Tanki
JF-Expert Member
- Apr 7, 2013
- 538
- 248
Amakweli vita vya panzi furaha kwa kunguru.
Hivi serikali inajua kuwa huku kwetu ( Kivule - Gongo la mboto ) kuanzia juzi yani baada ya mafuriko na kuvunjika daraja lililo karibu na Kivule Shule nauli ya mwanafunzi imekuwa shilingi 500 badala ya shilingi 200. Wakati watu wazima wakilipa shilingi 1000 badala ya 500.
Tena hapo kwakuwa daraja halipitishi gari isipokuwa watembea kwa miguu tu. Hivyo inatubidi tutembee kutoka kivule mwisho hadi tuje kuvuka daraja kwa juu kuna kituo kinaitwa Muembeni hapo ndo unakuta gari. Lakini licha kutembea umbali mrefu hadi kufika hapo lakini bado tu tunalipishwa 1000 na wanafunzi wanalipishwa 500. Hiyo hata ukiwa Banana unataka kuja Kivule bado tena nauli ni 1000 na mwanafunzi 500. Hali ni tete sana. Cha ajabu hadi magari ya UDA nayo yanafanya hivyo hivyo 1000 kwa 500.
Wito wangu : Serikali tunaomba mtutupie jicho la huruma. Watu mnaohusika na maswala ya usafiri mje huku Kivule - Gongo la mboto msaidie wananchi dhidi ya huu uhalamia.