KERO Hali ya Barabara Ipole – Tabora ni mbaya hasa mvua ikinyesha

KERO Hali ya Barabara Ipole – Tabora ni mbaya hasa mvua ikinyesha

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,420
Reaction score
5,024
Hiki ni kipande cha Barabara inayotoka Ipole – Tabora kuelekea Mbeya, hali ni mbaya sana, wananchi tunateseka kwa kushindwa kupita kwa utulivu.

Kuna muda abiria tunalazimika kushuka ili gari liweze kupita na kuvuka mashimo yaliyopo hapo hasa nyakati za mvua.

Serikali ifanye kitu kuhusu Barabara hiyo kwani tuoteseka ni sisi Wananchi tunaotumia kila siku.

1773649728603.png

Ipole 3.jpg

Dah!Barabara ina tope kama mnaelekea "selamagazi" kusensemya?Wapigieni kelele wafanye jambo.
 
Tanzania hii ni wapi pana afadhali kipindi cha mvua, hata Dar haifai, ukiingia ndanindani ni kichefuchefu.
 
Kutoka Sikonge (Ipole) hadi Mbeya (Makongolosi) hicho Siyo kipande, ni distance Kubwa Tu (370 kilometers). Ni kama limeshakuwa fupa gumu lililowashinda Serikali kulifanyia kazi.
Tangu na tangu zimepigwa kelele kuhusu kuunganisha mtandao WA barabara, kwa kiwango cha lami, kutoka Mbeya to Singida na Mbeya to Tabora lakini Serikali ni kama vile imeziba masikio. Haitaki kuwatatulia wananchi wake kero iliyopo tangu miaka ya Uhuru. Hadi ziara za viongozi WA serikali zinafanywa kuhusu hiyo barabara lakini hatimaye hàkuna la maana lolote linalofanyika.
 
Hiki ni kipande cha Barabara inayotoka Ipole – Tabora kuelekea Mbeya, hali ni mbaya sana, wananchi tunateseka kwa kushindwa kupita kwa utulivu.

Kuna muda abiria tunalazimika kushuka ili gari liweze kupita na kuvuka mashimo yaliyopo hapo hasa nyakati za mvua.

Serikali ifanye kitu kuhusu Barabara hiyo kwani tuoteseka ni sisi Wananchi tunaotumia kila siku.

Mbona hiyo barabara ni nzuri tu. Sijaona ubaya wake.
 
Hiki ni kipande cha Barabara inayotoka Ipole – Tabora kuelekea Mbeya, hali ni mbaya sana, wananchi tunateseka kwa kushindwa kupita kwa utulivu.

Kuna muda abiria tunalazimika kushuka ili gari liweze kupita na kuvuka mashimo yaliyopo hapo hasa nyakati za mvua.

Serikali ifanye kitu kuhusu Barabara hiyo kwani tuoteseka ni sisi Wananchi tunaotumia kila siku.

Yale mazwazwa na mazezeta yatakwambia hayana deni na mama yao.
 
Hii barabara ilikiwa katika mpango wa ujenzi baada ya ile ta Manyoni - Tabora Sikonge - Ipole hadi Mpanda kukamilila.

Sasa sijui kama Serikali ya tarehe 29th October kama bado ina mpango nayo. Ila ni bonge la chocho yaani kuikamata Mbeya kutoka Mwanza - Tabora ni fastaa tu kama unapuliza moto wa mabua.
 
Back
Top Bottom