Hali imezidi kuwa mbaya katika kampuni ya Business Times Ltd inayochapisha magazeti ya Majira, Spoti Starehe na Business Times baada ya menejimenti ya kampuni hiyo kuwaita polisi kwa ajili ya kuwadhibiti wafanyakazi walioitisha mgomo.
Wafanyakazi hao waliitisha mgomo kuanzia jana saa 7 mchana wakidai kupatiwa malimbikizo yao ya mishahara ambayo hawajalipwa tangu Mei mwaka huu. Taarifa za ndani kutoka katika kampuni hiyo zinasema baadhi ya waliogoma tayari wamesimamishwa kazi. Waliosimamishwa ni pamoja na Mhariri wa Habari wa gazeti la Majira, Regnald Miruko na Mpiga Picha Mkuu, Emmanuel Kwitema.
Polisi walioingia na silaha katika ofisi za kampuni hiyo wameletwa kudhibiti hali iwapo vurugu itatokea. Inaelekea kuwa hali si shwari kutokana na ukata mkubwa unaodaiwa kuikumba kampuni hiyo inayoendeshwa kifamilia zaidi kuliko kitaaluma. Viongozi wa kampuni hiyo ni Rashidi Mbuguni (Baba) ambaye ni Mkurugenzi, Aga Mbuguni (mtoto) ambaye ni Meneja Mkuu na Imma Mbuguni (mtoto) ambaye ni Mhariri Mtendaji. Hata hivyo, inasemekana kuwa pamoja na kwamba Mhariri Mtendaji siyo mwandishi kitaaluma na kwamba hajawahi kuandika habari yoyote, kampuni hiyo ilimkabidhi dhamana ya kuwa juu ya wahariri wote.
Wasiwasi uliotanda ni iwapo wafanyakazi watapata haki zao wanazodai baada ya kufanya kazi kwa miezi kadhaa bila malipo. Wasiwasi mwingine ni madai ya baadhi ya wafanyakazi yanayosema kwamba kuna malipo ya NSSF ambayo hayajalipwa na kampuni hiyo kwa muda mrefu.
Kampuni iliyosifika sana katika miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 sasa imefikia hali mbaya kiasi cha kushindwa kuwalipa wafanyakazi wake. Inasemekana pia kwamba hata wanaoacha au kuachishwa kazi wengi wao hawajalipwa tangu walipoondoka katika kampuni hiyo. Huenda hali ikawa mbaya zaidi katika siku zijazo kutokana na tetesi kwamba inewezekana kampuni hiyo ikatangazwa kuwa imefilisika.
Katika kuhakikisha kuwa mgomo huo unadhoofika, menejimenti ilitumia mbinu ya kuwagawa wafanyakazi hao na 'kuwashikisha' wengine ambao walikuwa tayari kuendelea na kazi.