Hali ya umeme nchini yazidi kuimarika

Hali ya umeme nchini yazidi kuimarika

pinpilojr

Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
59
Reaction score
10
Hali ya Umeme nchini yazidi kuimarika

Shirika la Umeme TANESCO limesema kuwa Uhakika wa umeme unaonekana sasa kwa mikoa iliyoungwa kwenye grid ya taifa unatokana na kuendelea kuwashwa kwa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gesi.

Mitambo hiyo ni ya Kinyerezi 150 MW, Ubungo 2 (105MW) na Symbion 112 MW. Mvua zilizoanza kunyesha bado hazinyeshi kwenye mikoa yenye mita inayoweza kujaza Bwawa la Mtera, Kidatu na Kihansi ambayo ndio vyanzo vikubwa vya kufua umeme wa maji.

Hayo yalisemwa leo na Meneja Uhusiano TANESCO Adrian Severin wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Ubungo jijini Dar es salaam
 
Hali ya Umeme nchini yazidi kuimarika

Shirika la Umeme TANESCO limesema kuwa Uhakika wa umeme unaonekana sasa kwa mikoa iliyoungwa kwenye grid ya taifa unatokana na kuendelea kuwashwa kwa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gesi.

Mitambo hiyo ni ya Kinyerezi 150 MW, Ubungo 2 (105MW) na Symbion 112 MW. Mvua zilizoanza kunyesha bado hazinyeshi kwenye mikoa yenye mito inayoweza kujaza Bwawa la Mtera, Kidatu na Kihansi ambayo ndio vyanzo vikubwa vya kufua umeme wa maji.

Hayo yalisemwa leo na Meneja Uhusiano TANESCO Adrian Severin wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Ubungo jijini Dar es salaam.

"Tanesco imejipanga kuwahudumia watanzania. Hali ya Umeme nchini imeimarika sana kwa sasa kutokana na ujio wa gesi, na bado kuna mitambo inaendelea kuwashwa. Mtuamini." Alisema Severin.
 
Maana yake ni kwamba Magufuli asihangaike na Tanesco kwa sasa, aendelee kufanya ziara za ghafla sehemu zingine lakini sio Tanesco, si ndio eeh??!!
 
Nimeshangaa sana maeneo ya Buguruni umeme upo 24 hrs.naomba waendelee hivyo hivyo.
 
Kweli kabisa yaaan kwa sasa umeme kukatika kwetu imekuwa historia na i hope now Tanesco they have comeup
 
Back
Top Bottom