dSamizi
Senior Member
- Jan 2, 2016
- 106
- 54
Nimepokea taarifa za majambazi kuvamia na kuua mtu mmoja pale Kitahana Center Wilayani Kibondo. Naungana na wanafamilia kuwapa pole kwa msiba huo lakini tunawaombea majeruhi na wote waliothirika na tukio hilo wapone haraka. Sasa natoa wito kwa serikali kuchukua hatua kali na za dharula kwa wahusika. Kwanza ifahamike kua matukio ya ujambazi yalipungua xna karibu na kuisha mkoani Kigoma baada ya wakimbizi kuondoka kuanzia 2008. Sasa tukio la jana ni ishara kua ujambazi umerudi baada ya wakimbizi kuja tena. Tunaomba Mkuu wa mkoa aombe askari wengi ikiwa ni pamoja na kutumia mbinu zake za kijeshi (km ilivokua kwa DC Lut. Canal Mzurikwao, tunampongeza) ili kudhibiti kuzagaa kwa wakimbizi vijijini. Pia majambazi wengi inasemekana huwa ni wanajeshi waasi hivyo jeshi ikiwezekana lihusike.