Hali ya hewa ya Mbeya inakera sana

Hali ya hewa ya Mbeya inakera sana

Saguda47

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
11,751
Reaction score
21,970
Wakuu habari za muda huu?

Mada yangu inajikita kwenye Hali ya hewa ya mkoa wa Mbeya hasa Rungwe na Mbeya mjini.

Mkoa wa Mbeya kiufupi hauna kipindi Cha kilele Cha kumuacha mtu awe huru badala yake watu ni watumwa wa Hali ya hewa kuanzia January Hadi September kila mwaka.

A. Kuanzia January Hadi April - mvua za muda mrefu na manyunyu yasiyo na ukomo

Changamoto:- Tope, maji kutuama hovyo kutokana ubovu wa miundombinu maeneo mbali mbali kama vile Kabwe, Mwanjelwa, Ituha n. k
  • kukosa uhuru wa matembezi na mazoezi hasa jogging
  • kuvaa masweta, jacket na Makoti muda mwingi

B. Kuanzia Juni Hadi Agosti - Baridi Kali sana na upepo ukiambatana na vumbi maeneo mengi ya mji.
- kiukweli ukiacha maeneo kama Njombe, Mafinga, Arusha n. K, basi Mbeya Kuna Baridi ya hovyo sana.
Mfano Leo ( jumatano, Julai 9, 2025) jotoridi ni 9°C
Changamoto: kama una afya mgogoro lazima uibuke na homa, kupauka na kukauka hovyo ngozi ( kuwa kijivu😂)
  • muda wote uvae Sweta zito, jaketi au koti.
  • matembezi hayafai kabisa, ni kukaa ndani baada ya kazi.

C. Mwezi Septemba Hadi Novemba- jua Kali na vumbi.
- ukivaa vizuri uwe na usafiri wako, usitembee umbali mrefu.

Pamoja na karaha za mkoa huu, Mbeya Ina Raha zake.

1. Vyakula bei nafuu.
Mfano, viazi ( vitamu na mviringo), matunda bwerere ( ndizi, parachichi, tikiti maji, n. k), mahindi, mihogo, Michele,
- Nyama hasa kitimoto Kwa walaji wake.
2. Starehe.
- viwanja muhimu Kwa wapenda starehe kama vile MBEYA PAZURI, NASOMA, MWAIRUBI, Baa maarufu kama JJ Njora n. k.
 
Shokaga kaya bageshi. Misungwi huku hali ya hewa safi sana! 😂

20230723_160521.jpg
 
Back
Top Bottom