada ya kusitafu almost wote waliendelea kuingiziwa mishahara kama kawa. Kutokana na kucheleweshewa Malipo yao ya Pensheni walidhani kuwa labda ni utaratibu wa kawaida wa serikali kuwapunguzia makali ya maisha wakati wakisubiri staiki zao, baadae mishahara ilikata na hawakuulizwa chochote.

Mziki na kimbembe kimeanza mapema mwaka huu, wanatuhumiwa kuwa wameiibia serikali kwa mtindo wa ajabu kidogo kwani baadhi ya maofisa wamekuwa wakiwapigia simu au kutuma SMS na kuwapiga threat kwamba ni wezi na wamejipanga kuwashughulikia, zaidi wamekuwa wakiwaita mmoja au wawili wawili kuwadai pesa hizo in a more personal way that organizational procedures! Hii inazua mashaka kwa wazee hawa whether the issue is official or ni plans za maofisa hao.

Taarifa za ndani kabisa ya halmashauri zinaonesha kwamba hakuna kikao chochote ambacho wamekaa na kuamua kuwasulubu hawa waalimu wasitafu ambao wengi wao walishamaliza pesa na wanahangaika na magonjwa ya uzeeni.

Pia kuna walioandika barua ya kulalamika kuendelea kulipwa mishahara na wakaomba kusitishiwa lakin kwa uzembe na jeuri mkaendelea kuwapa na barua zipo.

Itakuwa vyema kama wamo humu wanipe ufafanuzi wa mambi yafuatayo.

1. Kosa hasa ni la nani? Kati ya aliyeingiza pesa kimakosa (kizembe) na aliyepokea akijua ni utaratibu wa kawaida wakati wa kusubiri pensheni.

2. Kuwaita mmoja mmoja ina lenga nini hasa au ndo divide and rule method?

3.Je? Kwa wasitafu ambao tayari wameaga dunia muna utaratibu gani?

4. Upande wenu nyinyi mliofanya uzembe munawajibikaje kabla ya kuwawajibisha hawa vikongwe?

5. Kikao gani hapa halmashauri kimeadhimia kufuatilia jambo hili? Tena kwa njia za kienyeji kabisa?

6. Mnafahamu kuwa hawa wasitaafu hadi wanaondoka kwenye utumishi wa umma walikuwa wanaidai serikali pesa kiasi gani? Je walilipwa au walisamehe?

7. Je, tangia wastaafu kazi zao mmewarudusha makwao sambamba na kuwalipa masurufu ya njiani kama sheria inavyotaka?


RAI:
Mwisho ningependa kutoa rai kwa watumishi wa halmaahauri hii changa ya Ushetu waache Mara moja kuwafanyia umafia wazee hawa. Pia kama nikufatilia waliweke wazi maaana usiri unatia mashaka na walakini mkubwa.Pia serikali ijitafajali na kuona kama ni haki kwa wazee hawa kusumbuliwa kiasi hiki.

Chanzo cha habari ni mimi. Maana nipo hapahapa halmashauri na naona kinachoendelea na wizi nothing more.

WAKUU ASANTENI.
 
Back
Top Bottom