PreGE2025 Halima Nabalanganya wa ACT atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Mtwara mjini

PreGE2025 Halima Nabalanganya wa ACT atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Mtwara mjini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Mwanachama wa chama cha ACT-Wazalendo, Halima Yusuph Nabalanganya, Mei 22, 2025 amechukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Mtwara Mjini kupitia chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Halima amesema hatua hiyo inalenga kuomba ridhaa ya wanachama wa ACT-Wazalendo ili aweze kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2025.

Kwa sasa, chama cha ACT-Wazalendo tayari kimefungua rasmi zoezi la uchukuaji fomu kwa wanachama wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchi nzima mwaka 2025.

 
Back
Top Bottom