Majambazi Saba wauawa wakipambana na Polisi Kigoma

steve_shemej

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,092
1,433
Watu 7 wanaotuhumiwa kuwa majambazi, wameauawa katika eneo la Kata ya Kumwambu, Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma baada ya kukabiliana na Polisi wakati wakijiandaa kufanya uvamizi na kupora katika kampuni ya ujenzi wa barabara ya Sino Hydro Engineering Company Ltd.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Martin Otieno, alisema tukio hilo limetokea juzi saa tano usiku baada ya jeshi hilo kupokea taarifa ya kikundi kinachopanga kwenda kutekeleza uhalifu huo.

Kamanda Otieno alisema kufuatia taarifa hizo, kikosi kazi kilijipanga kwenda kuimarisha ulinzi katika maeneo ambayo walipanga kujificha na baadaye kuona kundi la watu 12 wakitembea kuelekea kutimiza adhima yao na walipobaini kuwa wanafuatiliwa walianza kuwarushia risasi askari na kuibuka majibizano ya risasi yaliyodumu kwa takribani dakika 25.

Pia, Kamanda Otieno alisema katika majibizano hayo askari waliwaua majambazi watatu hapo hapo na wanne walikufa njiani wakati wakipelekwa hospitali ya wilaya ya Kibondo huku wengine watano wakikimbia kusikojulikana.

Jeshi hilo pia limekamata bunduki tatu zilizotengenezwa kienyeji, pisto moja, risasi 89 za SMG, 15 za pisto na kofia za kuficha sura ambazo zilikuwa zikitumika katika uhalifu.
 
Kuua kwa njia yeyote kwa dhumuni lolote ni dhambi.

Sisi tunapiga risasi RAIA wetu walioenda kuimba kwenye kampuni la kichina ,huku wachina wakiwabagua waafrica wenzetu
 
Sijawahi kusoma mtuhumiwa wa ujambazi akilelekwa hospitali na polisi na kufika hositali. Wote hufia njiani.

Labda sasa kazi ya kupeleka majeruhi wa ujambazi isifanywe na polisi - nahisi huenda kuna jambo la "the dead don't tell stories"
 
Kwa akili yako inayokutosha unadhani wanamuibia mchina?

Na je unadhani wangeua mlinzi angekuwa mchina?

Unadhani ujenzi wa bara bara ukichelewa kukamilika anayeteseka ni mchina?

Kuua kwa njia yeyote kwa dhumuni lolote ni dhambi.

Sisi tunapiga risasi RAIA wetu walioenda kuimba kwenye kampuni la kichina ,huku wachina wakiwabagua waafrica wenzetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Polisinwapo trained mzee majambazi wengi kama mimi hapa hatuna mafunzo so uwezekano wa jambazi kuibuka mshindi mdogo na pia mara nyingi huwa wanapigwa ambush

Sent using Jamii Forums mobile app

Aisee...kwamba majambazi hawapo trained sio kweli..Mara nyingi umeshasikia majambazi yenye background ya majeshi yetu ya ulinzi na usalama. Halafu kwenye huko unakokuita kuibuka kwa ushindi inamaana wao hata kujeruhiwa tu Hamna?

Halafu kama wanapigwa ambush,huko kutupiana risasi tunapoambiwa kila siku kunawezekanaje?Halafu ambush gani ambapo mnakamata majambazi saba huku matano yakitoroka?Na wote waliokamatwa wamekufa...?
 
Back
Top Bottom