Mwalimu Makini
Member
- Dec 5, 2009
- 65
- 23
Pamoja na Waziri Mkuu kuamuru kuwa wale wote waliokamatwa kwa uchochezi wa matukio ya vurugu Mtwara waachiwe hali ni kinyume kabisa kwani kila siku watu wanakamatwa hovyo. Kwa sasa watu wanakamatwa kwa kosa la kuwa wananchama wa CHADEMA. Jana huko Lulindi kata ya Namalenga kijiji cha Mitesa mwenyekiti wa kijiji hicho kupitia CHADEMA aitwaye GHADAFI amekamata saa 6 usiku na polisi wa Masasi. Alikamatwa pamoja na kaimu mtendaji wa kijiji hicho.
Jana hiyo hiyo yapata Mahabusu 110 walifikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya mwanzo. Kwa kuwa mahakama ya mwanzo ilichomwa moto hakimu alilazimika kuwasomea mashitaka yao katika chumba cha hakimu mkazi. Kosa kubwa linalowagharimu viongozi na wanachama wa CHADEMA ni kukutwa na kadi ya CDM. Kwa sasa imewalazimu wananchi kutembea na kadi za CCM kama njia pekee ya kunusurika na kukamatwa na polisi ambao wengi wao wametoka Tunduru na Songea.
Askari hawa wakija kukamata watu wanapora vitu mbalimbali vya ndani. Ukikutwa una TV unadaiwa risiti kama huna wanaichukua. Viongozi wote wa mashina wa CDM wamekamatwa. Kwa kweli hali ni mbaya sana. Hakuna chombo cha habari hata kimoja kinachotoa taarifa ya mambo yanayotokea huku. Wananchi wanadai kwamba vyombo vya habari vimenyamazishwa.
Viongozi kadhaa wa CHADEMA wa Masasi na karibu mkoa wote wa Mtwara wako katika wakati mgumu sana. Baadhi wamekimbia majumbani mwao na sasa wengine inasemekana kwamba wameenda DSM kujificha.
CCM wameamua kutumia jeshi la polisi kuhakikisha kwamba wapenzi, wanachama,viongozi na mashabiki wa CHADEMA wananywea na kuogopa kabisa kujitambulisha na chama chao. Hii sasa ni nchi ya vitisho. Sioni kama tutafika tuendako. Hali ni tete sana huko Mtwara.
Dumisha uhuru wa kupiga raia na umoja wa wenye nacho.Mungu Ibariki Tanzania , Dumisha Uhuru na Umoja,
Wake kwa Waume na Watoto..........
Nikiikumbuka versi hii halafu ikiwa inaimbwa na MCCM machozi hunidondoka.
Poleni Wanantwara
kama mulianzishe tena
Kwa sasa imewalazimu wananchi kutembea na kadi za CCM kama njia pekee ya kunusurika na kukamatwa na polisi ambao wengi wao wametoka Tunduru na Songea.
Poleni wana wa Masasi... Napenda kuwapa faraja kwamba haya yote yatapita na mwisho mtashinda..
Hakuna majeshi, polisi,mahakama, mabomu na nguvu zote za uovu zimewahi kushinda nguvu ya umma.. hata kama wakileta majeshi yote ya nchi hii na kuazima ya jirani bado ukweli utabakia palepale na nguvu ya umma itashinda.
Msife moyo kwani wa tz wapenda haki wapo pamoja nanyi na tunawaombea kwenye wakati huu mgumu...
Msiache kupambana kwa umoja kwani utengano wenu ni nguvu kwa adui yenu... TUTASHINDA ... WAO WANA JESHI SISI TUNA MUNGU