Baba Kapompo
JF-Expert Member
- Sep 11, 2013
- 1,344
- 468
Nimependa sana aina ya ujuzi ulionao, sina ushauri mzuri ila kama uko serious na mambo yakiwa tight kabisa nenda pale KK security lazima watakuchukua wakati huo unatafuta namna ya kuchomoka, but hii ipe final option
Pole mkuu Mungu atasaidia naamini hujapoteza muda wa mtu kwa namna yoyote ile.
Habari zenu wana JF
Nimerudi tena jamani toka pale nilipoomba nafasi ya kujishkiza/kuvolunteer ikawa imeshindikana nikawa nakomaa na vibarua vya hapa na pale .But kwa sasa nimelazimika kusitisha masomo yangu (Dip of CMPTR SCIENCE) kutokana na na matatizo ya kidunia na uchumi...leo nimekuja kwenu coz naamini labda kusoma sio bahati yangu so wacha niangalie upande wa pili wa maisha .Jamani natafuta ajira aina yoyote narudia yoyote ile ila nisivunje sheria za nchi hii na iwe legal..maisha yanakuwa magumu upande wangu nitafurahi sana kama mwenye kufahamu wapi naweza kupata ajira (viwandani,makampuni,ujenzi,etc) Kitaaluma mimi ni form four, nina certfct ya infomrtion cmmnctn and technology. second semister nimeishia 2Nd semister in diploma of computer science.. uzoefu nilionao kutokana na kuhangaika kwangu
1.mimi ni blogger mzuri tuu(kutengeneza na kuendesha)
2.nina uzoefu wa kazi ngumu (ujenzi/zege/kupauwa/blandaring and fishering but sio professionala wa hizo kaz coz sijasomea na ktk harakat za kuhangaika tuu)
3.computer maintance,nipo vizuri kwenye mambo ya computer network pia computer application etc
4.naamini kazi yoyote inayohitaji nguvu ntamudu pia koz ni mwanaume ilimrad mkono uende kinywani (legally)
5.kazi yoyote ambayo unajua hii haihitaji Elimu ya juu masterz <PHD< etc me naamini ntaweza tuu kulingana level yangu
Jamani kwa yoyote aliye tayari kunisaidia kimawazo,au kama umeskia wapi nnaweza kupta ni vyema kuambiana ila najua wengi mtakuja na mawazo ya kujiajiri (napenda kujiajiri na ninaziona njia nyingi za kutoka tatizo mtaji) lengo nipate mtaji kupitia ajira then nijiajiri
ni PM
AHSANTE kwa kupoteza mda wako wa kusoma uzi wangu na unisamehe kma utakuwa umeboreka na huu uzi
Nawasilisha
Nadhani una agenda nyingine unataka tujue sio hii ya kumsaidia Mpwa wetu, na sijui umetumia vigezo gani kulinganisha WaTz na Wakenya! Ungekuwa una maarifa kidogo ungejua kuwa watu hawafanyi kazi kwa kutumia utashi wa mtu bali kwa kufuata ToR zilizoko kwenye Contract yenu......Daahhh nina project yangu, i think ungenifaa sana tuunganishe nguvu pamoja but tatizo sijafahamu attitudes zako nami hufahamu zangu! Km ujuavyo watz kwenye issue ya partnership in business are lowly rated compared to wenzetu wakenya et all kisa hawakawii kuzingua! Keep fighting brother one day yes! God may bless you!
Kaka wah peleka cv zako erolonk huenda watakuita mkuu
Sasa hapo umemsaidia nn,au ndo misifa unaproject yako?mwenzako anashida ujue..Daahhh nina project yangu, i think ungenifaa sana tuunganishe nguvu pamoja but tatizo sijafahamu attitudes zako nami hufahamu zangu! Km ujuavyo watz kwenye issue ya partnership in business are lowly rated compared to wenzetu wakenya et all kisa hawakawii kuzingua! Keep fighting brother one day yes! God may bless you!
kwa kuangalia avatar yako naona ni yuleyule mwenye nguvu asili za kuongea na maiti. pepo linalokupa nguvu ya kuongea na watu waliokufa ndo linakuharibia kibali chako, okoka, fanyiwa maombezi kazi nzuuri itajileta yenyewe
hauhitaji daktari wa kukupima akili wewe ni wakupelekwa direct milembe maana comment yako na uzi ni vitu tofauti kabisa.. nakushaur km ulidhamiria kukoment hiv kwenye huu uzi bhas ntakusaidia hata namba ya daktar