Hakuna siku kiongozi atakuletea hela mfukoni

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,152
Reaction score
1,696
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa muda mrefu vijana wengi nchini Tanzania tumekuwa tukisubiri kwa matumaini: ahadi za ajira, mitaji ya biashara, misaada ya serikali au nafasi ya “kubebwa” na mtu fulani mkubwa. Lakini leo nataka kusema kile ambacho wengine wanasita kukisema — tumepumbazwa na kusubiri!

Rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan, kwa ujasiri mkubwa aliwahi kusema:

"Hakuna siku fedha zitaletwa na kiongozi kutoka juu. Kila mmoja wetu anatakiwa kufanya kazi."
Kauli hiyo ilipita kama upepo kwa baadhi ya watu, lakini kwa anayefikiri kwa kina, hayo ni maneno ya dhahabu. Hakuna serikali yoyote duniani yenye uwezo wa kuwapa kila kijana kazi au pesa mkononi. Lakini serikali inaweza kutengeneza mazingira. Na hilo Mama Samia analifanya — mazingira ya utulivu, fursa za elimu, teknolojia, uwekezaji na hata mikopo ya vikundi. Lakini mwisho wa siku, kazi ni yetu.

Tatizo Ni Nini?

Vijana wengi hatuna tatizo la uwezo, tunazo akili, nguvu, na ndoto. Tatizo ni kwamba tumetegemea sana miujiza badala ya mipango. Tumekuwa watazamaji wa maisha badala ya kuwa washiriki wa mabadiliko. Tuna muda mwingi kwenye mitandao, lakini hatutumii hata nusu saa kwa siku kusoma au kujifunza kitu kipya.

Sasa Tufanye Nini?

1. Jifunze ujuzi wowote – hata YouTube au simu yako ni darasa. Kuna vijana wanatengeneza pesa kupitia freelancing, content creation, coding, ujasiriamali mdogo, kilimo cha kisasa n.k.
2. Ungana na wenzako – kama huna mtaji, tafuta watu wawili au watatu mchanganye nguvu. Tangu lini kijana maskini akawa na sababu ya kujitenga?

3. Ondoa aibu ya kuanza chini – si kila mtu ataanza na ofisi ya AC. Fanya biashara ya mtaa, tumia kile ulichonacho.

Mama Samia Ametufungulia Njia — Ni Jukumu Letu Kupita

Tuna rais anayetuliza nchi, anavutia wawekezaji, anasimamia diplomasia, anahimiza amani na anawapa vijana nafasi. Lakini hawezi kutufanyia kazi.
Tunaweza kukosoa serikali, ndiyo. Lakini tukikosa kujikosoa sisi wenyewe, tutakosa maendeleo binafsi.

Vijana, tuchukue hatua. Tusiwe kizazi cha lawama. Tuwe kizazi cha suluhisho.

Kama umesoma mpaka hapa, chukua hatua moja leo.

#VijanaNaKazi
#TanzaniaMpyaNiSisi

Asanteni kwa kunisikiliza Vijana wenzangu.
 
Hata Upinzani wakichukua nchi hakuna siku watakuletea chakula mezani.

Wake-up kijana fanya kazi.
 
Acha uchawa. Kosa katutendea jiwe kwa kuumba huyu kiumbe
 
Back
Top Bottom