‘Halmashauri Ilala hauhisiki kuanguka jengo la ghorofa 16’

‘Halmashauri Ilala hauhisiki kuanguka jengo la ghorofa 16’

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
[h=2][/h]
MEYA wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, amesema halmashauri hiyo haihusiki na tukio la kuanguka kwa jengo la ghorofa 16 lilitokea wiki iliyopita na kuua zaidi ya watu 30. Akizungumza kwenye kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo jana, alisema halmashauri hiyo haina mamlaka ya usimamizi wa masuala ya ujenzi.

“Kutokana na taratibu zilizokuwa zimezoeleka tangu huko nyuma usimamizi wa shughuli za ujenzi mjini zimeonekana kuwa mamlaka ya usimamizi ni halmashauri ya mji, manispaa au jiji husika na siyo wadau wengine.

“Kwa ujumla dhana hii siyo sahihi hata kidogo. Wadau katika sekta hii ni wengi ambao wanapaswa kusimamia shughuli zote za ujenzi pamoja na ubora wa kazi zinazofanywa na wakandarasi, wataalamu washauri kwa maana ya wahandisi na wasanifu majengo,” alisema.

Hadi sasa watu tisa wamekwisha kukamatwa kuhusuaiana na tukio la kuanguka jengo hilo, wengi wao wakiwa ni maofisa wa Halmashauri ya Wilaya ya |Ilala. Hao ni Mhandisi Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Ogare Sallu,Mhandisi wa Majengo, Godluck Mganga, Mkaguzi wa Majengo Wilbrod Mulyagusu na Vedasto Ferdnand ambaye ni Mchambuzi wa Ubora na Gharama za Ujenzi.

Silaa alisema kazi kubwa ya halmashauri ni kufuatilia kama muombaji anajenga kama alivyoomba katika mchoro iliyopitishwa.

“Kwa mantiki hiyo halmashauri haina mamlaka ya kusimamia majengo makubwa iwe ya umma au ya binafsi,” alisema Silaa.

Silaa alisema mujibu wa sheria, kuna taasisi mbalimbali zinazohusika ambazo ndizo zimekabidhiwa mamlaka ya kusimamia shughuli zote zinazohusiana na masuala ya ujenzi.

Alizitaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni Bodi ya Wasanifu Majengo ambayo ilipewa majukumu ya kusimamia shughuli na utendaji kazi wa wasanifu majengo, kukagua shughuli zote za ujenzi na kuhakikisha kuwa kazi ya ujenzi inafanywa na mtu aliyesajiliwa.

“Bodi ya Usajili wa Wahandisi ambayo ina kazi ya kufuatilia na kusimamia shughuli na utendaji kazi wa wahandisi ikiwa ni pamoja na kampuni zinazofanya kazi ya utaalamu, na Bodi ya Wakandarasi (CRB) ambayo inasimamia usalama mahali pa kazi na kusimamia miradi ya ujenzi kwa kutoa kibali na kusajili,”alisema Silaa.
 
Asante kwa Taarifa basi tutaendelea kuwasaka wanaouhusika.popote walipo wajitokeze.
 
[h=2][/h]MEYA wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, amesema halmashauri hiyo haihusiki na tukio la kuanguka kwa jengo la ghorofa 16 lilitokea wiki iliyopita na kuua zaidi ya watu 30. Akizungumza kwenye kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo jana, alisema halmashauri hiyo haina mamlaka ya usimamizi wa masuala ya ujenzi.“Kutokana na taratibu zilizokuwa zimezoeleka tangu huko nyuma usimamizi wa shughuli za ujenzi mjini zimeonekana kuwa mamlaka ya usimamizi ni halmashauri ya mji, manispaa au jiji husika na siyo wadau wengine. “Kwa ujumla dhana hii siyo sahihi hata kidogo. Wadau katika sekta hii ni wengi ambao wanapaswa kusimamia shughuli zote za ujenzi pamoja na ubora wa kazi zinazofanywa na wakandarasi, wataalamu washauri kwa maana ya wahandisi na wasanifu majengo,” alisema.Hadi sasa watu tisa wamekwisha kukamatwa kuhusuaiana na tukio la kuanguka jengo hilo, wengi wao wakiwa ni maofisa wa Halmashauri ya Wilaya ya |Ilala. Hao ni Mhandisi Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Ogare Sallu,Mhandisi wa Majengo, Godluck Mganga, Mkaguzi wa Majengo Wilbrod Mulyagusu na Vedasto Ferdnand ambaye ni Mchambuzi wa Ubora na Gharama za Ujenzi.Silaa alisema kazi kubwa ya halmashauri ni kufuatilia kama muombaji anajenga kama alivyoomba katika mchoro iliyopitishwa.“Kwa mantiki hiyo halmashauri haina mamlaka ya kusimamia majengo makubwa iwe ya umma au ya binafsi,” alisema Silaa.Silaa alisema mujibu wa sheria, kuna taasisi mbalimbali zinazohusika ambazo ndizo zimekabidhiwa mamlaka ya kusimamia shughuli zote zinazohusiana na masuala ya ujenzi.Alizitaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni Bodi ya Wasanifu Majengo ambayo ilipewa majukumu ya kusimamia shughuli na utendaji kazi wa wasanifu majengo, kukagua shughuli zote za ujenzi na kuhakikisha kuwa kazi ya ujenzi inafanywa na mtu aliyesajiliwa.“Bodi ya Usajili wa Wahandisi ambayo ina kazi ya kufuatilia na kusimamia shughuli na utendaji kazi wa wahandisi ikiwa ni pamoja na kampuni zinazofanya kazi ya utaalamu, na Bodi ya Wakandarasi (CRB) ambayo inasimamia usalama mahali pa kazi na kusimamia miradi ya ujenzi kwa kutoa kibali na kusajili,”alisema Silaa.
sasa hao walokamatwa amboa nimewawekea blue wana kazi gani manispaa???au kukagua majengo ya ofisi zao?Kwenye red ndo ananiacha HOI maana kama wao wanatoa kibali,je walifatilia kujua kama idad ya ghorofa ni sahihi?
 
Wao ndiyo wanatoa kibali cha ujenzi, hawawezi kukwepa hili!
nimeshangaa shana mgoshi,yani jeri shilaa anakanusha kwamba manishpaa haihushiki?nkati vibai wanatoa wao,,,,,taari washaanza kuruka kimanga,na huyu shlaa anaanza kuruka kimanga maana ana agenda yake ya 2015 ya ubunge wa Ilala,,,,,shasha mi namshaui kuwa ashiishemee manishpaa n'goshi
 
sasa hao walokamatwa amboa nimewawekea blue wana kazi gani manispaa???au kukagua majengo ya ofisi zao?Kwenye red ndo ananiacha HOI maana kama wao wanatoa kibali,je walifatilia kujua kama idad ya ghorofa ni sahihi?

Yap, nadhan huyo Silaa angetafakar haya kabla asingekurupuka kulopoka huo utumbo wake.

Huu sio muda wa kukanusha, ni muda wa kuwajibishana na kuwajibika akiwemo yeye mwenyewe.

Kama hawahusik, kwanin wamekamatwa.?? Yupo tayar kwenda kuwatetea mahakaman, kuwa hawahusiki??
 
kazi ya manispaa ni kutuma mgambo kukamata mamantilie na wamachinga! Asante meya!
 
Mbona anajichanganya huyu tozi? Kunatofauti ya Kusimamia na Kufuatilia?
Kama Halmashahuri haihusiki mbona wafanyakazi wake wapo ndani saa hizi?
 
Back
Top Bottom