Halmashauri: Moja ya chanzo cha umasikini kwa taifa

Halmashauri: Moja ya chanzo cha umasikini kwa taifa

samurai

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2010
Posts
11,478
Reaction score
24,250
Hii hoja haihitaji maneno mengi wala ubishi, ukweli uko wazi kabisa.
TANZANIA kwa sasa ni moja ya nchi masikini sana duniani na watu wake wengi kwa asilimia kubwa huishi katika umasikini mkubwa.

Inatia uchungu sana kuambiwa eti nchi yenu ipo kundi la nchi masikini kabisa na ombaomba huku mkijua kabisa hali hii husababishwa na wapumbavu wachache kwa maslahi binafsi na vimada wao.

Kiukweli moja ya chanzo kikuu cha umasikini wa taifa hili ni halmashauri zetu, watendaji wa halmashauri zote wamechangia kwa kiasi kikubwa umasikini huu, sio wakati tena wakucheka na hawa wapumbavu bali ni wakati wakuwajaza kwenye jela zetu, kuwafilisi na mwisho kuwaua kabisa.

Maneno mengi hatuyahitaji tena na tuko nje ya muda, ni wakati sasa wakutoa adhabu na hakuna adhabu nyingine zaidi ya kuwafilisi, kuwafunga jela za pembezoni na adhabu kali.
Vyomba vyote vya usalama ni mali ya serikali, Mh Rais ndio mtoa amri, sasa nini tunashindwa kuadhibu asilimia ndogo ya wapumbavu wanaoleta huu mkwamo?, watu zaidi ya mil 45 tunashindwaje na hawa wapumbavu wachache mpaka Taifa linakuwa maskini hivi.

INAKERA, eti tunaitwa moja ya taifa masikini duniani nasi tumekaa tu tumeridhika, huku wengine eti wanajiita wasomi na videgree, vimasters, viphd na wengine maprofesa sasa sijui unajiitaje msomi huku taifa lako ni masikini.
 
kwani hao wafanyakazi wa Halmashauri ndio matajiri,we kweli hata hujui flow ya watu wengi kuwa masikini inaanzia wapi
 
Mleta maada anayo hoja, msikimbilie kumshutumu hasa kama hamuzijui halmashauri/majiji. Kwa ufupi halmashauri utendaji ni zero, labda kwa Dr Magufuli ndiyo watabadilika, ila zimejaa watu wanaooneana wivu wao kwa wao. Yaani ni uhuni, wizi na ubunifu ni hakuna, wanawaza posho tu na kuiba.
 
Kuna kiongozi flani slisema mchwa wanaotafuna kodi zetu wako halmashauri na kuahidi angewashughulikia ktk utawala wake. Lkn kipindi chake ndy halmashauri zilizidi kwa bahirifu
 
Ungeainisha ni kwa namna gani halmashauri zinaleta umaskini na kutoa mifano.

Ndio maana nimekwambia hili halihitaji maneno mengi, kiufupi haya maneno na ujuaji ndio vimetufikisha hapa, yaani unataka utafuniwe kila kitu, nenda kapitie ripoti za maCAG wote waliowahi kukalia hicho kiti...
 
Hamna kitu hapo.Aweke mifano badala ya shutuma zisizo na kichwa wala miguu
Mifano ni mingi tu,mama kabeba karai la mchicha kuelekea sokoni kabla hajauza anatozwa ushuru na mara nyingi anapewa risiti ya malipo fake.Hela yake haendi kwenye mfuko wa kuimarisha huduma anatarajia toka Halmashauri
 
kwani hao wafanyakazi wa Halmashauri ndio matajiri,we ******** kweli hata hujui flow ya watu wengi kuwa masikini inaanzia wapi

Uwongo,ujuaji,wizi,unafiki ndio mitaji ya watanzania wengi, nimesema halmashauri ni moja ya chanzo cha umasikini wa watanzania, kama umeelewa tafsiri vizuri ni kwamba kuna Vyanzo vingi, na halmashauri ni moja ya chanzo.
Inawezekana husomagi hata ripoti za CAG na kuona hela nyingi zinapotelea wapi, miradi mingi huanzia huko halmashauri na serikali inachanel pesa nyingi sana huko kwenye halmashauri matokeo yake zinaenda kupigwa huko...
 
Wafanyakazi wa Halmashauri wanawaza posho na wizi muda wote..Utendaji ni ziro kabisa
 
  • Huwezi kuwa mtumishi wa halmashauri ukamiiki nyumba zaidi ya mbili na magari zaidi ya moja huku ukiwa na miaka 10 kazini na huna mradi wowote, mkopo benki yoyote na mshahara wa halmashauri wote tunaujua. Tuishi kwa uhalisia na tuwe wakweli, tusiwe na tamaa ya utajiri kwa kuiba mali ya umma.
 
Mleta maada anayo hoja, msikimbilie kumshutumu hasa kama hamuzijui halmashauri/majiji. Kwa ufupi halmashauri utendaji ni zero, labda kwa Dr Magufuli ndiyo watabadilika, ila zimejaa watu wanaooneana wivu wao kwa wao. Yaani ni uhuni, wizi na ubunifu ni hakuna, wanawaza posho tu na kuiba.
Kwani si ni DK Magufuli amepeleka huko MADED wasomi na wenye uwezo mkubwa? Mnalalamika nini tena?
 
Acha kutukana wenzako. Jikite kwenye chanzo na siyo matusi.

Ukweli Lazima usemwe hakuna aliyetukanwa hapo, taifa hili ni la watanzania wote sio la watu fulani peke yao. Nimesema halmashauri ni moja ya chanzo cha umasikini wa tanzania, inawezekana kukawa na vyanzo vingine ambavyo labda nawe unavijua. Wizi wa mali ya umma kwa manufaa binafsi na vimada haukubaliki maana huleta umasikini mkubwa kwa watanzania walio wengi huku wewe mmoja ulinufaika. Tunafanye kazi kwa bidii tulijenge taifa tuache wizi, ukitaka kuishi vizuri kawe mfanya biashara na si kujificha kwenye mali za umma..
 
Mhuu mtoa mada nadhani amekurupuka., habari yako hata kama inaukweli mimi sijaona ulichoandika. Eleza kivipi hizi halmashauri zina sababisha umaskini toa mifano halisi ili tuanzie hapo kuchangia mada na kuongeza ishu nyingine ambazo na sie tunaziona.
 
Kwani si ni DK Magufuli amepeleka huko MADED wasomi na wenye uwezo mkubwa? Mnalalamika nini tena?
Hatulalamiki ila uwepo wa halmashauri nyingi kumerudisha maendeleo nyuma. Pamoja na wasomi hao ma DED kumbuka maafisa mipango, wachumi, mipango miji ni wale wale wasiojituma na wezi. Yaani kwa ufupi panahitajika kufumilwa tena hasa muundo wa utumishi wa halmashauri. Mfano si ajabu mchumi kuwa hajui miradi inayoendelea kwenye halmashauri yake. Si kama enzi zile siku hizi wachumi kazi yao ni kukaa tu ofisini wala hawafuatilii miradi unakuta miradi hewa kibao. Na kibaya zaidi wafanyakazi wengi wa halmashauri siyo wabunifu wana akili mgando. Mimi nasema hayo kwa sababu nawajua. Chukua mfano mwingi, halmashauri kwa asilimia kubwa au 100% hazina policy ya majengo/miji/ etc. Unakuta wanagawa viwanja then hata huduma za jamii hazipelekwi, kila mtu anajenga anavyotaka, kumbi za starehe hazijengwi kuzuia sauti kutoka nje, nyumba hazina mpangilio wa rangi, yaani ni ovyo ovyo. Na kwa kutegema hizi halmashauri hatutakuja kufikia ulaya standard zao
 
Back
Top Bottom