Halimashauri ya Kinondoni, Okoeni biashara za MWENGE, la sivyo serekali itapoteza mapato makubwa sana

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
Unaambiwa ukistajabu ya musa utaona ya firauni, Hivi ndio naweza kusema ukifanikiwa kupita eneo la mwenge jioni hii.
Nakumbuka rais aliruhusu machinga wafanye biashara zao, Lakini alitadharisha kutokubugudhi walipa kodi wengine.
Sijajua ni kiongozi gani karuhusu barabara ya mwenge sokoni kugeuzwa soko la wamachinga, Lakini kwa akili ndogo tu aliyefanya hivyo ni mtu asiyefikiri vema.
Eneo hilo linamakazi ya watu pamoja na frem za biashara zilizo chini ya halimashauri ya kinondoni.
Hivi tunavyoongea huduma ya kituo cha polisi haifikiki kwa gari, Ambulance haiwezi kuingia kukitokea dharura, Gari la zimamoto haliwezi kuingia kukitokea moto. Machinga wameblock barabara yote. Viongozi wapo na hamna hatua yoyote iliyochukuliwa.
Mbaya zaidi mkuu wa wilaya aliwatengea machinga wa mwenge eneo lao maeneo ya cocacola, Lakini kwa kuendelea kuwaruhusu baadhi kubaki maeneo ya polisi, Eneo lile limekosa msukumo wa biashara.
Hapa swali la kujiuliza, Ni vipi serekali kuu na halimashauri watapata kodi ikiwa wenye biashara rasmi biashara zao zimezuiwa na machinga mpaka mlangoni?
Inahitajika maamuzi ya haraka sana ili kunusuru kodi na mali za wafanyabiashara zilizopo bank, Hali ikiachiwa ikaendelea kama ilivyo, Athari itakuwa kubwa sana kwa biashara rasmi za mwenge na upande wa mapato serekalini.
Wenye mamlaka chukueni hatua za mapema,
Mimi mpita njia mzalendo nimeshauri!!
 
Back
Top Bottom