Siri ya sifuri
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 2,024
- 1,526
Habari zetu wakuu?
Hali si hali huku kitaa kila Mtu na lake. Huwezi tena kumfahamu anaelipwa mshahara au anaepewa posho labda uwe unaijua ofisi yake, ila kwa huku kitaa hakuna tofauti ya wazi utakayoiona baina yetu
Kila mmoja wetu anajaribu kujionesha yupo kwenye hali mbaya, kipindi kigumu ili asijekuombwa msaada, Si ndugu si jamaa si rafiki wala si mwengine yeyote yule ambaye angeweza kukufaa pindi unapokwama anaeonesha utayari katika kipindi hiki.
Tumekua wabinafsi kupitiliza kuliko kipindi kingine chochote kile. Leo hii Mtu anafikiria kujibu hata Salaam!!kumjulia hali jamaa yako mpaka ujishauri Mara nyingi ukihofia majibu!!yaani kabla ya Salaam kwanza unafikiria majibu, vipi akinijibu hali mbaya nitawezaje kumsaidia!? Anaesalimiwa naye anafikiria"si bure anajambo huyu nikimjibu tu ataniripua; atanililia shida.
Kila Mtu sasa hivi anapigania nafsi yake, tunalazimishwa tusiaminiane kwa maana kikulacho kinguoni mwako, na kila Mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe. Tunaishi kwa tahadhari ya hali ya juu kiasi kwamba hata mshirika wako unamhofia!? Ni hatari kwakweli lakini tutafanyeje maana hali hii imeandaliwa haikutokea tu kwabahati mbaya, ndivyo Mheshimiwa anavyotaka.
Mwenye-ez-Mungu atuwezeshe tuyashinde majaribu haya na kisha turejee kwenye hali ya umoja na mshikamano. Amiin,Amiiin.