Hali ya nchi ni tete! Tumjadili rais tumtakaye 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali ya nchi ni tete! Tumjadili rais tumtakaye 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kabindi, Apr 29, 2011.

 1. k

  kabindi JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 334
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  U-TETE ninaozungumzia hapa sina maana ya kuwa Raisi wa sasa ataachia ngazi kabla ya muda wake, au atapinduliwa, pia kuumwa na kufariki ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu!

  Ninachotaka kuzungumza hapa bora hayo yangetokea yangekuwa ni majibu ya moja kwa moja na pengine yangekuwa ndiyo matokeo au Mungu kutimiza wajibu wake!

  Hapa kuna Maswali yanayohitaji majibu. la sivyo mambo hayatakuwa salama.

  Umasikini wa watanzania: Umasikini unaongezeka kwa kasi ya kutisha na ni wazi kwamba Serikali hakuna lolote inaloweza kufanya kwa sasa maana wameishachanganyikiwa na wameshindwa kuwa wabunifu wa utatuzi wa matatizo yanayowakabili wananchi.

  Wizi na kesi zisizokwisha na zenye matokeo ya kutia wasiwasi: Watanzania wanataka uwajibikaji na majibu ya haraka na yenye ufanisi. Inatia wasiwasi kwamba kesi nyingi za EPA zitakuwa kiini macho na hivyo watanzania watakosa majibu kabla ya 2015, KAGODA, MEREMETA,RADA na wizi mwingine havitakuwa na majibu.Kutopatikana kwa majibu halisia ya hoja hizi kutaendelea kuibomoa Serikali ya KIKWETE.

  Raisi ni FISADI!: hii ni kauli na tuhuma nzito kwenda kwa kiongozi aliyechaguliwa na wananchi na kula kiapo kwa vitabu vya dini na katiba ya Nchi, kuilinda, kuitetea na kuisimamia. KIKWETE ametajwa kila mara na viongozi wa upinzani kuwemo katika orodha ya mafisadi! na Kwamba kuingia kwake madarakani mwaka 2005 kunahusishwa na wizi wa pesa za EPA. Kama angekuwa mtu safi kwa nini asiwachukulie hatua za kisheria!? inaonyesha kuna uozo nyuma yake!. Hili ni tatizo kubwa kwa CCM kwa maana kwamba ni nyundo juu ya Kichwa cha Chama. Wananchi wanataka majibu na hawatayapata! Serikali na chama vitaendelea kubomoka.

  Mifarakano ndani ya CCM:, Mifarakano nadani ya chama haikuanza leo, ni ya muda mrefu na imekomaa.Wakati huko nyuma ikitokea na kuambiwa kwamba kuna nyufa au mipasuko ndani ya Chama wao walijitutumua na kusema kwamba CCM ni imara na ni kitu kimoja!. Sasa lah! tunashuhudia kwa macho na masikio. Nani ajivue gamba? Lowasa, Rostam na Chenge peke yao?!! it is too late!. ni uongozi mzima wa chama yaani kuanzia Mwenyekiti wake. Huu ni mpasuko wa kishindo!.

  Katiba Mpya: Wananchi sasa wanataka katiba mpya na hili lieleweke si kwa matakwa ya kIKWETE bali ni kwa nguvu ya Umma. Analizimika kufanya hivyo ama sivyo moto wake ni mkali! kero za muda mrefu katika katiba ya sasa lazima zijibiwe katika katiba mpya! kama vile tume ya uchaguzi, nguvu za Raisi na suala zima la Muungano lazima majibu yapatikane kabla ya 2015.! Watanzania leo sio tena mbumbumbu ukiwaambia Tanganyika iliungana na Zanzibar tukapata Tanzania na Zanzibar, utaonekana mpumbavu.! hari si shwari tena hakuna hiari tena, yale ya lazima ni lazima yawe na majibu chanya! Utekelezaji wake lazima uiyumbishe CCM

  Uwazi na Uwajibikaji: Hili ni tatizo kubwa kwa Serikali hii na Chama Chake! kumbuka wakati Chadema wakipiga kelele kwamba Ufisadi umekithiri, na wakati mwingine wana-CCM wenyewe kama vile kamati ya Mwakyembe na Spika aliyepita, RAISI KIKWETE alisikika akimwambia LOWASA kwamba ni AJARI YA KISIASA, na alipita katika majimbo wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2010 akiwanyayua mikono juu akisema ni watu saaafi! leo hii anawambia hapana mjivue Gamba!!!! aliziba masikio na kushindwa kuchukua hatua wakati huo!. Wananchi wanashangaa na kukosa imani na Raisi! hari si shwari tena Kikwete Mwenyewe anaibomoa CCM!.

  Siasa za dunia na Raslimali za nchi: Tanzania siyo kisiwa, yanayotokea ktk nchi nyingine Duniani lazima yawe na impacts katika nchi yetu hasa pale yanapokutana na uozo! "that is enough a catalyst to catalyse the reaction". Watanzania hawatapendelea kuona wana raslimali nyingi na bado wanaendelea kuwa masikini wakati wenzetu huko na hasa hapa jirani Rwanda, na Kenya wao wanashamiri siye tunataabika?! Watanzania tayari wana hasira huwezi tena kuwatuliza! Wamekasirika kweli.

  Kukata Tamaa: It is too late! kutokana na hayo na mengine mengi Watanzania hawana imani tena na CCM na Serikali yake. Ni vigumu tena kuwashawishi. Wanaonekana kutaka mbadala!. Weka tena watafiti wenu akina REDETI wawape majibu!.

  Nguvu ya Mawasilianao:
  Watu sasa wanapashana habari kwa kasi ya ajabu! matendo mabaya yanakwenda kwa kasi! Mitandao ya kijamii imewaweka watu karibu sana tofauti na unavyofikiria! ni kama kila siku watu wanakuwa na "Indirect meetings and almost 24 Hrs" Ubaya wa CCM na Serikali yake umesambazwa kwa kasi ya ajabu! and this is irrevisible arregetations! Nguvu ya Uma kupitia Mitandao ni kubwa!. Chama na Serikali yake vinabomoka maana sasa vinamulikwa na habari zinaenea duniani kote!

  PENDEKEZO!.
  Naelewa tupo ktk wakati mgumu wa Maisha(Umeme, Mafuta, miundombinu,na Afya sasa tunamtegemea Babu) pamoja na mijadara ya kuwa na Katiba mpya. wakati hayo yakiendelea, 2015 siyo mbali. Inawezekana mapungufu yaliyopo yametokana pamoja na kuwa na katiba isiyokidhi matakwa ya Wananchi! lakini pia tupate muda wa kutosha kumjua na kumjadili Raisi tumtakaye 2015. Tumjadili kwa sifa na ikiwezekana tumjue kwa mapendekezo ya watu mbalimbali kupitia katika mitandao ya Kijamii. Maana hatutaki Raisi goigoi!, anayechekacheka, dhaifu, asiye na Makundi, Mdini, Mkabila asiyetegemea uraisi kulipa fadhira !!

  Kwa kuanza napendekeza wafuatao;
  Dr. Slaa wa Chadema-Ni Mkweli, Jasiri, ana ufahamu na anaonekana kukerwa na matumizi mabaya ya raslimali za nchi pamoja na kukerwa na umasikini wa Watanzania.
  Ndg, Samwel Sitta wa CCM: Jasiri, na mchapa kazi, na anaonekana kukerwa na matumizi mabaya ya raslimali za nchi pamoja na kukerwa na umasikini wa Watanzania.

  Endelea........................
  ANGALIZO! haya ni mawazo yangu, na si lazima yakubaliwe. Niliowataja hapo juu si kwamba nawafahamu vizuri, inawezekana wana madhaifu makubwa ambayo siyajui au mazuri zaidi ya hayo! basi tuyataje watu wajue, tumtafute kiongozi wa nchi mapema kwa kumtafiti, kumdodosa na kumuweka bayana kama ambavyo Roman Catholic na mchakato wao wa kumtafuta mtakatifu. kwa maana kwamba vyobo vinavyohusika vimeshindwa kutupatia kiongozi muadilifu na sasa nguvu ya uma kupitia mitandao ya kijamii ifanye kazi!.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Shime kwa huo uchanganuzi makini!!!!!!
   
 3. MLAU

  MLAU JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2017
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 4,498
  Likes Received: 3,068
  Trophy Points: 280
  Mmmmh
   
Loading...