Halmashauri ya manispaa ya Geita kuanzishwa

Halmashauri ya manispaa ya Geita kuanzishwa

profmazungu

New Member
Joined
Aug 10, 2018
Posts
3
Reaction score
3
Geita. Halmashauri ya mji wa Geita imeongeza kata tatu na kuifanya kuwa na kata 16 ikiwa ni mchakato wa kutaka ipande hadhi na kuwa manispaa.
Kata zilizoongezwa ni Nyanza yenye mitaa mitano, Mwatulole yenye mitaa mitano na kata ya mkolani.
Akizungumza katika kikao maalum cha ushauri cha wilaya (DCC) jana Julai 26, 2018 mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi amesema moja ya kigezo kinachotakiwa na Tamisemi ni kuwa na kata 15 na kwamba awali walikuwa na kata 13 na sasa zimeongezeka na kuwa 16.
“Kigezo cha eneo, idadi ya watu na uwezo wa kujitegemea halmashauri hiyo inakidhi, mapendekezo hayo yatapelekwa Tamisemi ili waweze kuidhinisha na kutimiza kiu yao ya kuwa manispaa,” amesema Kapufi.
 
kapufi kitambo sana ametumbuliwa, mkuu Wa wilaya ni Mwl Maganga.
 
Back
Top Bottom