Hali ni tete TFF, Takukuru mfuatilieni Malinzi

aka2030

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
2,650
3,662
Yamkini hali si shwari kwa wafanyakazi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) makao makuu yaliyopo Karume, kufuatia kudai mishahara yao ya miezi miwili na nusu.

Tangu kuingia madarakani kwa Jamal Malinzi hali ya taasisi hiyo imekua mbaya kila kukicha mpaka kupelekea kushindwa kuwalipa mishahara watumishi wa taasisi stahiki zao tokea mwezi Machi, 2016.


Habari za ndani zinasema hiyo imetokana na Malinzi kuwa na matumizi ya ufujaji wa pesa za TFF kwa maslahi yake binafsi, kwani yeye ndio anapanga matumizi ya taasisi hiyo kwa kutazama sehemu alizo na masilahi nayo, huku akiwaacha wafanyakazi wakiungua na jua.

Suala hili linaonekana kuwa sugu, wafanyakazi hawajalipwa mishahara ya mwezi Machi, Aprili na sasa ni katikati ya mwezi Mei, na hakuna taarifa wala dalili ya kupata mishahara yao hivi karibuni.

Rai kwa serikali, PCCB, wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo naombeni mfuatilie na kuichunguza hii taasisi muhimu nchini kwa kuwa na matumizi ya kufuja hela na kutowathamini watumishi wake.

Mfanyakazi ambaye hajalipwa mishahara yake kwa miezi mitatu, unategemea anaishije? Hapo ndio chanzo cha kuomba rushwa kwa viongozi wa vilabu?

Kwa nini kipindi cha Malinzi hali imekua tete TFF kifedha tofauti na utawala wa Tenga? Tenga aliwathamini wafanyakazi wake kwanza , huku Malinzi akiwathamini marafiki zake.

wafanyakazi wako wamezidi kutuomba hela mitaani wengine tunawadai madeni makubwa mpaka sasa au wataka tuwaaibishe baba uwe na aibu
 
ZILE AKAUNTI ZAO TRA zimefunguliwa?
bado ila jamaa anawafanya wafanyakaz,wake wakishi kimaskini sana toka akaunti zifungwe hela zote za wadhamini mapato yeye ni kujiandikia safari tu
 
tukiwa wakweli tukaacha unafiki, jamali hafai kabisa wala hafit kuwa mwenyekiti wa tff, hyu angeweza kuwe mwenyekiti wa chama cha ngum, hapo labda angemdu ila mpira, i mean soccer, / kandand hapana hawezi, hana mvuto wa kuwa mwanampira....

kiujumla anaweza kuwa na kazi nyingine ila mpira hpn
 
tukiwa wakweli tukaacha unafiki, jamali hafai kabisa wala hafit kuwa mwenyekiti wa tff, hyu angeweza kuwe mwenyekiti wa chama cha ngum, hapo labda angemdu ila mpira, i mean soccer, / kandand hapana hawezi, hana mvuto wa kuwa mwanampira....

kiujumla anaweza kuwa na kazi nyingine ila mpira hpn
Lawani Ni kwa wale waliomchagua na kumpa madaraka makubwa kuliko uwezo wake
 
Back
Top Bottom