Hali Ya Utulivu Imerejea Iringa...

Hali Ya Utulivu Imerejea Iringa...

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,251
Ndugu zangu,


Jioni hii baada ya mazoezi ya mpira wa watoto niliongozana na makamanda wangu hadi mitaa ya kati ya Iringa. Nilifika maeneo ya Stendi Kuu, Mashine Tatu na hata Soko Kuu. Hali ya utulivu imerejea. Sikuona hata polisi mmoja barabarani.


Baadhi ya shughuli za biashara zimerejea kama kawaida. Lakini, la msingi, katika miaka yangu kumi ya kuishi hapa Iringa hili ni tukio la kwanza la aina yake.


Bado naamini, kuwa hili la Wamachinga na Manispaa ni jambo dogo ambalo, kama wahusika watatanguliza hekima na busara, linaweza kumalizwa mezani na kunusuru amani na utulivu wa Mji wa Iringa.


Maana, katika nchi za wenzetu kwa yaliyotokea leo wangefanya pia mahesabu ya hasara ya kiuchumi iliyotokana na kusimama kwa shughuli za kiuchumi.


Maana, kama mtu atapiga hesabu za haraka tu kuangalia machache yafuatayo: Gharama za mafuta na posho kwa idadi ya magari ya polisi yaliyotumika, idadi ya polisi walioshiriki zoezi la leo. Idadi ya mabomu yaliyotumika leo na gharama yake.


Iangaliwepia hasara ya kimapato kwa idadi ya maduka yaliyofungwa kwa siku ya leo. Daladala zilizoshindwa kufanya kazi. Achilia mbali mali zilizoharibiwa.


Maana, kadhia kama hii ya leo imepelekea kupungua kwa kiasi kikubwa cha mzunguko wa fedha na hivyo kuwaathiri wengi kiuchumi.


Ni dhahiri, kuwa ni muhimu kwa Wamachinga wakatafutiwa namna ya kufanya kazi yao ya kujipatia riziki, lakini, itangulizwe pia hekima na busara katika kulitafuta jawabu ili kuepusha madhara ya kiuchumi na kijamii.


Ni matumaini yetu, kwa mji wetu wa Iringa na Mkoa wetu kwa ujumla, tukio la leo liwe pia fundisho la kubaini njia bora za kutatua migogoro yetu , ya kisiasa na kijamii. Na hakuna njia iliyo bora kabisa, kama njia ya mazungumzo.


Na kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine ya kutufikisha hapa, basi, watafakari kwa makini, ili kilichotokea leo kisitokee tena, kama inawezekana.


Maggid,

Iringa.
0754 678 252
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio
 
mkuu kwa nini usingeweka update kwenye theard yako ya awali.?
 
Sijui kwa kwa nini hujapewa ukuu wa wilaya mpaka leo manake unajikomba kwa chama tawala mpaka utafikiri mtoto wa miaka 18 kumbe ni baba mzima, wamachinga ni watu,watanzania kama wewe wanahitaji fursa kama zako,na wanatakiwa kusikilizwa,uchumi unaoutetea unachangiwapia na wamachinga acha kulaaumu na kutafuta sababu bali uwe kati ya wale wanaoona ukweli na kutatua tatizo wewe unashiba na wenzio wanahitaji kushiba halmashauri zinakusnaya fedha nyingi sana hivi ni kwa nini hawajengi maeneo kwa ajili ya amchinga
 
Kwanini wakati yanatukia hukututarifu unakurupuka saa hizi kaa umefumaniwa.Punguza unafiki we kaka yake Ludovick.
 
Maggid acha unafiki,leo ndio umejua machinga wanamgogoro na manispaa,juzi wakati mbunge wako anatoa hoja hukusikia,kama meza moja umeona ijadiliwe baada ya hili tukio au ilitakiwa kabla ya tukio,matatizo ya serekali hii ni kutibu matokeo badala ya chanzo...
 
maggid,you are always writing in defence of a ruling party while accusing opposition parties' leaders.My son,stop being biased. Write on the truth and you will be free forever!

Huyu Majid ni miongoni mwa mandumilakuwili anayekuja na mambo ya ajabu ajabu kila siku. ambacho hajagundua mpaka leo kuwa mwandishi au kuwa na chombo cha tv kinachoweza kuzuia mabadiliko. Wasomi, wajinga , mataahira, vichaa wote wameshtuka mabadiliko tena ya haraka lazima yatokee
 
Last edited by a moderator:
Waliofny fujo viroba walivyokunyws vitakapoisha wataisoma namba
 
Mtoa mada na Wengi tunaochangia humu hatuelezi madai ya Machinga ni nini na kwamba sisi tunadhaninini kifanyke kuleta suluhu.

NIjuavyo mimi Barabara tajwa ni ya magari yanayoenda kituo kikuu cha mabasi na Jee? Machinga wameivamia na kupanga bidhaa?

Kama ni hivyo Mbunge Msigwa katika sera za mipango miji za Chadema mkishika nchi ndo zinataka biashara zifanywe kwa mtindo huu?
 
kwa maoni yangu ni bora tutumie gharama yoyote kulinda aman. hongera jeshi la polisi.
 
kwa maoni yangu ni bora tutumie gharama yoyote kulinda aman. hongera jeshi la polisi.

Ukumbuke pia kwamba, "AMANI NI TUNDA LA HAKI". Vinginevyo mtatumia gharama kubwa na amani isipatikane. Hakuna risasi inayo shinda ukweli na madai ya haki.

Kiongozi! This is the BEGINNING OF THE END.
 
shida zote hizi ni pale akili ndogo tu inaruhusiwa kuongoza akili kubwa. nasikitika nchi ya hii na viongozi wake wanashindwa kuwapanga wananchi hii inakimbilia kutumia mabomu nasikitika sana haya yatakuwa mawazo ya mwigulu na yule wa mtera na pia chief whip wa sisiemu
 
Tatizo lako Maggid ni kwamba unapoandika unakuwa umeegemea upande mmoja wa huu mgogoro. Kwenye thread yako ya asubuhi uliandika na kusema wazi kwamba Mbunge Msigwa anahusika kwenye huu mgogoro. Lakini kiuhalisia wa mambo ni kwamba tatizo la wamachinga limekuwepo kwa muda mrefu.
Sasa kwa kuwa tatizo limelelewa kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi na leo limelipuka, solution yako ya kusema msigwa ndiye tatizo inakosa mantiki.
Nakushauri unapoandika juu ya mambo Kama haya ujaribu kuwa objective kidogo. Angalia chanzo cha tatizo badala ya kuja na solution ambayo haitibu chanzo cha tatizo. Hiyo siyo njia nzuri ya kumaliza tatizo.
 
Tatizo la viongozi wetu hutegemea sana nguvu na vyeo walivyonavyo wakizani kuwa ni suluu,swala la wamachinga ni nchi nzima,kwani idadi ya wamachinga huongezeka kwa kasi kubwa,hii ni kutokana ukusefu wa ajira.Pia viongozi wetu ni km hawaelewi mmachinga ni mtu wa namna gani,mara nyingi huwatengea maeneo ambayo haya wezekani wao kuuza :-Ikumbukwe kwamba mchinga ni mfanyabiashara anayemfuata mteja na sio mteja kumfuata mtu huyo.Ushauri wangu serikali isiwatengee maeneo ambayo sio makutano ya mtu!
 
Msimlaumu mtoa mada acha watandikwe ndio washike adabu nchi lazima iongozwe na sheria

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
maggid,you are always writing in defence of a ruling party while accusing opposition parties' leaders.My son,stop being biased. Write on the truth and you will be free forever!

The question Dear VN, will one only be free by supporting CDM? To be free is to be honest and being courageous enough to admit when you r wrong or the one you love or support is wrong. Maggid has posted a very conciliatory posting that is full of truth. Politics is not destroying or insiting. For the first time i have been disappointed by clergy msigwa. I hope he will change, being a man of the cloth he should preach harmony, tolerance and he should fight for the oppressed in a godly manner, na sio kihuni.
 
kwa kila kumi na 2 iskariot lazima awepo pole Maggid mjinga:shock::shock:
 
Ukumbuke pia kwamba, "AMANI NI TUNDA LA HAKI". Vinginevyo mtatumia gharama kubwa na amani isipatikane. Hakuna risasi inayo shinda ukweli na madai ya haki.

Kiongozi! This is the BEGINNING OF THE END.

Endeleeni kuleta chokochoko muone. soon mwisho wa kuwavumilia kwaja.
 
The question Dear VN, will one only be free by supporting CDM? To be free is to be honest and being courageous enough to admit when you r wrong or the one you love or support is wrong. Maggid has posted a very conciliatory posting that is full of truth. Politics is not destroying or insiting. For the first time i have been disappointed by clergy msigwa. I hope he will change, being a man of the cloth he should preach harmony, tolerance and he should fight for the oppressed in a godly manner, na sio kihuni.

Mkirindi seems you have got Maggid half way. The problem as to the space where Machingas can do their business has been for a long a time. What's is needed is a viable and permanent solution as they are also citizens of the country and stakeholders in what we are boasting of 'AMANI NA UTULIVU". Relocating them at gun point is not a solution as that creates hatred that will hardly die. Msigwa is a human being and cannot run away from the Machingas and on top of that he's the elected leader. Why should he remain passive while his voters are being tortured for no cause. They are forced to drink the bitter chalice due to irresponsibilities of municipal functionaries and police who are used without applying psychology. Seems you are happy with they the manner police are ordered to suppress poor people and opposition. However, note we all living in the catastrophic planet and one day what police are doing to other people will turn to you guys as long we continue surviving
 
Maggid, wewe kama mmoja wa wadau wakubwa hapo Iringa ni lini ulishawahi kuchukua all channels and tools at disposal to send a message kwa viongozi wa serikali, CCM na wahusika wa manispaa hapo ili Wamachinga wapate sehemu mwafaka kuweza lufanya shughuli zao? Kama hujawahi kufanya hivyo basi na wewe ni sehemu ya tatizo. Mheshimiwa Msigwa amejitahidi sana na akaongea mpaka bungeni kwa kuiambia serikali kuwa huwezi kuleta suluhu za Machingas kwa mtutu wa bunduki. Tabia ya kushughulikia matatizo kwa kutumia silaha haijawahi kuleta suluhu duniani kote toka Adam. Sasa mmemwacha Mh.Msigwa atetehe peke yake mpaka kiasi cha kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi. Mimi nilitegemea wewe ambaye walau you have pedestal upon which you can stand and write and speak ungeanza tangu zamani kufanya hivyo na ungewaambia poilisi na wale waliowatuma kumkamata mbunge kuwa walichofanya sio kizuri na hakiachi alama nzuri kuliko kuja na maelezo marefu lakini yako prejudiced and biased
 
Back
Top Bottom