Halal badr, tawaswil na visomo vilivyosomwa wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika

unaweka mapicha tu ya watu na 'vibagarashia' vilivyotoboka
weka ushahid wa maandishi wacha hizo ngano zako,unakuja kuleta stor za kusimuliwa hadith njoo ...uongo njoo

sasa kama kisomo dawa nyerere asingeenda uno babu zako wangesoma tu wazungu waondoke

toka uhuru mpaka sasa, ulivyozaliwa mpaka leo povu linakutoka serikali inawaonea kasome kisono kitatue matatizo yenu!

HAYA FURAHIKA NA HII PICHA YA RAISI WAKO AKIPIGA MAGOTI

14.jpg
 
Attachments

  • upload_2017-9-21_6-20-1.jpeg
    upload_2017-9-21_6-20-1.jpeg
    27.9 KB · Views: 68
Uhuru na Umoja,
Mzee Kimaro namjua vyema sana tena sana.

Alikuwa mtu muungwana na nawajua hadi wanae.

Waulize kama watanisahau ni kwa kuwa walikuwa wadogo.

Mimi sina tatizo la ghitilafu baina yetu.
Kinachonishangaza kwako na kwa wengi ni jinsi historia hii inavyowachoma.

Nadhani umesoma hapa niliyoeleza yaliyotokea mara tu baada ya uhuru katika mradi wa TANU wa kuandikia historia yake mradi ambao uliongozwa na Abdul Sykes akisaidiwa na Dr. Wilbard Klerruu.

Ikiwa umesoma utakuwa unajua kuwa wengi ndani ya TANU yenyewe walijuta kwa nini nchi ilikombolewa na hawa?

Kilichotokea ni njama za kufifilisha historia hii na wazalendo wote.

Baba yangu aliona historia yote ya TANU ikijifingua machoni pake si kwa kuwa baba yake alihusika toka enzi za African Association 1929, la hasha ni kwa kuwa waasisi wawili wa chama chenyewe Abdul na Ally Sykes walikuwa rafiki zake toka udogoni na wakimweleza kila kitu.

Lakini kwa wakati ule 1950s hakuna aliyejua kama mambo haya yatakuja kuwa makubwa kupita makamo yao.

Hii ndiyo sababu unaona mimi najua mengi katika historia ya TANU na sidhani kama kuna mtu anaweza kusimama na mie katika hili.

Muhimu kwako ni kuwa chukua tahadhari kwangu na chunga ulimi wako.

Nakuwekea hapo chini picha niliyopiga na watoto wa Abdul Sykes siku waliponionyesha Medali ya Mwenge wa Uhuru aliyotunukiwa baba yao (post humus) ambayo wao wanaamini imetokana na mimi kuandika maisha ya baba yao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

20170429_185254.jpg

Kulia: Ilyas Abdulwahid Sykes, Daisy Abdulwahid Sykes, Mwandishi akiwa ameshikilia Medali ya Mwenge wa Uhuru, Misky Abdulwahid Sykes na Kleist Abdulwahid Sykes

Wanae ni kaka kaka zangu, ingawa sasa wamebaki wawili tu. Ni kaka na dada yangu kwakua Yeye Kimaro na Baba yangu ni laka na mdogo toka nitoke. Na walikua wote Bandari ingawa Baba alikua director CMB, sijui kama walilumbuka kampuni hii?

Miaka ya ya themanini CMB directors walikua wakiendeshwa na Toyota 4x4 za nguvu mno na nadra kuona kampuni or mashirika mengine wakati huo Mabosi wa Bandari kama General Manager Joseph N Kimaro walikua wamepewa "Nissan Sendrik" Gari ndogo lakini zikitamba miaka hiyo. Nakumbuka, Jioni nilazima walinzi wa bandari lazima waje toa ulinzi kwa wakuu wa bandari, nliwaona home.

Kipindi hicho, doctor wetu alikua bwana Eden Maro, alikua hapo muhimbili, alienda masomoni Uingereza na kurudi 1991/2 na kufika nyumbani. Nilisikia alikua doctor wa Mkapa.

Anyway, nliishi maisha mazuri sana wakati wa uhai wa baba yangu na niliendelea kuishi vizuri nikiwa nyumbani kwa Baba mkubwa Joseph N Kimaro.
 
Uhuru na Umoja
Mzee Kimaro namjua vyema sana tena sana.

Alikuwa mtu muungwana na nawajua hadi wanae.

Waulize kama watanisahau ni kwa kuwa walikuwa wadogo.

Mimi sina tatizo la ghitilafu baina yetu.
Kinachonishangaza kwako na kwa wengi ni jinsi historia hii inavyowachoma.

Nadhani umesoma hapa niliyoeleza yaliyotokea mara tu baada ya uhuru katika mradi wa TANU wa kuandikia historia yake mradi ambao uliongozwa na Abdul Sykes akisaidiwa na Dr. Wilbard Klerruu.

Ikiwa umesoma utakuwa unajua kuwa wengi ndani ya TANU yenyewe walijuta kwa nini nchi ilikombolewa na hawa?

Kilichotokea ni njama za kufifilisha historia hii na wazalendo wote.

Baba yangu aliona historia yote ya TANU ikijifingua machoni pake si kwa kuwa baba yake alihusika toka enzi za African Association 1929, la hasha ni kwa kuwa waasisi wawili wa chama chenyewe Abdul na Ally Sykes walikuwa rafiki zake toka udogoni na wakimweleza kila kitu.

Lakini kwa wakati ule 1950s hakuna aliyejua kama mambo haya yatakuja kuwa makubwa kupita makamo yao.

Hii ndiyo sababu unaona mimi najua mengi katika historia ya TANU na sidhani kama kuna mtu anaweza kusimama na mie katika hili.

Muhimu kwako ni kuwa chukua tahadhari kwangu na chunga ulimi wako.

Nakuwekea hapo chini picha niliyopiga na watoto wa Abdul Sykes siku waliponionyesha Medali ya Mwenge wa Uhuru aliyotunukiwa baba yao (post humus) ambayo wao wanaamini imetokana na mimi kuandika maisha ya baba yao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

20170429_185254.jpg

Kulia: Ilyas Abdulwahid Sykes, Daisy Abdulwahid Sykes, Mwandishi akiwa ameshikilia Medali ya Mwenge wa Uhuru, Misky Abdulwahid Sykes na Kleist Abdulwahid Sykes

Picha hii nimeiona sio mara moja, umeipost si chini ya mara mbili ingawa sikujihusisha na mada husika bali nilipita kimya kimya.

kwanini unanionya niwe mwangalifu na wewe na nichunge ulimi wangu? ilhali sija kutusi or kukushambulia? Mada ziletwazo humu lazima zisomwe na wakati mwingine contents za mada hizo lazima zichambuliwe na watu wenye ufahamu, mimi nikiwa mmoja wao.

Kuwa na muono or maoni tofauti haimaanishi ya kua, mada husika inanichoma, la hasha! Katika Dunia hii, hutapata kukutana na mtu atakaye kubaliana na wewe kwa kila kitu, si wewe tu yeyote. Hakuna mtu atakuna na mtu atakayekubaliana nae kwa kila jambo, ni nature ya wanaadam.
 
Uhuru na Umoja,
Sasa unaandika kama muungwana.
Ahsante sana.

Tunaweza kuendelea na mjadala bila shida.
 
Kaka Mohamed Said , nini maudhui ya bandiko lako hili?, yaani unataka kutuaminisha kuwa Halal Badr inafanyakazi kweli na ni kitu cha kidini hasa na wala sio Shirk?

Nyerere na viongozi wengine wa TANU kufanyiwa hiyo Halal Badr ndio kumeifanya hiyo Halal Badr iwe shwahihi?

Binafsi sijakuelewa uanataka kusema nini?, kama ntakuelewa basi mtu wa kwanza ningependa asomewe hii kamà walivyosomewa Wakoloni basi ni Prof. Lipumba
 
Kituko,
Hapana sijasema mahali popote kuwa Halal Badr inajuzu.

Mimi kama mtafiti wa historia nimeeleza tu yale ambayo niliyoona katika utafiti wangu.

Unaweza kurudia kusoma bandiko langu kwa uelewa zaidi.

Kuna mengi na mengine nimeshuhudia kwa macho yangu utotoni yakifanyika ingawa siku hizi naona hakuna tena na nimeyaandikia mathalan kupunga mashetani.

Naingia maktaba nikipata kitu nitaweka hapa kwa faida yetu sote.
 
Uhuru na Umoja,
Sasa unaandika kama muungwana.
Ahsante sana.

Tunaweza kuendelea na mjadala bila shida.

Wewe hutaki or hupendi kupingwa kwa hoja unachotaka ni watu kukaa kimya.

Sidhani kama ni sahihi. Huku tutaichambua tu mada, kwa kina.

Hii ni nchi yetu sote na ni wajibu wakila mmoja wetu kufanya jambo litakalo leta tija kwa Taifa kadri ya uwezo wake: usalama, amani, upendo, mshikamano baina ya watanzania bila kujali itkadi zao za kisiasa ama kidini na usalama.

Ni wajubu wakila mmoja wetu, kukosoa, kukemea maovu ama waovu wenye mrengo wa kuvunja ama kuhamasisha uvunjwaji wa amani, upendo, mshikamano na usalama wa taifa letu.

Amani, upendo, mshikamano are among executive virtues this great nation has for so long been known for.

Tusiharibu haya kwa visingizio.

Mimi usinichukie, nipo humu, na nitaendelea kuwepo nikitimiza wajibu wangu kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.

Zidumu fikra za Baba wa Taifa, Julius K Nyerere.
 
Uhuru n Umoja,
Mbona napingwa sana hapa JF na sijatukana mtu au kutumia lugha chafu kwa hilo?

Historia hii haina uhusiano wowote na kauli mbiu za siasa na mengineyo.

Toa hofu sina sababu ya kukuchukia ati kwa kuwa unanipinga.

Tuendelee na mjadala.
Mimi hupata faraja sana ninapoisomesha historia hii kwa watu kama nyinyi ambao hamkuwa mnaijua kabla.
 
Wewe hutaki or hupendi kupingwa kwa hoja unachotaka ni watu kukaa kimya.

Sidhani kama ni sahihi. Huku tutaichambua tu mada, kwa kina.

Hii ni nchi yetu sote na ni wajibu wakila mmoja wetu kufanya jambo litakalo leta tija kwa Taifa kadri ya uwezo wake: usalama, amani, upendo, mshikamano baina ya watanzania bila kujali itkadi zao za kisiasa ama kidini na usalama.

Ni wajubu wakila mmoja wetu, kukosoa, kukemea maovu ama waovu wenye mrengo wa kuvunja ama kuhamasisha uvunjwaji wa amani, upendo, mshikamano na usalama wa taifa letu.

Amani, upendo, mshikamano are among executive virtues this great nation has for so long been known for.

Tusiharibu haya kwa visingizio.

Mimi usinichukie, nipo humu, na nitaendelea kuwepo nikitimiza wajibu wangu kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.

Zidumu fikra za Baba wa Taifa, Julius K Nyerere.

ulisahau kulipongeza kanisa Katoliki ambalo lilikuwa likimwelekeza Nyerere nini afanye katika utawala wake
 
Mohamed Said

Mimi sina habari na historia ya nani kafanya nini. Uhuru wa Tanzania/Tanganyika haukupatikana kwa vita.

Pili, mimi sichomwi na chochote juu ya mijadala yako ya kidini zaidi ya kuona ya kua wewe ni Adui mkubwa wa Amani, Mshikamano na Usalama wa Tanzania na Watanzania ukiwemo wewe.

Najua wajua ya kuwa Watu wenye akili timamu, hawajisaidii sebuleni am vyumba vya kulala; wenye akili timamu huenda Malwatoni aka Msalani.

Mimi niliandika inshu za Abadr baada ya kuona ni kwa muda sasa inshu hii imeshika hatam baada ya Wasioitakia mema inchi hii kama wewe kutaka kumuua Lisu ili ionekane ni Serikali yetu pendwa inayosomamia haki za wanyonge na yenye nia ya dhati kuleta maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa ama uhuru wetu wa kuabudu.

Nimeongea swala la Albadr na Waaarabu sio kwakua wanauhusiano wowote na uhuru na Tanganyika [kama unavyependa kuandika ila mimi naiita nchi yangu pendwa Tanzania] bali ni juu ya prejudicial beliefs wengi walizo nazo juu ya imani zetu za kidini.

Ndio maana nilitoa mfano wa Nguvu ya Albadr na Vita visivyoisha kati ya Waraabu na Waamerika na manyanyaso ya Taifa la Palestina--kama albadr inafanya kazi ilitakiwa ianze huko, inshaalah.

HITIMISHO

No matter how intellect you may be or claim to be, the matter of fact is, no one in this world has intrinsic aptitude to perceive anyone’s mind by introspection. For this reason, I humbly beseech you to desist from arbitrary presupposition(s) [“historia ya uhuru wa Tanganyika imewaghadhibisha wengi nanaona wewe ni mmojawapo]

Mimi sio mtu wa ghadhab wala sighadhibishwi na maandishi ambayo kwa kiasi kikubwa ni private opinion(s) za mtu na wote tuna uhuru wa kufanya hivyo.
Historia inabaki kuwa historia na mengi ambayo mohamed anayoyaandika wengine tumehadithiwa hivyo hivyo kama yeye anavyoandika. Mimi nimekulia mtaa wa sukuma na sikukuu.Nyumba tuliyokuwa tunakaa ilikuwa inatizamana na Makao ya Yanga na kwa upande mwingine inatizamana na chuo cha sharif abdulrahman.
Ingawa nilikuwa mdogo lakini nakumbuka kuna wakati mwalimu na wazee walikuwa na vikao vyao ndani ya klabu na huko njee ili kuwa inapigwa taarab ya geresha na umati kujaa. Sisi kama watoto tulikuwa tunapenya hadi ndani na nimeshawahi kuona ikipigwa dua kali na mwalimu akiwa amekaa kati akizungukwa na wazee ambao walikuwa wanamsomea .
Ukweli utabaki hivyo hata tukiupinda namna gani utabaki tu. Ni bora tuukubali kwa sababu hakuna njia nyingine ya kukabiliana na ukweli.
 
Back
Top Bottom