Halmashauri Tandahimba yapata hati safi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Halmashauri Tandahimba yapata hati safi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by AridityIndex, May 5, 2011.

 1. A

  AridityIndex Senior Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  na Khamis Mvulla, Mtwara  HALMASHAURI ya Tandahimba mkoani Mtwara imepata hati safi ya mahesabu baada ya ukaguzi wa Tamisemi.

  Hayo yalisemwa na Abdallah Njovu, katibu wa baraza la madiwani na pia mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo katika kikao maalumu cha baraza la madiwani mwishoni mwa wiki.

  Njovu alisema hati safi waliyoipata ni ya mwaka 2009-2010 baada ya ukaguzi wa hesabu ya Tamisemi na kuridhika na matumizi ya fedha za miradi zilizopelekwa katika halmashauri hiyo na kutumika vyema bila ubadhirifu na kuridhika na miradi husika iliyotekelezwa kwa viwango vinavyokubalika.

  Aidha Njovu aliwashukuru madiwani pamoja na wakuu wa idara na vitengo kwa kusimamia vyema miradi yote na kupelekea kupata hati safi.
  Katibu huyo wa baraza la madiwani alisema kuwa katika fedha za makusanyo ya ushuru wa halmashauri imekusudia kumaliza shida ya madawati ya shule za msigi 116 mwaka huu ambapo zimetengwa jumla ya shilingi 242,775,000 kwa kutengeneza madawati 4,866. shule zitakazonufaika na madawati hayo ni za tarafa ya Mahuta, shule 42; tarafa ya Litehu, shule 30; na tarafa ya Namikupa, shule 44.

  Ni mara ya pili halmashauri ya Tandahimba inapata hati safi kufuatana na utekelezaji bora wa miradi na utumiaji mzuri wa fedha za miradi husika ya maendeleo wilayani humo.
  Njovu alisema kuwa katika bajeti ya mwakani halmashauri yake ina mpango kabambe wa kuanzisha kituo cha redio FM abacho kitakuwa kichocheo kwa maendeleo ya watu wa Tandahimba.

  Source: Tanzania daima. 5/05/2011
   
 2. A

  AridityIndex Senior Member

  #2
  May 5, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera sana viongozi na wananchi wa Tandahimba, kwa muda mrefu maendeleo yenu yamekuwa yakikwamishwa na viongozi wabinafsi, wenye husda na wasiotakia mema maendeleo ya wananchi wa kusini waliojaa kashfa badala ya kuwa wabunifu wa mbinu za kukabiliana na uduni wa maisha uliopo.

  Hongera Abdalah Njovu (Mkurugenzi), hongera kwa kufikiria kuanzisha kituo cha redio, ushuri wangu ni kwamba kituo kisitumike kupiga rumba tu badala yake kisaidie kusambaza taarifa za maendeleo pamoja na kutoa elimu.

  Ni vema pia mh. Mkurugenzi mkaimarisha mfuko wa elimu kwa kuwasaidia vijana wanaoonyesha jitihada katika elimu kufikia elimu ya juu yaani chuo kikuu bila kusahau kujenga daraja kwa kuanzisha shule za hadi kidato cha sita angalau 2 ili zipokee wanafunzi kutoka shule zetu za kata. achana na mawazo ya kusubiri mipango ya kitaifa kwani wakati wote mnajua kuwa tumeishia kuwa wahanga na kusahauliwa au kudharauliwa.

  Mdau mzawa wa Tandahimba
   
Loading...