mwalimu mkweli
Member
- Dec 23, 2017
- 35
- 69
HAKUNA SHORT KATI KWENYE ELIMU
[HASHTAG]#Haya[/HASHTAG] matokeo ya Kidato cha nne yamebeba mambo makuu 2
1. [HASHTAG]#SWALA[/HASHTAG] LA UCHANGIAJI
[HASHTAG]#Kwenye[/HASHTAG] elimu hakuna Short Kati, swala la kupata elimu bora lina njia zake. Shule za binafsi zinapita kwenye njia hizo haishangazi tena kwa matokeo kutoka na shule kumi bora kuwa za binafsi huku kumi duni zikiwa za Umma.
[HASHTAG]#Huku[/HASHTAG] tulikotoka Shule za Umma zilikuwa zikichangia majaribio ya kila mwezi, zinachangia swala la Chakula nk . Pamoja na yote hayo bado tulikuwa tunakungutwa na Shule za Binafsi.
[HASHTAG]#Kwa[/HASHTAG] sasa wazazi wanajifanya hawaelewi maana ya Elimu bure. Wanavamia mashule kudai michango ya chakula, na michango mingine ya kuinua taaluma. Kama serikali haitafafanua vizuri sera hii ya Elimu bure hawa watoto wa walalahoi watakuwa wanajidanganya.
Hebu angalia shule hizi kumi bora
1: St Francis girls
2: Feza boys
3: Kemo bOSS
4: Bethel Saabs
5: Anuarite
6: Marian girls
7: Canossa
8: Feza girls
9: Marian boys
10: Samshei boys
Nendeni kwenye hizi shule mkaangalie wanakula nini, wanalala wapi, wanasomea wapi, mishahara ya wafanyakazi nk.
Angalieni wazazi wanachangiaje nahitaji ya Muhimu kwa watoto wao nk. Halafu wakati mnaondoka ukizieni ni watoto wa akina nani wanaosoma kwenye shule hizo yaani viwango vyao vya kiuchumi na hali zao kijamii.
#Ni kweli kwamba tunataka wanafunzi wa shule zetu za Kata kutoka saa nane kisa hawana chakula shuleni? Wakati wao wanatafuta chakula wenzao wa binafsi wanawaza kusoma tu.
[HASHTAG]#Kitu[/HASHTAG] pekee cha kumkomboa mtoto huyu wa mlalahoi ni Elimu tu. Viongozi wetu tunaomba mfafanue vizuri sera yetu ya Elimu bure....
2. # LUGHA YA KUFUNDISHIA.
Kwenye Ufaulu wa mwaka huu Somo la Kiswahili ndilo lililofanya vizuri limefaulisha kwa asilimia 84 huku Hisabati likifaulisha kwa asilimia 19.
[HASHTAG]#Niliwahi[/HASHTAG] kufundisha hapa kuwa Feral child ni aina ya watoto wanaokuwa au kukuzwa bila kupata malezi ya Binadamu mwenzao. Kwa maana nyingine tunasema ni watoto wa binadamu waliokuzwa na kulelewa na jamii nyingine za wanyama kama vile jamii ya Sokwe, Mbwa, Mbuzi nk.
Ipo mifano mingi ya watoto kama hawa duniani, hii hapa ni mifano michache tu:-
1.Saturday Mthiyane alipatikana mwaka 1987 huko Kwa Zulu Natal alikuwa kwenye Kundi la Skokwe na alikuwa tayari ameshajifunza tabia zote za Sokwe na alikuwa hawezi kuongea chochote.
2.Baby Hospital (1984) Huko Sierra Leone Wamisionari walimwokoa, alikwa tayari kashajifunza tabia zote za Sokwe na alikuwa hajui kuongea chochote.
3.Oxana Malaya, (1990s)Ukraine, huyu alitelekezwa na wazazi wake huko Ukrain kutokana na ulevi alikuwa akiishi na Mbwa alipokutwa alikuwa tayari ameshajifunza kubweka kama mbwa. Madaktari walimhudumia walidai kuwa alizaliwa akiwa na afya njema kabisa lakini alipookolewa alikuwa tayari anatabia zote za Mbwa.
4.Danielle Crockett, U.S.A aliokolewa na vyombo vya Usalama mtoto huyu kwa kuwa wazazi wake walikuwa wamemtelekeza ndani. Walikuwa wakimfungia ndani kwa hiyo alipata Ulemavu wa viungo na Kushindwa kuongea kwa kuwa hakupata Interactions na binadamu wenzake.
NAMAANISHA NN
Binadamu hujifunza tabia ikiwemo Lugha kutokana na Mazingira aliyopo. Kama watoto hawa wakati wanazaliwa wangelitunzwa na binadamu basi wangeliweza kuongea na kuwa na tabia za Binadamu.
Nadharia hii nimependa kuitumia siku ya leo ili kuihusianisha na elimu yetu tunayoipata. Leo nitaongelea kipengele kimoja tu cha Lugha.
Kwa WATANZANIA walio wengi Lugha yao ya Kwanza kujifunza na wanayoijua kwa ufasaha zaidi ni Lugha za makabila yao. Yaani ipo Kisayansi kuwa Lugha ya kwanza utakayojifunza utakuwa na uelewa nayo mkubwa zaidi kuliko lugha ya pili kujifunza na ya tatu. Kuna baadhi ya makabila wanajua lugha yao hiyo ya kikabila tu. Na Lugha utakayojifunza ukiwa bado na Umri Mdogo unakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuimudu kuliko Lugha zozote zile utakazokuja kujifunza baadaye.
Kiswahili ni Lugha yetu ya pili kujifunza, hii tunaimudu vizuri sana kwa kuwa hata kwenye familia zetu tunaiongea. Kiingereza hii ni lugha ya tatu kujifunza kwa hapa kwetu Tanzania kwa waliowengi.
SHULENI
Kwa Tanzania Lugha inayotumika kufundishia na kujifunzia ni Mbili tu yaani Kiswahili na Kiingereza. Kiswahili tunakitumia kwa shule za msingi na kiingereza tunakitumia kuanzia sekondari hadi Chuo kikuu.
Nchini Kenya na Uganda lugha ya kufundishia ni Kiingereza isipokuWa kwa baadhi ya masomo.Nchi ya Rwanda ilibadili lugha yake ya kufundishia kutoka Kifaransa hadi Kiingereza.
Nchi nyingi za Ulaya na Amerika zinztumiz Lugha zao kufundishia na mambo yanakuwa marahisi sana. China wameamua kukomaa na kichina chao huko Korea na Kwingineko.
Kuanzia darasa la awali mpaka darasa la saba mtu anasoma kwa Kiswahili miaka yote 8 Halafu miaka 9+ iliyobakia unamwambia atumie Kiingereza. Mtu huyu unamfundisha miezi mitatu English Course halafu unaanza kumfundisha mada na nadharia mbalimbali huu ni utani tunafanya kabisa.
Wahitimu wengi wanamaliza wanaitwa kwenye interview wanashindwa kujieleza na hawa ni wahitimu wa shahada ya kwanza. Hii ni hatari kubwa sana kuna ambao hata CV zetu hatuwezi kuziandika kabisa.
SHULE ZA MCHEPUO WA KIINGEREZA.
Kwa Tanzania kuna Shule tunazoziita English Medium primary schools. Kuna baadhi ya Watanzania wamefanikiwa kupeleka watoto wao kwenye Shule hizi. Hawa wanafundishwa kwa Lugha ya Kiingereza kuanzia darasa la Awali hadi Secondari.
Afadhali hawa hawachanganyi sana mambo na imeaanza kubainika wakifika Sec wengi wao wanafanya vizuri ikilinganishwa na hawa ambao wamechanganya Lugha.
TUFANYE NINI?
1. #Ni wakati wa Serikali sasa kuamua kutumia Lugha Moja kuanzia awali hadi chuo kikuu. Kuna ambao wanapendekeza iwe kiswahili mimi sioni tatizo.
Kuna ambao wanapendekeza iwe kiingereza pia naona sio tatizo alimradi hatuchanganyi mambo.
2. [HASHTAG]#Tutazame[/HASHTAG] upya wanaojiunga ba vyuo vya ualimu. Kwa miaka mingi Tanzania imekuwa ikitumia wale waliopata madaraja ya chini kwenda kufundisha mashuleni.
Hii inapelekea waalimu wengi kutokumudu stadi husika zinazopaswa kufundishwa darasani. Yaani waliofaulu vizuri tunawapngia kazi nyingine huku kwenye idara ya elimu wanapelekwa hawa waliopata ufaulu hafifu.
[HASHTAG]#Sifa[/HASHTAG] za kujiunga kwa sasa na ualimu kwa shule za msinhi zimepandishwa hadi kufikia Sifa div three. Sifa hii ni sifa inayolingana na mtu anayetaka kujiunga na masomo ya form six. Watu wengi wenye sifa hizo wamekuwa hawataki kujiunga na ualimu badala yake wanakimbilia form six jambo ambalo litakuja kuleta uhaba mkubwa sana wa waalimu wa shule za msingi siku za usoni.
3. #Ni wakati sasa Serikali kukubali kuajiri moja kwa moja wahitimu wa chuo kikuu kwenda kufundisha shule za msingi. Na serikali iamue moja kwa Lugha ya kufundishia kuanzia sasa iwe moja.