Halima Mdee amtaka Rais Magufuli ataje posho na marupurupu anayolipwa

Aliyeanzisha mada hii sio wananchi,wala wabunge;raisi mwenyewe anayependa sifa ndio alianzisha mjadala huu akithani watu mafala.
Raisi anapewa 36M kwa mwezi mkuu na anajengewa nyumba anakotaka na kulisha,kuvishwa na kulindwa maisha yake yote.
Hivi hujawahi msikia Zito na Tundu lisu toka enzi za jk wakitokwa na povu kuhusu mshahara wa rais?
 
Huyu Mama angekuwa anawaheshimu hao waliokuwa wanamsikiliza angenza kwa kutaja mishahara, posho na marupurupu ya viongozi wake...then ataje mshahara, marupurupu na mshahara wake yeye, kisha ndio aombe na Raisi ataje za kwake.
 
Msisahau pia kuwa mapato yote ya Rais hayatozwi kodi. Kwa hivyo ukiacha fiscal privileges nyingine, Rais is better off by 30% than the rest of us.
You are damm right fool!!!!!!!
He is better than us and you know it.
JPM is the president of The United Republic of Tanzania.
Any question?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Napata wasiwasi pale magufuli aliposema yeye binafsi,makamu wa rais na waziri mkuu watakuwa wanachangia sh 6 milioni kila mwezi kwenye mishahara yao kwa ajili ya elimu kwa mkoa wa dar es salaam.sasa kama analipwa 9.5 milioni pekee si rahisi kuchangia 6 milioni.labda kama ana marupurupu mengi zaidi.dah....ama kweli CCM ni ile ile.
hakusema watachangia kila mwezi bali alisema wachangie kwa ile 100mil.ambayo ilipelea haikutimia sasa cjui iyo ya kuchangia kila mwezi umeitoa wapi au aliisema rais wa rwanda
 
Hii nchi ndio maana inazidi kuwa masikini kwa kuwa nguvu zetu na akili zetu tumeviwekeza katika mambo yasiyo ya msingi.....haya malumbano na majibizano ya kisiasa yanayoendelea hayana tija yoyote kwa taifa badala yake inazidi kutuongezea umasikini....wanasiasa wanatakiwa wawahamasishe watu kufanya kazi kwa bidii na kujileletea maendeleo yao na sio kuwakusanya na kuwaambia mambo yasiyo na tija kwenye maisha yao....
 
Mdee ameonyesha udhaifu na upuuzi wa Hali ya juu sana , Kwa nini asingewasilisha bungeni mswada wa maslahi ya Rais ili yajadiliwe bungeni Kwa uwazi zaidi kuliko hizi kiki za majukwaani.
 
Halima, Halima, unashindwa kuja na hoja za maana unaleta hoja za posho ya Raisi!
Jamani kuna mambo ya msingi zaidi ya Posho ya mtu mmoja tena kiongoni mmoja wa nchi!
Halima usianze kupoteza credibility yako kwa hoja mfu! mfano akikupa taarifa itakusaidia nini sasa! tuna taka hoja zenye multiplier effect not minor issues
 
Tukiwa kama Taifa, naamini yapo mambo mengi ya msingi ambayo tunapaswa kuyajadili kwa Mustakabali chanya wa Taifa letu. Sidhani kama kufahamu Mshahara/ Posho anazopata Rais zinaweza kutusaidia sisi wananchi. Nawashangaa wanaoleta hoja ya kutaka kufahamu mapato ya Rais yatokanayo na kazi yake ya Urais. Hapo awali watoa hoja waliotangulia, hakuna hata mmoja aliyeeleza kuhusu kutaka kufahamu masuala ya posho/marupurupu anayolipwa. Isipokuwa walihitaji kufahamu mshahara wa Rais.

Katika kujibu hoja hiyo, Rais aliamua kutangaza mshahara wake kuwa analipwa 9.5M/=, na aliahidi kutoa uthibitisho wa nyaraka za mshahara wake. Kabla hilo halijatokea, walewale walioleta hoja ya kutaka kufahamu mshahara wa Rais, ndio wamekuwa wa kwanza kupinga kiwango hicho kwa kujaribu kuuaminisha Umma kwamba huenda analipwa zaidi ya alichokieleza.

Wengine wame-'quote' vipengele vya Katiba kuonesha kwamba Rais hana Mamlaka ya kujipunguzia mshahara, in otherwords wamemaanisha kuwa Rais alipaswa kuendelea kulipwa mshahara kama wa mtangulizi wake au zaidi ya ule. Wengine mbali na kutajiwa mshahara huo, pia wamehitaji kutajiwa na marupurupu anayolipwa Rais. Wapo walioenda mbali na kukosoa Rais kulipwa mshahara eti kwa vile anahudumiwa kila kitu..

Katika hili nawashangaa sana wafuasi wa vyama vya upinzani hususani Chadema na viongozi wao na Mdee akiwemo. Kwamba badala ya kuibua hoja zenye mashiko kwa Taifa, sasa wameanza kuja na Hoja zisizo na mashiko kama hizi za mshahara wa Rais.. Shame on them!!!

Binafsi sioni mashiko yyt ktk kuendeleza mjadala/ hoja ya mshahara au marupurupu anayolipwa Rais. Hayatusaidii na hayatakaa yatusaidie, Period.
 
Kumbe tumemaliza kuzungusha mikono sana tumeamia kwenye mifuko ya watu kujua mishahara yao. Kumbe aliyesema wajinga na wapumbavu hakukosea. Nchi ina matatizo lukuku sisi tunazungurusha mikono kwenye pochi , duh watu ni vibaka kweli kweli
 
Tukiwa kama Taifa, naamini yapo mambo mengi ya msingi ambayo tunapaswa kuyajadili kwa Mustakabali chanya wa Taifa letu. Sidhani kama kufahamu Mshahara/ Posho anazopata Rais zinaweza kutusaidia sisi wananchi. Nawashangaa wanaoleta hoja ya kutaka kufahamu mapato ya Rais yatokanayo na kazi yake ya Urais. Hapo awali watoa hoja waliotangulia, hakuna hata mmoja aliyeeleza kuhusu kutaka kufahamu masuala ya posho/marupurupu anayolipwa. Isipokuwa walihitaji kufahamu mshahara wa Rais.
Katika kujibu hoja hiyo, Rais aliamua kutangaza mshahara wake kuwa analipwa 9.5M/=, na aliahidi kutoa uthibitisho wa nyaraka za mshahara wake. Kabla hilo halijatokea, walewale walioleta hoja ya kutaka kufahamu mshahara wa Rais, ndio wamekuwa wa kwanza kupinga kiwango hicho kwa kujaribu kuuaminisha Umma kwamba huenda analipwa zaidi ya alichokieleza. Wengine wame-'quote' vipengele vya Katiba kuonesha kwamba Rais hana Mamlaka ya kujipunguzia mshahara, in otherwords wamemaanisha kuwa Rais alipaswa kuendelea kulipwa mshahara kama wa mtangulizi wake au zaidi ya ule. Wengine mbali na kutajiwa mshahara huo, pia wamehitaji kutajiwa na marupurupu anayolipwa Rais. Wapo walioenda mbali na kukosoa Rais kulipwa mshahara eti kwa vile anahudumiwa kila kitu..

Katika hili nawashangaa sana wafuasi wa vyama vya upinzani hususani Chadema na viongozi wao na Mdee akiwemo. Kwamba badala ya kuibua hoja zenye mashiko kwa Taifa, sasa wameanza kuja na Hoja zisizo na mashiko kama hizi za mshahara wa Rais.. Shame on them!!!

Binafsi sioni mashiko yyt ktk kuendeleza mjadala/ hoja ya mshahara au marupurupu anayolipwa Rais. Hayatusaidii na hayatakaa yatusaidie, Period.
Mkuu Halima mdee amefanya vile washabiki wanavyotaka hivyo yeye hana tatizo kwa sababu mambo yake yanamuendea vizuri tu,ila tatizo lipo kwa hao wenye kupenda habari kama hizo.
 
Napata wasiwasi pale magufuli aliposema yeye binafsi,makamu wa rais na waziri mkuu watakuwa wanachangia sh 6 milioni kila mwezi kwenye mishahara yao kwa ajili ya elimu kwa mkoa wa dar es salaam.sasa kama analipwa 9.5 milioni pekee si rahisi kuchangia 6 milioni.labda kama ana marupurupu mengi zaidi.dah....ama kweli CCM ni ile ile.

hay ndo matatizo ya kukosa information. it is very simple. kama kitu hukijui nyamaza ili utunze utu na heshima yako.
eti watakuwa wanachangia milion 6 kila mwezi!!
 
Rais Magufuli na wasaidizi kukatwa mishahara ili kuchangia elimu
magufuli1.jpeg


Rais John Magufuli amewaomba mawaziri, manaibu mawaziri, Makatibu wakuu na Manaibu wao wakubali kukatwa Sh. milioni moja kwenye mishahara yao ili zipatikane fedha za ujenzi wa madarasa jijini Dar es Salaam.

Alisema iwapo fedha kutoka kwenye mishahara yao zitakatwa, zitapatikana Sh. milioni 82 na zitabaki Sh. milioni 18 ili zitimie milioni 100 ambazo atazitoa yeye, Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Alisema kuwa anaamini kwasababu yeye ndiye aliyewateua kushika nyadhifa hizo bila kuombwa na mtu yeyote, basi watakubaliana na ombi lake hilo jema ambalo limelenga kuimarisha elimu katika Mkoa wa Dar es Salaam.

“Kwa kuwa niiliwateua mimi mwenyewe na wala sikuombwa na mtu yeyote basi, naamini watakubali kukatwa mishahara ili zipatikane hizo Sh. miloni 82,” alisema Rais Magufuli na kwamba “zitakazobaki haiwezi kuwa shida.”

Alisema kiasi kilichobaki hakiwezi kuwa tatizo kupatikana “kwasababu mimi nipo, Makamu yupo na Waziri Mkuu yupo, kila mmoja wetu atatafuta Sh. milioni sita ili tutimize milioni 100.”

Mbali na kuchangisha michango hiyo kutoka kwa viongozi hao, Rais Magufuli pia aliahidi kuupatia Mkoa huo Sh. Bilioni 2 kuongeza nguvu ya ujenzi wa madarasa, lakini alionya kuwa watakaojaribu kuzitumia vibaya basi “watakwenda na maji.”

“Ntawaongezea Sh. bilioni mbili kwa maana ya milioni elfu mbili, sasa Mkuu wa Mkoa ole wenu atakayejaribu kuzichepusha kwenda kufanya mambo ya ovyo ovyo, nasema kwa dhati kutoka moyoni maana msema kweli mpenzi wa Mungu… mkizichezea mtakiona,” alisema Rauis Magufuli na kusababisha ukumbi kulipuka kwa kicheko.

Aidha, Rais Magufuli alisema Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri ambao kwenye maeneo yao kutakuwa na wanafunzi wanaokaa chini watakuwa wameshindwa kazi na hawatakuwa na uhalali wa kuendelea na nafasi zao.

Alisema haiwezekani kiongozi akakaa kwenye gari zuri, ofisi yenye kiyoyozi na kulala kwenye nyumba nzuri wakati kuna watoto wa watanzania ambao wanakaa chini darasani halafu akaendelea kushika wadhifa wake.

“Hicho kitakuwa kipimo tosha kwamba huna sababu ya kuendelea kuwa Mkuu wa Mkoa, Wilaya ama Mkurugenzi wa Halmashauri,” alisema.

“Mkiona wanafunzi wanakaa chini mtakuwa mmeshindwa kazi na ni heri mkapisha ili watakaoweza kukabiliana na changamoto hizo wakalie hizo ofisi.

“Tanzania hii inautajiri wa kila aina, hakuna sababu kwa wanafunzi kukaa chini wala wagonjwa kulala wawili wawili kitandani, haiingii akilini kila ukipita sehemu ni shida tu wakati tuna rasilimali za kila aina, lazima viongozi tuwajibike kuondoa chanagamoto hizi kwasababu uwezo tunao na atakayeona hawezi apishwe wengine wanaoweza.”

Kufuatia kuanza kutimizwa kwa ahadi ya Rais Magufuli ya Elimu Bure kuanzia daraa la awali mpaka kidato cha nne mwaka huu, shule nyingi, hasa za mkoa wa Dar es Salaam zimekumbwa na ongezeko kubwa la wanafunzi.

Katika baadhi ya shule, idadi ya wanafunzi walioandikishwa kwa mara ya kwanza imezidi maradufu wanafunzi wote waliokupo wa darasa la kwanza mpaka la saba.

Shule ya Msingi Majimatitu ya Temeke jijini Dar es Salaam, kwa mfano, imeingia kwenye rekodi ya aina yake hapa nchini na pengine Afrika kutokana na kusajili wanafunzi 1,022 wa darasa la kwanza. Idadi ambayo inatosha kuanzisha shule nyingine.

Idadi hiyo imeifanya Majimatitu kuwa na jumla ya wanafunzi 6,000.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa shule hiyo ndiyo inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaosomea chini ya miti.

Shule hiyo ina madarasa 22 na ili iweze kumudu idadi hiyo ya wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la saba inahitaji nyongeza ya madarasa 109. Aidha inatakiwa kuwa na matundu 239 ya choo lakini kwa sasa yako matundu 36 tu.
matatizo ni nani mzee alcohol CCM wanatawala kwa miaka hamsini sasa au umesahau
 
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee amemuomba Rais John Magufuli kuweka wazi posho na marupurupu anayoyapata ili Watanzania wajue kiasi halisi anachokipata mbali na mshahara wake.

Mdee ambaye ni mbunge wa Kawe, alitoa ombi hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Sokoni, Jimbo la Mtama mkoani Lindi, uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo.

Kauli hiyo ya Mdee imekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kutaja mshahara wake kuwa ni Sh9.5 milioni kwa mwezi.

“Juzi Rais anasema eti mshahara wake Sh9.5 milioni, sasa atutajie posho za kila siku ili kila Mtanzania ajue kiasi ambacho anakipata,” alisema Mdee. Mdee aliongeza kuwa wabunge wanalipwa mshahara wa Sh3 milioni, lakini kuna posho mbalimbali kutokana na kuhudumia wananchi.

“Sisi wabunge mshahara wetu katika hati ya mshahara unasomeka Sh3 milioni, lakini posho na pesa ya mambo ya utendaji ya mbunge inafika Sh10 milioni, Rais atuambie na yeye posho zake ni kiasi gani,” alisema Mdee.


Chanzo: Mtembezi

Yaani huyu Bi mdada huwa ananikosha sana kwenye hoja zake anavyozipanga na vile ambavyo huwa anayakabili majipu makubwamakubwa kama kina Dr Mwakyembe, kina Sitta, yaani Mdee bhana, yuko vizuri sana hadi raha.

Haya, kazi kwako Mheshimiwa Mkuu wa nchi, hebu jibu sasa tuhuma na hoja hiyo ili wananchi kweli waujue uzalendo wako. Lakini pia ni kama ushauri, ikishatangazwa, basi watanzania tungeomba Mkaguzi mkuu na mdhibiti wa mapato ya serikali-CAG kwa kushirikiana na tume ya maadili na uwajibikaji kwa watumishi wa umma wayafanyie kazi matamko ya commander-in-chief His Excellency Mr JPM kwa kuunda tume huru ya kuchunguza kama kuna ukweli au uongo katika matamshi yake.

Nawasilisha,

 
Ukawa ni mabingwa wa kudandia matukio ngoja Magu awape tena lingine muimbe nalo, come 2020, tunawavuruga tena..
 
Back
Top Bottom