Halmashauri ya Kinondoni yapata tuzo ya Halmashauri bora Afrika

Halmashauri ya Kinondoni yapata tuzo ya Halmashauri bora Afrika

Hiyo hapo juu ni ndani ya kinondoni tena Msasani sasa hivi!
 
[h=1]MEYA MWENDA WA KINONDONI ASHINDA TUZO YA MEYA BORA AFRIKA[/h] http://ift.tt/1zL2xn7
Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam ​

​
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda ameshinda Tuzo ya Meya Bora katika Bara la Afrika katika kundi la Majiji ya Kati na kuyabwaga majiji mengine mbalimbali. ​

​
Tuzo hizo zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (The United Cities and Local Government of Africa- UCLGA) na kupewa jina la Rais wa Angola ‘President Jose Eduardo Dos Santos- Africa Mayors Award’ ni za mara ya kwanza kufanyika Barani Afrika. ​

​
Tofauti na Tuzo za Tanzania, Tuzo hizi za Afrika zinahusika na Mamlaka ya miji tu. ​

​
Tuzo hizi zilikuwa ni katika makundi matatu ambayo ni Tuzo za Majiji Makubwa (Large Size Cities), Tuzo za Majiji ya Kati (Medium Size Cities) na Tuzo za MajijiMadogo (Small Size Cities). ​

​
Tuzo za Majiji Makubwa (Large Size Cities) zimekwenda jijini Accra, Ghana wakati zile za Majiji madogo zimechukuliwa na Praia katika visiwa vya Cape Verde. ​

​
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilishiriki mashindano ya Tuzo za Meya (Halmashauri Bora za Afrika baada ya kushinda Tuzo za Meya/ Halmashauri Bora Tanzania zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT). ​

​
Miradi iliyoshindanishwa kutoka Manispaa ya Kinondoni ni pamoja na ukusanyaji wa mapato na kituo cha Mabasi Sinza. Hata hivyo Manispaa ya Kinondoni ilipimwa katika vigezo vyote vilivyoanishwa na UCLGA. ​

​
Zawadi zilizotolewa ni kikombe, Cheti na Fedha tasilimu kiasi cha Dola za Kimarekani 100,000 ambazo sawa na shilingi milioni 200. ​

​
Majiji mengine yaliyoshinda yalipata Dola za Kimarekani 200,000 (Sawa na shilingi Milioni 400) kwa Miji Mikubwa na Dola za Kimarekani 50,000 (sawa na shilingi milioni 100 kwa Miji midogo IMG_20150505_101714.jpgIMG_20150505_101720.jpgIMG_20150505_101726.jpgIMG_20150505_101753.jpgIMG_20150505_101759.jpg
 
Manispaa ya Kinondoni ni kweli wanajitahidi, hata kule Masaki wamejenga apartments nyingi tu za kupanga ambazo kwa namna moja zinaongeza mapato kutokana na kodi za pango...
 
Hakuna mguu mfupi usiokanyaga chini. Msishangae! Kinondoni iekanyaga chini. Ilala na Temeke wanaelea!!
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1431204339.732332.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1431204339.732332.jpg
    54 KB · Views: 49
  • ImageUploadedByJamiiForums1431204405.533581.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1431204405.533581.jpg
    67.7 KB · Views: 51
Back
Top Bottom