Hali tete vyuo vya VETA Tanzania

Hali tete vyuo vya VETA Tanzania

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Chuo Cha VETA nchi nzima, wafanyakazi hawajalipwa mishahara mpaka leo, pamoja na kuhusu zote zilizofanywa na Baraza la chama chama Cha wafanyakazi kwenye maeneo husika, japo kumekuwa na tetesi kwamba leo tar4 pesa imeanza kuwekwa.. kinyume na Ahadi za Rais mwenyewe kwamba mishahara inawahishwa kwa wakati na kuwa yote itatolewa kwa wakati mmoja kwa watumishi wote, na kuwaambia watanzania kwamba hakuna ugumu wa maisha..

Pesa za kuendeshea chuo ambazo hutolewa kila mwezi, kwaajili ya mafunzo (skills development levy), haijapelekwa vyuoni tangu mwezi wa 4 (April), wanafunzi hawafanyi mafunzo kwa vitendo, na Ada wanalipa kwa wakati, na Ada hiyo ikilipwa ndani ya siku tatu inatakiwa kupelekwa benki kuu (BOT), na huu ndiyo utaratibu mpya aliojiwekea magufuli na serikali yake kukusanya fedha zote kwenda serikali kuu kwaajili ya maendeleo ya serikali na sio wananchi.

Moja wapo ya chuo Cha VETA nchini, chuo Cha hoteli na mafunzo ya utalii Arusha (Njiro), magari yake yamepakiwa hayajafanyiwa maintenance, na hayana mafuta, kwasababu fedha hakuna, zote zinakusanywa zinakwenda benki kuu.

Chuo hicho, kinadaiwa fedha na wazabuni, kinadaiwa umeme na Tanesco, kinadaiwa maji, na bado hakuna serikali kuonekana ikichukua hatua..

Kama mishahara imeingizwa leo, kwa maana ya tar4, Basi ni baada kusikika fununu kuwa suala hili lilikuwa linaratibiwa kufanyika mgomo wa wafanyakazi wote, na kumhoji mkuu wa chuo hicho.. mbaya ni kwamba hata sekretariet ya chama Cha wafanyakazi nayo imewekwa mfukoni mwa serikali, Jambo linalowafanya watumishi kukosa wa kuwasemea.

Wafanyakazi wa chuo Cha VETA wamelalamika na kudai kuwa, mkuu wa chuo hicho hajalipa uzito suala hilo kwasababu yeye aliteuliwa kutoka chuo Kikuu, na mpaka Sasa mshahara wake unatoka chuo Kikuu Cha DSM, huenda ndiyo sababu yeye haoni shida kutokuwashughulikia watumishi wengine maslahi Yao kwa wakati.

Watumishi wa chuo hicho wanahoji, inawezekanaje kuzungumza kuhusu ujenzi wa viwanda ilhali unaua chuo Cha ufundi stadi (vocational)?????

Chuo Cha VETA (Njiro) jijini Arusha mfano, lakini karibu vyuo vyote nchini vilivyo chini ya mamlaka hii ya mafunzo ya ufundi stadi VETA, hali ipo hivyo, na maeneo mengine Hali ni mbaya kuliko hata hapo Njiro jijini Arusha (VETA).
 
VETA = Vi-Wonder ila habari yako haiko sawa Ni Chuo kimoja au vyote coz maelezo Na heading tofauti
 
Na huyo jamaa anajua kujiliza siku ya mei mosi nilisema huyu jamaa ni kuwa makini sana kauli zake. In fact huyu ameshakuwa mwanasiasa mbaya asieaminika kwa kila neno alisemalo.
Hapa ni kuangalia ustaarabu wako badala ya kulalamika
 
Back
Top Bottom