Hali ya usikivu mdogo inavyonikosesha ajira/fursa

Pole kaka yangu....
Me nataka kujua ni tatizo la kuzaliwa au limekuja ukubwani??
 
Gharama sana ndiyo kiasi gani?

Inawezekana zikawa gharama Tanzania lakini wengine wakawa na njia rahisi ya kuzipata nje.

Fuatilia utupe mrejesho. Zinahitajika za aina gani, za specification gani.
Ngoja nifatilie mkuu tutajuzana
 
Pole sana!
Tinnitus haina tiba kamili ila ukienda Muhimbili kumuona ENT Specialist anweza kukufanyia tathmini kamili na kukushauri kutumia electronic device to supress noice..
Kilichokutokea ni sehemu ya sikio inayochuja sauti na kupeleka kwenye ubongo kwa ajili ya utambuzi.
Vifaa vya kusaidia kuchuja sauti vipo.
All the best na Mungu akupe wepesi.
 
Gharama sana ndiyo kiasi gani?

Inawezekana zikawa gharama Tanzania lakini wengine wakawa na njia rahisi ya kuzipata nje.

Fuatilia utupe mrejesho. Zinahitajika za aina gani, za specification gani.
Navojua kwa hearing aids nzuri za kumfaa pamoja na kumpunguzia kelele za tinnitus gharama zake ni si chini ya dola 5000/=.
 
Ngoja tufatilie mkuu
 
Samahan ndugu naweza pata nafasi ya kuja DM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma elimu maalum kaka ujue lugha ya alama ndugu
 
Mimi mwenyewe nina hilo tatizo japo niko kada ya elimu.
 
Pole sana mkuu, mimi binafsi nina hilo tatizo tangu 2008 niko form one. Tulishazunguka sana hospital zote Tanzania mpaka ujerumani ila holla.

Hearing devices hazikusaidia, sijfuatilia tena kama zipo more advanced siku hizi.

But trust me my friend, with time tatizo linapungua. Now mtu hawezi jua kama nina tatizo labda akikaa na mimi kwa muda mrefu sana.

Zamani ilikua hatuelewani na mtu kabisa, but now miaka inavozidi kwenda hali inazidi kuwa better.

Nishapitia hali zote hapo umetaja, kuchekwa, dharau etc.

Naweza kubaliana na wewe kuhusu kubaniwa ajira sababu ya tatizo lako, lakini pia naweza kutokubaliana na wewe (based on my own experiences). Nadhani kikubwa zaidi Onyesha uwezo wako, mimi napata deals kibao kwenye mashirika mbalimbali na ni wao wananitafuta mimi (nina masters katika kada ya afya).

Kuwa na tatizo kusikufanye mnyonge au kuona haufai (ingawa kibinadamu **** wakati nilikata tamaa) but amini nakwambia ukijikubali WEWE NI BORA KABISA. Mimi pamoja na kuwa na tatizo langu nimekua mwanafunzi bora kitaaluma kuanzia sekondari, bachelor degree mpaka masters pale MUHAS kote nimekua nikatunukiwa best final year student. Je, tatizo la kusikia ni sababu ya kukata tamaa? HAPANA. Naamini kabisa tatizo hili haliwezi kuwa kikwazo kwako maana kwangu haijawa kikwazo (ukiachana na changamoto za kawaida za kijamii)

All in all pole sana, unayopitia i can feel you kutoka moyoni kabisa. Nimejisikia simanzi sana maana umenikumbusha changamoto nilizopitia.

NB: kama utaweza kujiajiri itakua poa zaidi, hapo you will set your own rules

cheers
 
But trust me my friend, with time tatizo linapungua. Now mtu hawezi jua kama nina tatizo labda akikaa na mimi kwa muda mrefu sana.

Zamani ilikua hatuelewani na mtu kabisa, but now miaka inavozidi kwenda hali inazidi kuwa better.
Ni nini ulifanya mpaka tatizo liwe linaenda linapungua ? Au kuna lifestyle ulibadili kama diet nk
 
Ni nini ulifanya mpaka tatizo liwe linaenda linapungua ? Au kuna lifestyle ulibadili kama diet nk

Sikufanya chochote mkuu.

Ilifika mahali nikakubaliana na tatizo. Maana ilifika mahala tunatumia costs kubwa sana bila ahueni.

Nadhani pia ni genetics, mdogo wangu wa kike nae alipofika form two nae tatizo likaanza.

Nadhani kadri miaka inasogea tatizo linapungua. Maana mimi ni miaka almost 15 niko na tatizo
 
hazina msaada kabisa naona ni kama biashara za madaktari wa ENT na hospitali za masikio.
Mkuu, upo sahihi kabisa. Mimi baada ya kukutana na shida hiyo, ndugu walimshauri mzee tuje dar, hospital inaitwa EKENYWA, ENT akanisafisha masikio, then wakaniambia nirudi alhamis nionane na audiologist kwa ajili ya kupima usikivu, siku hiyo nikarudi wakanipima, then nikarudi tena kwa ENT, akasema hapo tujaribu hearing aids. Nikapewa namba ya muhusika.

Kuja kumtafuta muhusika, katuambia tumfuate Mlongazila Hospital, kufika kule ni jamaa wa audiology alinipima Ekenywa, akasoma tena ripoti yake, akaanza kuniandikia bei za hearing aid zitakazofaa, akasema kwa level yangu itakayofaa ni ya 1.4M za kitanzania, sawa tukamwomba jina la pharmacy au duka la vifaa tiba, jamaa aligoma kabisa kutupa jina na location. Akisema pesa tumpe yeye halafu atatuletea. Najua tulipigwa parefu tu, na hearing aid ndo hivyo tena.
 
Pole sana mkuu
Huko kote mimi nimepita pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…