Hakuna vita kati ya Mwigulu na Makamba, walitegewa mtego na kiongozi wao mwoga, Chawa wapumzike sasa

Samson Kwayu

Member
Jun 9, 2022
18
90
Hizi ni picha zilizopigwa leo tarehe 4/5/2023 zikiwaonesha vijana manguli wa siasa za Tanzania, Dkt Mwigulu Nchemba, January Makamba na Nape Nnauye wakiwa katika mjadala na tabasamu zito.

Picha hizi zimeibua mijadala mikubwa katika mitandao ya kijamii, baada ya hivi karibu kuiibuka mzozo mkubwa kuwa kuna vita kubwa kati ya Dkt Mwigulu na January Makamba, kuwa hawapikiki chungu kimoja na wanawindana kutoana roho.

Mjadala wa vita ukaanza kuvamiwa na watu mbalimbali wakichagiza yao wa sababu zisizojulikana lakini kubwa zaidi inasemekana kuna kiongozi mkubwa sana ambae anamiliki kundi la waandishi wa habari alichomeka majeshi yake ili kukoleza vita hii kwasababu hii ilikuwa inampatia haueni yeye kuelekea siasa za 2030 na kuendelea kuwa mkuu wao.

Ujio wa picha hizi unaonesha dhahiri shahiri kuwa wanasiasa hawa vijana wanachanga vyema karata zao na walimtega adui yao, na inawezekana tayari wamemwingiza kwenye kumi na nane zao, kinachosubiriwa na kumfyatua tu.

Vijana hawa watakumbukwa kwa mambo makubwa waliyoyafanya miaka 12 iliyopita muda ambao CCM ilikuwa imeelekezwa kibra lakini wao wakaingia na kuinasua, lahaula wakaambulia mabua baada ya waliemwingiza kuwageuka na kuanza kuwamaliza kisiasa kabisa.

Mimi kama mwanasiasa mkongwe nimefurahishwa na picha hizi kwani zinatoa funzo kwa wanasiasa wote nchini kuwa siasa zinahitaji akili tu sio papara.

Rai yangu kwa maadui wa hawa vijana, Rudin nyuma mfanye vyema calculations zenu maana wengi mmeingizwa kwenye siasa juzijuzi tu na mwendazake, hawa wenzenu wamepikwa wakaiva, wameteswa wakajifunza sio rahisi kunasa kwenye mitego ya kitoto.

Wasalaaam.
 
Imedhaminiwa na Serikali?

Je, hiyo mitegoi ndizo zinazochukua pesa zilizoombwa kupambana na Dis-information.....yaani Unataka kusema Serikali au Hawa Mawaziri ni moja ya Watu wanaosambaza habari Potoshaji Nchini kwa ajili ya michezo ya Kisiasa? Ati wameeingia kwenye Kumi na nane? Nani hao Wananchi.

Kweli kwa unguli wako unaodai wa Siasa umeona ni Sifa kuja kuutarifu Umma jinsi gani Mawaziri(Serikali?) inajihusisha na kuchakata, kuaandaa, na kueneza Habari Potofu? yaanu kana tamthilia? Ahhhhhh Jamani ehh Aiseee.

Mwanasiasa Mkongwe, Wananchi kuuliza maswali kuhusu utendaji wa hawa unatafsiriwa kuwa ni Uadui? Wananchi sasa wamekuwa Maadui?
 
Imedhaminiwa na Serikali?
Je, hiyo mitegoi ndizo zinazochukua pesa zilizoombwa kupambana na Dis-information.....yaani Unataka kusema Serikali au Hawa Mawaziri ni moja ya Watu wanaosambaza habari Potoshaji Nchini kwa ajili ya michezo ya Kisiasa? ...
Inasikitisha sana. Akiingia Mkenya humu jf anaweza kulia kwa akili na mijadala ya baadhi ya watu humu
 
Back
Top Bottom