hali hii mpaka lini

Chiwa

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
3,978
4,743
Mimi ni mtanzania

Ndio ni mtanzania .tena asili ya nchi yangu tena yaTanganyika na Zanzibar,
Bali nimekuwa mdanganyika nikidanganywa kila kukicha na watawala wangu,
Nilio waweka mwenyewe nikitegemea watanikomboa na umaskini wangu, kwa uadilifu wao na ahadi zao.
Lakini sasa watawala hawa wamekuwa ni kisu cha kuniangamiza.
Wananifanyia mengi kwa ujinga wangu. naendelea kuvumilia.

kama haitoshi Sasa siwawezi tena, wao wameshika hatamu na mimi ni mekuwa punda au
Farasi ninaye lazimishwa kwenda kwa kadri ya mpandaji atakavyo.
Kwa nini imekuwa hivi,kwa nini nimeendelea kunyonywa na kudanganywa?
Hali hii mpaka lini? Nimekuwa daraja la mafanikio kwa wengine na hasa katika
Vita za maslahi yao na ubinafsi wao bila kujali ni kwa jinsi gani nitaathirika.
Lililo nzuri zaidi nikishatumika hakuna anayeomba radhi
kwa mapungu aliyonitendea auKushukuru kwa kufanikisha ubinafsi wake.

Nimetumika kwenye mgomo wa madaktari na wanangu na ndugu zangu wa karibu
Yaani wadanganyika wenzangu wamekufa na hakuna aliyesema kuwa kutokana na mgomo huu,
Tumepata madhara kiasi Fulani, japo watuambie wadanganyika wangapi wamekufa hilo halipo.

Kwa kweli inauma mno na hakuna wakunitetea tena
kwani hata niliyemchagua akani saidie kusema amelewa na kodi yangu ,
ameungana nao kuniangamiza kwa kuakikisha kiinua mngongo changu
nilichoweka kwa kulazimishwa sikipati. Kama haitoshi ameamua kuchukua rushwa
kuhakikisha sioni mbele na niwe gizani nay eye aendelee kunitawala.
nimeendelea kuwa daraja kwa matumizi ya wenginie.mpaka lini hali hii jamani?

Achilia mbali namwangalia binti yangu aliyemaliza chuo kikuu kila siku anatoka na bahasha zake.
kifuani kwake kaninginiza hirizi za kithungu (flash)na naogopa hata kumuuliza
Anaenda wapi ikwa haniombi nauli wala vocha na kila siku akitoka akiwa amependeza na akirudi hana raha.
Kinachonifurahisha kama si zaidi ya kusikitika , mwakilishi wangu anasema tatizo la ajiria ni globle issue!
tena afadhali kwetu mtu anaweza kumtegemea mzazi au mlezi wake hivyo sio kubwa kama Marekani!

Inaniuma lakini sina uwezo umaskini wangu imekuwa fimbo ya kunipigia.
Mbaya zaidi wakiona nataka kutoka katika hali hii ,
wananigawa kwa kuniletea mgogoro wa kidini au kikabilaIli nisahau kinachonisumbua.

Nimeamua sasa sitaki tena kutumika ikiwa ni pamoja na kumpeleka mwanangu shule
kwa kuuza sehemu yangu ya ardhi ili mwangu atoka hapa nilipo nikitegemea ataweza kujitegemea.

lakni leo nakumbana na mgomo wa waalimu.
Wanangu wanashida nje ,wengine wanadakwa na watawala(viongozi na matajiri wasio waaminifu)
kwa ngono. wakilipwa ujira wa chips na vijisenti kidogo
( ikiwa ni sehemu ya kodi wanayoitoa wazazi wao) kwa haja zao.
hili ndilo linaniuma zaidi kwani nauhakika kuna wanafunzi wengi saa hizi wako wanafanya
ngono na tutegemee maambukizo yatakayo tokana na mgomo huu.

Watoto wao wakiwa salama wakisoma shule bora na sisi tukibaki bora shule.
Hali hii mpaka lini? Nitalalamika mpaka lini ikiwa watawala hawako tayari kusikiliza kilio changu?
Maisha ni magumu kila siku afadhali ya jana hii mpaka lini
Lakin naamini kwa imani yanngu ipo siku MUNGU atasimama kutetea na wataumbuka!
 
Subiri 2015 ,Chadema inachukua Utawala wa nchi ,Madaktari mshahara kuanzia milioni tatu,walimu kuanzia milioni mbili ,wabunge kupunguziwa mshahara kwa asilimia 45, mshahara wa chini kwa walio serikalini ni milioni moja ,wasio na kazi kila mwisho wa mwezi lakimoja.Mawaziri kupunguziwa mshahara kwa asilimia 52,Raisi kupunguziwa mshahara kwa asilimia 75 na wastaafu nusumilioni.

Hivyo uwe na subira ,karibu mambu yataiva.
 
hali hii itaisha endapo kila mtu atatimiza wajibu wake wa msingi ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha mafisadi.jipange 2015 ukombozi uleeeeeeeeeeeeeeeeee,nauona kwa mbali.
 
Ni hapo tu Watanzania watakapojua umuhimu wa kufanya maamuzi sahihi kwenye chumba cha kupigia kura bila kujali rangi ya bendera ya chama, kofia au kanga.
 
Subiri 2015 ,Chadema inachukua Utawala wa nchi ,Madaktari mshahara kuanzia milioni tatu,walimu kuanzia milioni mbili ,wabunge kupunguziwa mshahara kwa asilimia 45, mshahara wa chini kwa walio serikalini ni milioni moja ,wasio na kazi kila mwisho wa mwezi lakimoja.Mawaziri kupunguziwa mshahara kwa asilimia 52,Raisi kupunguziwa mshahara kwa asilimia 75 na wastaafu nusumilioni.

Hivyo uwe na subira ,karibu mambu yataiva.

Magari yote ya kifahari marufuku; gari la mbuge ni Rav4, posho zote zinapigwa panga, mikaataba yote ya kifisadi inafutwa, mirahaba ya uchimbaji madini ni 40% badala ya 3%, serikali inakuwa na wizara/mawaziri 17 tu, wakuu wa wilaya wanapigwa ridandansi na kazi zao zitafanywa na kurugenzi........

HAYA MAMBO MKUU YANAWEZEKANA, HILI LINCHI NI LINCHI TAJIRI JAMANI, UFISADI NI KITU KIBAYA!
 
Magari yote ya kifahari marufuku; gari la mbuge ni Rav4, posho zote zinapigwa panga, mikaataba yote ya kifisadi inafutwa, mirahaba ya uchimbaji madini ni 40% badala ya 3%, serikali inakuwa na wizara/mawaziri 17 tu, wakuu wa wilaya wanapigwa ridandansi na kazi zao zitafanywa na kurugenzi........ HAYA MAMBO MKUU YANAWEZEKANA, HILI LINCHI NI LINCHI TAJIRI JAMANI, UFISADI NI KITU KIBAYA!
Ni kweli hayo yanawezekana ila tunatakiwa watanzania wote tuamke kupiga vita vitendo vyote vya kifisadi ikiwa ni pamoja na viongozi kufanya nchi yetu ni mali yao na familia zao. Na tusipofanya hivyo 2015 tutabaki vilevile. Magamba nao wanataka kuhakikisha wanarudi kwa mbinu yoyote. Umoja wa kitaifa ni muhimu sana katika kuikomboa nchi yetu. Naamini kila mtanzania amechoshwa na hali hii. hivyo kila mmoja kwa nafasi yake asimame kuikomboa Tanzania yetu ili siku moja tufurahie raslimali zilizopo nchini.
 
Back
Top Bottom