Hali ya usalama wa raia Burundi ipo hatarini.

Hali ya usalama wa raia Burundi ipo hatarini.

MzamiajiX

Member
Joined
Nov 14, 2018
Posts
36
Reaction score
34
Baada ya ya rais Pierre Nkurunzinza kuvunja katiba na kugombea urais kwa mhula wa tatu hali ya usalama nchini Buriudi imekua sio nzuri.
Uchaguzi uliomuweka madarakani Nkurunzinza ulilaumiwa vikali na jumuiya za kimataifa kuwa sio wa huru na wa haki kwani ulivunja katiba na kukiuka sheria za nchi hiyo.
Pia upinzani nchini humo ulilalamikia serikali ya Nkurunzinza vikali na kutoiunga mkono serikali yake.
Hali imekua si shwari nchini humo mpaka hivi sasa kumekua na hatari kubwa sana ikizingatiwa jamii ya kimataifa imefukuzwa nchini humo hasa balozi kadhaa.

Mauaji ya wapinzani wake na raia wanaoipinga serikali hiyo yamepamba moto.
Baadhi ya nyumba zimekua zikitumika kwa siri kuua viongozi walioasi na upinzani kwa ujumla kuwachinja kwa visu na Nkurunzinza mwenyewe na serikali yake.

Hali ni mbaya sana katika nchi hiyo pengine msaada unahitajika kuiweka nchi hiyo katika hali ya usalama.

NB: Kwa siasa za dunia hii hamna jipya mambo ni yale yale chamsingi raia wajifunze namna ya kuepukana na machafuko ya kisiasa pindi machafuko yanapotokea.
 
Back
Top Bottom