Halima Mdee ajisalimisha kwa Gwajima

Halima Mdee ajisalimisha kwa Gwajima

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,680
Reaction score
59,179
Katika hali ya kutokutegemea, Halima Mdee kaamua kujisalimisha kanisani la Ufufuo na uzima lililopo Kawe.

Kitendo hicho kimemuamsha Gwajima na kusema Kanisa la Ufufuo litakuwa naye katika uchaguzi wa 2015 na watamchagua tena.

Kanisa la Ufufuo na Uzima limemuahidi kumsaidia Halima Mdee kuhakikisha shule zote za Msingi Kawe zinakuwa na Umeme vilevile watahakikisha wanafunzi wote wa shule za Msingi Kawe wanakaa kwenye Madawati.

Gwajima kaitaka Serikali imruhusu kufanya Mikutano katika Mikoa ya kusini mwa Tanzania. Kasema gesi ni ya watanzania, Hata hivyo kasema migogoro ya Gesi haihusiani na imani za watu hivyo kataka waislam na Wakristo waruhusiwe Kufanya mikutano kusini Mwa Tanzania. Kaitaka serikali itambue gesi ni kwaajili ya Watanzania hivyo watanzania ndio inabidi wanufaike kwanza na hiyo gesi.

Band ya Jeshi la Magereza ndiyo imealikwa kumpigia Nyimbo Halima Mdee atakapokuwa anasimama kutoa salamu. Kasema anamheshimu Halima Mdee kwa kuwa ndiyo Mbunge Mwanamke wa kwanza Tanzania na Dar es Salaam kutoka Upinzani kushinda Uchaguzi bila kutoa Rushwa.

Kasema Halima Mdee anaiwakilisha na kuitangaza vizuri Kawe hivyo wanakawe inabidi watambue Umuhimu wake.

Gwajima anasema sisi ni Watanzania hatupaswi kuwekewa mipaka sehemu ya kufanya Injili ndo maana nimenunua Helkopta kuzunguka Tanzania nzima hata huko Mtwara nitaenda japo Serikali inakataza. Watu wa Mtwara nao inabidi wamjue Mungu ili kupunguza Uharifu. Vilevile Gwajima na washirika wake wamesema wanaunga Mkono Serikali Tatu. Kasema wale wanaodai mbili hata hizo mbili hazipo. Zingekuwa mbili kama Tanganyika ingekuwepo.

Gwajima kasema Zanzibar ipo lakini ipo na Serikali nyingine ambayo ni Tata. Hivyo watu wanapaswa watambue uwepo wa Tanganyika.

Kasema Tanganyika na Zanzibar ni mbili tayari hivyo tunatakiwa tupate ya Tatu ambayo inaziunganisha hizi mbili.

VIDEO:

 
Last edited by a moderator:
Nasikia serikali ya MaCCM wanataka kumtoa Gwajima pale viwanja vya Kawe kutokana na msimamo wake wa kuunga mkono harakati nyingi za upinzani na hasa uswahiba wake na Dr Slaa ......MaCCM acheni visasi nyakati hizi zilizojaa uwazi bana ......
 
gwajima hana lolote la uadilifu. kanisa lake kama kakobe ni kampuni ya kujipatia kipato kwa udanganyifu. baada ya kuwazuga wafuasi wao na kupata utajiri mkubwa uroho umewazidia. wanaona kwenye siasa kuna pesa zaidi.
 
Yaliyomkuta emmanuel mbasha na kuzua mgogoro kwenye familia yake sasa yataikuta chadema pale itakapojulikana gwajima anatwanga kinu cha mh mbunge
 
gwajima hana lolote la uadilifu kanisa lake kama kakobe ni kampuni ya kujipatia kipato kwa udanganyifu. baada ya kuwazuga wafuasi wao na kupata utajiri mkubwa uroho umewazidia. wanaona kwenye siasa kuna pesa zaidi.
Halima kesha kuwa msukule!
Kwa Gwajima wanajipeleka wengi!!
 
nasikia serikali ya maccm wanataka kumtoa gwajima pale viwanja vya kawe kutokana na msimamo wake wa kuunga mkono harakati nyingi za upinzani na hasa uswahiba wake na dr slaa ......maccm acheni visasi nyakati hizi zilizojaa uwazi bana ......

lazima slaa na gwajima wawe marafiki ukichukulia mapungufu yao kwenye suala la km
 
Fulo kampaisha Gwajima, sasa hivi atafikia level za Diamond kwa 'usukari wa warembo'
 
Back
Top Bottom