Halmashauri 688 vinara wa matumizi mabaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Halmashauri 688 vinara wa matumizi mabaya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 7, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Naibu Waziri wa wizara hiyo, Agrey Mwanri.  Winara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), imesema imebaini matumizi mabaya ya fedha katika halmashauri 688 nchini.
  Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Agrey Mwanri, alipokuwa akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma.
  Alisema wakurugenzi kadhaa wamewekwa ndani kutokana na tuhuma hizo na kwamba fedha nyingi zimetumika vibaya kupitia idara za ugavi na manunuzi.
  Alisema kupata cheti kisafi cha ukaguzi wa mahesabu si kwamba kuna matumizi mazuri ya fedha katika halmashauri zote bali ni kuweza kuweka mahesabu vizuri
  Aliwataka madiwani na viongozi wengine wa halmashauri hiyo kumtumia mkaguzi wa ndani wa mahesabu ili kubaini matumizi na mapato katika halmashauri zao.
  Alizitaja njia za kugundua ubadhilifu kuwa ni kusoma na kuhoji ripoti za kila miezi mitatu za mahesabu zinazotolewa na mhasibu wa ndani.
  Mwanri alisema idara ya ugavi na manunuzi katika halmashauri ndizo zimekuwa zikipokea fedha nyingi kuliko idara nyingine na kwamba asilimia 70 ya fedha zinazotumwa katika halmashauri za wilaya zimekuwa zikienda katika idara hiyo.
  Alisema jinsi ya kugundua kama kuna mchezo mchafu umetendeka ni kuitishwa kwa vikao vingi vya dharura katika halmashauri.
  Alisema vikao vya dharura huwa havina ajenda ambazo zinajadiliwa na hivyo ni vigumu kwa diwani kuhoji hoja yoyote inayohusiana na matumizi ya fedha.
  Alisema wakati mwingine idara ya ugavi na manunuzi, imekuwa ikivuta muda ili kuwawezesha viongozi wa halmashauri kusahau na baadaye kutangaza upya tenda.
  Mwanri alisema njia hii hutumika wakati wanapoona mtu waliyepatana naye hakuweza kufikia kiasi ambacho kinakubalika katika ugawaji wa tenda.
  Alisema kwa kawaida wanaocheza mchezo huo, wamekuwa wakifungua tenda za watu ambao hawajaingia nao njama ya kugawana fedha na kugundua wametenda kiasi gani.
  Alitaja eneo jingine ambalo linakuwa na matumizi mabaya ya fedha ni katika ujenzi ama ukarabati wa barabara, ambapo baadhi ya watendaji wasiowaaminifu hutengeneza barabara zisizo imara.
  Naye Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Lembris Kipuyo, alisema halmashauri hiyo imeidhinisha kutumia Sh. 3,861,999,000 kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sidhani kaa idadi ya halmashauri inafikia 600.
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  yeah ni kweli hazifiki idadi hiyo zipo 114 kama kama zimezidi ni chache zilizoanzishwa sasa hv!
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tazama hizo pesa ni total amount ndio unaweza kusema kwa kiasi gani Taifa letu linapoteza pesa katika uchumi wetu
   
Loading...