Natafuta kazi yoyote itakayoweza kuniingizia kipato

90sgeneration

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
275
375
Habari za wakati huu wana JF

Nitoe shukrani kwa mtu alienipatia wazo nianzishe thread hii hapa ili watu tofauti tofauti wasome na huenda nikapata mawazo au njia nzuri ya kusaidika.

Mimi ni kijana, nina 26 years sasa, na suala kubwa lilonifanya kuandika hapa ni kutafuta msaada wa kupata kazi. Kazi yoyote ambayo itaniwezesha kuingiza chochote, japo lengo hasa ni kupata kipato kitakachonisadia niweze kumaliza elimu yangu.

Kwa sababu mbali mbali japo kubwa ni kukosa funds kulifanya nishindwe kumaliza elimu yangu, nilifika hadi forn 6 na nikashindwa kuendelea sababu ya kukosa fedha, nikaenda IFM kusoma diploma ya insurance and risk management kwa cheti cha form 4 sababu nilipata ka ajira ka muda ila haikudumu hata 6 month sababu boss alipatwa na majanga hivyo sikumaliza pia.

Nikaamua nisitishe kwanza kusoma (japo ilikua ndio matamanio yangu nimalize degree ila njia zote zilifail) nikaingia mtaani kutafuta kazi, na nimefanya kazi maeneo kadhaa na niliaminika sana sababu ya uwezo wangu, sitaongelea sana ili isiwe ndefu.

Ila ajira yangu ya mwisho iliisha sababu nilipata kuugua stroke kwa muda mrefu na sasa nimepona ila kila navyojaribu kutafta ajira nakosa, nyingi ambazo naweza na naamini ningepata elimu inaniangusha.

Hii kitu inaniuma sana ndugu zangu, naumia sana, naona niliosoma nao wamemaliza wote degree zao na wengine wanaendelea vizuri sana ila mimi umasikini unanirudisha nyuma, naumia sana, naumiaaa, hata mtaji nakosa, nakosa hata elf 2 ya kutumia kwa siku, na umri unazidi kwenda.

Nimeazimia kurudi shule na kuhakikisha namaliza, na nitasoma open university ili niwe na uhuru wa kufanya kazi, ila nahitaji wa kunishika mkono, sihitaji msaada wa pesa au mahali pa kuishi (japo kama itatokea nitakubali), nahitaji kupata kazi, yoyote ile mtu akiweza aniunganishe tafadhari, iwe skilled or unskilled.

Huyu ndio mimi kwa kifupi:-

- Fluent in both English na Kiswahili.

- Computer Literacy - I know a lot about Microsoft Programmes, Excel, Publisher etc sababu nimeshafanya kazi mahali flani flani kwenye private companies na nilitumia hizo kuandaa reports zote, researches na annual budgets etc. Pia sababu nilianza kutumia computer tangu mdogo hivyo nafahamu mambo mengi kuihusu.

- Nina uzoefu wa kufanya kazi kwenye retail business kama cashier, stock controler, cleck, loss control manager (best award), sales (best award) and marketing na pia operations (kumanage kampuni hasa za retail) zote kwa ujumla na nina proof ya mafanikio yangu na awards kwenye hili, sitaelezea sana unless mtu atahitaji kufahamu zaidi.

- Nimewahi fanya kazi mbali mbali, kwa kifupi ni kwamba naweza fanya kazi yoyote ile hata kama sijawahi ifanya, as long as tapewa maelekezo ya msingi, iwe shambani, ujenzi, biashara, call center jobs, cashier, pia nina mawazo tofauti tofauti ya biashara ambayo kama mtu ana mtaji na anataka nimpee basi nitakupatia sababu sio mawazo tu bali nimeshakua kwenye field.

-Pia hata wale ambao hawawezi niajiri ila wana kazi ambazo naweza fanya kwa commission pia nipo tayari, iwe insurance, real estate agents, sales and marketing etc, yani hata kama una duka lako na niwe nakuletea wateja its ok, hasa hasa hapa wale wa electronic shops, maduka ya simu, maduka ya viatu, maduka ya retail kwa ujumla, yes i can do it.

Please, naomba mnishike mkono, baba, mama, dada na kaka zangu nawaomba, any terms and conditions niko tayari kufuata, hata kama mtu anataka kunisaidia ada nimalize masomo yangu au mtaji kodogo pia karibu.

Tena kama ni ada wala usinipe mkononi bali ni kulipia chuoni moja kwa moja, kama mtaji basi pia utakua sehemu ya biashara yangu kama CEO na hakika nitarudisha gharama zako na faida juu. Kama ni kazi pia nitafanya vile unataka sababu huwa na deliver the best always.

Vile elimu yangu hua inafanya nakosa confidence kutafta kazi na qualification ya education inaniangusha sana.

Please please please. Email yangu ni jackyrevocatus@yahoo.com au unaweza kuja dm nikupatie namba zangu za simu moja kwa moja.

Natanguliza shukrani na asante kwa kusoma, pia nakaribisha maoni na mawazo mbalimbali na ushauri.
 
Kwanza kabisa nikupe pongezi kwa kipaji ULICHO nacho.

Mungu ameweka kipaji Kikubwa sana ndani yako.

-Nimejaribu kuangalia uandishi wako upo vizuri sana.
-Uwezo wa kujieleza upo juu sana.
- Hata MATUMIZI ya Compyuta nk
Hongera sana Mdogo wangu.

Nikupe pole sana Kwa stroke.
Lakini namshukuru Mungu Kwa kuwa umepona.

MUNGU HAMTUPI MJA WAKE.

USIKATE TAMAA endelea kumtegemea MUNGU.
 
Hii dunia hata sijui inakwenda wapi, yani miaka 26 tayari stroke imeshakutandika!!

Pole sana, waliomshauri Samia kutowa scholarship za sayansi wamempoteza, vijana kama hawa ndio wanastahili Samia scholarship.

Anyway usife moyo, kama maelezo yako yote ni genuine utashikwa mkono.

Cc: Maxence Melo thread kama hizi muwe mnazifanyia verification bado watu kwema wapo kwenye jamii.
 
Mkuu unajieleza mpaka basi inavutia kama wewe sio muhaya basi una kipaji mengine utajifunza mbele ya safari kusoma sio muhimu hili pia utalijua badae, pesa ndio kila kitu pia hili utalielewa uko mbele kidogo.

Naimani umeshajipambanua vya kutosha kama una uwezo wa kuleta wateja kwenye maduka nenda kwa wenye maduka washawishi fanya hivyo baadae chukua bidhaa katembeze mtaani ...utakuwa na utatoka.

Ndiyo ukisoma utaajiriwa japo sio garantee wasomi wamejaa elimu uliyonayo inatosha kabisa isiwe ndio kigezo. Usichoke kuomba na tambua kuwa wema hufa mapema.
 
Amen, asante mkuu.
 
Amen, na nipo tayari kufanyiwa verification na yote nilioandika ni sahihi kama mtu atataka kujiridhisha kwa vithibitisho pia.
 
Mkuu unajieleza mpaka basi inavutia kama wewe sio muhaya basi una kipaji mengine utajifunza mbele ya safari kusoma sio muhimu hili pia utalijua badae, pesa ndio kila kitu pia hili utalielewa uko mbele kidogo.

Naimani umeshajipambanua vya kutosha kama una uwezo wa kuleta wateja kwenye maduka nenda kwa wenye maduka washawishi fanya hivyo baadae chukua bidhaa katembeze mtaani ...utakuwa na utatoka.

Ndiyo ukisoma utaajiriwa japo sio garantee wasomi wamejaa elimu uliyonayo inatosha kabisa isiwe ndio kigezo. Usichoke kuomba na tambua kuwa wema hufa mapema.
Amen Mkuu, na asante kwa ushauri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom