SENGANITU
Member
- Sep 19, 2012
- 50
- 15
Hali ya usalama wilaya ya mvomero imekuwa ni mbaya kutokana na vurugu iliyoanzishwa na wakulima wakidai haki yao ya ardhi waliyonyang'anywa na wafugaji. Wakulima wanadai waliiambia serikali juu ya tatizo hili lakini hawakulitilia maanani.
Kuanzia tarehe 13/10/2013 hadi 14/10/2013 wakulima walifunga njia kuu kuelekea morogoro kwenye maeneo ya mkindo wilayani humo. Jana tarehe 14/10/2013 mida ya saa 10 jioni walikubaliana na ujumbe wa mkuu wa mkoa kusitisha kizuizi hicho kwa muda wa siku tatu, yaani tarehe 15-17/10/2013, na kwamba kama hakuna suluhisho watarudi tena barabarani.
Hali ya kushangaza imejitokeza asubuhi ya leo baada ya polisi kupita kituo cha polisi cha Turiani wakiwa na maiti ya mtu wakimpeleka kufanyiwa uchunguzi katika hospitali ya bwagala kuchunguza chanzo cha kifo chake. Huyu marehemu inadaiwa aliuawa wakati wa vurugu hizo za maandamano ya wakulima.
Hali imekaa vibaya baada ya wakulima kusikia hilo tukio la kifo cha mwenzao, kuna hali ya sintofahamu kitakachofuata baadae kwa tukio hilo la kifo.