Hali Ya Utulivu Imerejea Iringa...

Hali Ya Utulivu Imerejea Iringa...

Kijana wangu Maggid,kumbuka ulivyokuwa nguzo enzi za Rai,lakini leo umeamua kuacha kujishughulisha,badala yake umechagua maisha ya kulelewa na mwanamke wa kizungu asiye na vibali vya kuishi nchini,kwa hiyo huna budi kuishi kwa kujipendekeza tu,maana mlezi wako asije akatimuliwa! Kusema kweli makala yako kwenye Raia Mwema kwamba kinana si jangili bila kutoa facts,ilitushangaza wengi,ila kwa vile umechagua maisha si vibaya endelea tu.
 
maggid,you are always writing in defence of a ruling party while accusing opposition parties' leaders.My son,stop being biased. Write on the truth and you will be free forever!

snitch tu huyo!
 
Last edited by a moderator:
Hivi huyu Maggid ni MUISLAMU AU MKATOLIKI?

Mana sisi wak......................tupo zetu CDM tunatafuta ukombozi wa nchi na wale wais.................wapo zao CCM.
Hivyo tukimjua yupo wapi basi shida hamna tena mana ni suala lilopo wazi.
 
Ndugu zangu,


Jioni hii baada ya mazoezi ya mpira wa watoto niliongozana na makamanda wangu hadi mitaa ya kati ya Iringa. Nilifika maeneo ya Stendi Kuu, Mashine Tatu na hata Soko Kuu. Hali ya utulivu imerejea. Sikuona hata polisi mmoja barabarani.


Baadhi ya shughuli za biashara zimerejea kama kawaida. Lakini, la msingi, katika miaka yangu kumi ya kuishi hapa Iringa hili ni tukio la kwanza la aina yake.


Bado naamini, kuwa hili la Wamachinga na Manispaa ni jambo dogo ambalo, kama wahusika watatanguliza hekima na busara, linaweza kumalizwa mezani na kunusuru amani na utulivu wa Mji wa Iringa.


Maana, katika nchi za wenzetu kwa yaliyotokea leo wangefanya pia mahesabu ya hasara ya kiuchumi iliyotokana na kusimama kwa shughuli za kiuchumi.


Maana, kama mtu atapiga hesabu za haraka tu kuangalia machache yafuatayo: Gharama za mafuta na posho kwa idadi ya magari ya polisi yaliyotumika, idadi ya polisi walioshiriki zoezi la leo. Idadi ya mabomu yaliyotumika leo na gharama yake.


Iangaliwepia hasara ya kimapato kwa idadi ya maduka yaliyofungwa kwa siku ya leo. Daladala zilizoshindwa kufanya kazi. Achilia mbali mali zilizoharibiwa.


Maana, kadhia kama hii ya leo imepelekea kupungua kwa kiasi kikubwa cha mzunguko wa fedha na hivyo kuwaathiri wengi kiuchumi.


Ni dhahiri, kuwa ni muhimu kwa Wamachinga wakatafutiwa namna ya kufanya kazi yao ya kujipatia riziki, lakini, itangulizwe pia hekima na busara katika kulitafuta jawabu ili kuepusha madhara ya kiuchumi na kijamii.


Ni matumaini yetu, kwa mji wetu wa Iringa na Mkoa wetu kwa ujumla, tukio la leo liwe pia fundisho la kubaini njia bora za kutatua migogoro yetu , ya kisiasa na kijamii. Na hakuna njia iliyo bora kabisa, kama njia ya mazungumzo.


Na kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine ya kutufikisha hapa, basi, watafakari kwa makini, ili kilichotokea leo kisitokee tena, kama inawezekana.


Maggid,

Iringa.
0754 678 252
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio

Hawapo kwa ajili ya wananchi bali matumbo yao, kwa hiyo watatengenezaje maeneo huru kibiashara!
 
Mggid wewe sio mwandishi wa habari, unaandika kile CCM wanapenda kukisikia. huijui Iringa inawezekana umezaliwa Iringa ila huijui Iringa. Watu wa Iringa hawapendi uonevu, muulize Dr Kleruu, Joseph Mungai nk.

Kama wewe unasema eti hayo uliyoyaona juzi ndio maandano au kasheshe ya polisi kwa wanchi nenda kaa chini na Mungai halafu muulize swaga la miaka ya tisini nini kilitokea hapo mjini. Iringa tachie sisi tunaokula kwa dua.
 
Back
Top Bottom