figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Halmashauri mkoani Mara zagomea fedha za mrabaha kutoka mgodi wa CATA Mine kwa kukiuka mkataba.
Picha inayoonekana hapo juu kwa hisani ya Mtandao.
Uongozi wa Halmasdhauri mbili za mkoa wa Mara,zimekataa kupokea kiasi cha Shilingi Milioni 40 kama mrabaha kutoka Mgodi wa dhahabu wa CATA Mine kwa madai ya kukiukwa kwa mkataba uliowataka kulipwa dola laki tano kama mrabaha kwa Halmashauri hizo za butiama na musoma vijijini.
Hatua hiyo imechukuliwa na viongozi wa halmashauri hizo mbili za musoma vijijini na Butiama ulipo mgodi huo, ikiwa ni siku moja tu baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kuagiza kupitiwa upya kwa mikataba yote ya sekta ya madini katika kuhakikisha raslimali hiyo inawanufaisha watanzania.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Butiama Bi. Annarose Nyamubi,amewaagiza madiwani hao kuchukua hatua ya kudhibiti mianya yote ya upotevu wa fedha ili kuhakikisha fedha zinazopatikana zinatumika kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
Chanzo: ITV