Hakuna wa kumshtaki Bashite katika nchi hii, labda 2035

Hakuna wa kumshtaki Bashite katika nchi hii, labda 2035

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,079
Reaction score
4,893
Mnaopanga kumshtaki Mh. Sana Bashite msipoteze muda wenu huyo bwana hakuna wa kumshtaki kwa sasa katika nchi hii na ukifanikiwa kumshtaki kushinda hiyo kesi ni ndoto za mchana.

Hebu ni wakumbushe wakati kesi hii inafunguliwa kwa mara ya kwanza mahakama ya kinondoni ilikataa kata kata kuifungua mpaka kibali kilichotoka mahakama kuu je ulitegemea aliyefungua kesi ashinde?

Bashite ametenda mambo mengi sana kinyume cha sheria katika utawala huu wa Awamu ya 5 na miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kulikejeli bunge.

Kuvamia Clouds TV usiku akiwa na silaha

Kuwataja watu mbalimbali bila ushahidi kuwa wanafanya biashara ya madawa

Kumsingizia Mzee Lowassa kuwa katelekeza mtoto

Kumtaza mbunge kuja Dar lakini yote haya hakuna aliyethubutu kumshtaki

Kumbukeni mpambano wake na askofu gwajima.

Bashite aliingiza kontena na akagoma kulipia ushuru, je alifanywa nini?

Kwa matukio hayo ni dhahiri bashite ana kinga ya kutoshtakiwa mpaka awamu ya 7 huko ndio unaweza kumshtaki lakini awamu ya 5 na 6 hakuna wa kumshtaki

Na muda si mrefu atapata teuzi.


Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Kwani bibi maridhiano yeye anasemaje katika hili?
 
Hapa inatakiwa wale aliowafanyizia wachukue sheria mkononi wamalizane naye kimila tu,tena wengi ni watu wenye uwezo wa kumkomesha
 
Mh. Sana Bashite!! ndo nani,au unamzungumzia PAUL MAKONDA? "Sana" ndo jina la bibi yake?
 
Back
Top Bottom