Hali Ikoje Kuhusu Fao La Kujitoa?

Hali Ikoje Kuhusu Fao La Kujitoa?

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
854
Nimekuwa napata shida kidogo kutokana na maoni ya watu kuhusu hotuba ya Rais alipokutana na wadau wa mifuko ya hifadhi ya jamii, vyama vya wafanyakazi na wengineo. Katika hotuba hiyo, Rais alinukuliwa akisema kwamba, utaratibu wa zamani katika kikokotoo na kabla mifuko haijaungwa urudi kwa kipindi hiki cha mpito ambacho kitakwenda hadi mwaka 2023.

Kutokana na kauli hiyo ya Rais, kumekuwepo maoni tofauti tofauti kuhusu sheria mpya iliyosainiwa na Rais. Wapo watu wanasema kwa kauli ya Rais, basi hata sheria iliyosainiwa na yeye imekuwa nullified, na kama imekuwa nullified, basi utaratibu wa zamani ndiyo utatakiwa kutumika mpaka hapo kutakapokuwa na utaratibu mwingine ambao utashirikisha wadau wa pande zote.

Ningependa kufahamu haya: Je, lile Fao pendwa maarufu kama FAO LA KUJITOA pia litatolewa kwa kipindi hiki cha mpito? Pamoja na hilo, pia ningependa kujua kuhusu mengineyo ya sheria hiyo. Je, wale ambao walikuwa wakiacha kazi kwa hiyari (resignation) sasa watapata fao hilo? Je, wale waliopunguzwa kazi watapewa pia mafao yao kwa asilimia mia moja? Je, lile fao la upotevu wa ajira ambalo kimsingi utaratibu wake ni wa kinyonyaji na kandamizi, ndiyo kusema limesitishwa?

Nawasilisha.
 
Jamani mmoja wa wasemaji wa hiyo mifuko ya hifadhi ya jamii ajitokeze atupe maelekezo hapa kwenye jamvi ili kupunguza maswali katika jamii ya wafanyakazi.

Nawasilisha...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa nashangaa sana wahusika wakuu wanapojifungia ndani ya ofisi na kusubiri Mh.Rais afafanue.

Waziri wa Kazi na Ajira ilibidi awe mstari wa mbele kufafanua hivi vitu..Na hili litakaliwa kimya mpaka Mkuu aje alisemee mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa nashangaa sana wahusika wakuu wanapojifungia ndani ya ofisi na kusubiri Mh.Rais afafanue.

Waziri wa Kazi na Ajira ilibidi awe mstari wa mbele kufafanua hivi vitu..Na hili litakaliwa kimya mpaka Mkuu aje alisemee mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa hivi ni mwendo wa timing anayejitokeza tu huyo ndio anatwishwa zigo.
 
Huyu Waziri hata mimi cmuelewi utakaaje kimya bila kutoleoa ufafanuzi juu kauli ya mheshimiwa rais. Bado jambo hili linahitaji ufafanuzi wa kina
 
Hilo la kujitoa nalisubiri sana kuna kaela kangu kangu pale PPF ni mwaka wapili sasa.
Na hakuna pension fund wasumbufu kama PPF wananiambia tunasubiri tupewe muhongozo kutoka serikalini kama kuna FAO la kujitoa.Bora NSSF ukifuatilia wanakupa chako ila huku PPF mmmmhhhh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawatoi fao la kujitoa kauli ya muheshimiwa ilikuwa ya kisiasa, hela hazipo kwa mujibu wa CAG.
 
Back
Top Bottom