Hakuna nchi iliyoendelea kwa kubadilisha Chama!

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,838
Watu wengi ukisikiliza maoni yao utasikia wanakwambia tunataka CCM iondoke, ukiwauliza nani aje wanakwambia yoyote tu bora tu tubadilishe ili tuendelee sasa mimi leo ninawasaidia kubadilisha Chama hakuleti maendeleo kwanza ni kinyume chake!

Hakuna nchi tajiri au iliyofanikiwa Duniani kiuchumi iliyowahi kubadilisha Chama, nchi zote zilizo tajiri leo hii zimekuwa zikiongozwa na Chama kimoja siku zote na hawajabadilisha na nitatoa Mifano, Ujapani inaongozwa na Chama kimoja kwa Miaka zaidi ya 50 na ndicho kilichoijenga Ujapani, Korea Kusini inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Korea, Uchina inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Uchina, Taiwani Chama Kimoja, hata Malaysia inaoongozwa na chama kile kile tangu Uhuru hawajawahi kubadilisha na ndicho kilicholeta maendeleo Malaysia!

Afrika Kusini iliongozwa na Chama Kimoja cha National Party kuanzia 1948 mpaka 1994 na ndicho kilichojenga AK tunayokimbilia kila siku, hata hapa Afrika nchi zilizofanikiwa kama Angola, Namibia, Botswana na sasa hivi Msumbiji wanakwenda vizuri hawajawahi kubadilisha Chama!

Sasa ukiangalia nchi zenye tabia ya kubadilisha badilisha Vyama ni masikini kama India, Pakistani, Zambia, Kenya, hata nchi za Ulaya siku zinaanza kuwa na matatizo ya Kiuchumi baada ya kuanza kubadilisha badilsha vyama kumbuka Ulaya ni tajiri kwa sababu ilijengwa na Wafalme ambao walikuwa hawabadilshwi!

Hivyo mimi bado naamini kabisa kwamba kama TanZania tunaweza kutoka hapa kimaendeleo basi ni ndani ya CCM na si kwingineko waache Upinzani watumike kama vile sasa hivi kuishtua CCM ili iamke kama ilivyofanya sasa hivi kwa kujivua gamba na sasa tuko ready for take off!

Basi kama Muanzisha Mada naifunga kama inawezekana kwa kusema hivi Wote mnaotukana na kukebehi nawaambia hivi tatizo ni ninyi na wala siyo CCM au TanZania ni kama vile mtoto aliyeshindwa maisha halafu anaishi siku zote kwa kumlaumu baba yake kwamba ndiyo sababu ya yeye kuwa na maisha magumu!

Kila la heri na fisadi Lowasa!

huhuhu.....ni kweli mkuu lakini sisiemu mbona mmechelesha maendeleo???? hizi nchi zote tulikuwa sawa wakati tunapata uhuru hata nyingine kama s.Africa tuliisaidia kupata uhuru.... sasa sisiem miaka 50 bado tuwape muda?????? no you must leave!!!
 
Kenya Je? ama unajitia upofu kuona jirani yetu uchumi upo juu baada ya kuondoa chama tawala?? kiliporudi kikawa na nidhamu

Nisome vizuri tena kama ukipenda nimesema hakuna nchi iliyoendelea leo hii ambayo iliwahi kubadilisha Chama, sasa Kenya ni nchi iliyoendelea?
 
Vipi Marekani, Uingereza na Ujerumani? . Narrow minded.

Ujerumani na Uingereza ni tajiri na hizi nchi kama zilivyo nyingi za Ulaya zilijengwa na Wafalme (Monarch) ambao walikuwa hawabadilishwi haya mambo ya kubadilisha vyama wameanza siku hizi baada ya kuwa nchi tajiri tayari lkn wakati wako ngazi ya maendeleo kama yetu kulikuwa na Wafalme tu ambao walikuwa wana absolute power na walikuwa hawabadilishwi!

Na nchi za Asia zote ambazo zimeendelea hivi karibuni zimeiga Ulaya nazo zote zimejengwa na Chama kimoja hakuna hata moja ambayo ni tajiri leo iliyowahi kubadilisha Chama si Japani, Korea Kusini wala Singapore na wale ambao wanabadilisha vyama kila siku kama India, Pakistani, Sri Lanka Bangladeshi ni masikini!
 
Nisome vizuri tena kama ukipenda nimesema hakuna nchi iliyoendelea leo hii ambayo iliwahi kubadilisha Chama, sasa Kenya ni nchi iliyoendelea?

sisi tunataka kubadilisha chama, maana ni chama mfu.
wewe unawaza kubadili wanaume, subiri mimba usiomjuwa baba halisi wa mtoto
 
Watu wengi ukisikiliza maoni yao utasikia wanakwambia tunataka CCM iondoke, ukiwauliza nani aje wanakwambia yoyote tu bora tu tubadilishe ili tuendelee sasa mimi leo ninawasaidia kubadilisha Chama hakuleti maendeleo kwanza ni kinyume chake!

Hakuna nchi tajiri au iliyofanikiwa Duniani kiuchumi iliyowahi kubadilisha Chama, nchi zote zilizo tajiri leo hii zimekuwa zikiongozwa na Chama kimoja siku zote na hawajabadilisha na nitatoa Mifano, Ujapani inaongozwa na Chama kimoja kwa Miaka zaidi ya 50 na ndicho kilichoijenga Ujapani, Korea Kusini inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Korea, Uchina inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Uchina, Taiwani Chama Kimoja, hata Malaysia inaoongozwa na chama kile kile tangu Uhuru hawajawahi kubadilisha na ndicho kilicholeta maendeleo Malaysia!

Afrika Kusini iliongozwa na Chama Kimoja cha National Party kuanzia 1948 mpaka 1994 na ndicho kilichojenga AK tunayokimbilia kila siku, hata hapa Afrika nchi zilizofanikiwa kama Angola, Namibia, Botswana na sasa hivi Msumbiji wanakwenda vizuri hawajawahi kubadilisha Chama!

Sasa ukiangalia nchi zenye tabia ya kubadilisha badilisha Vyama ni masikini kama India, Pakistani, Zambia, Kenya, hata nchi za Ulaya siku zinaanza kuwa na matatizo ya Kiuchumi baada ya kuanza kubadilisha badilsha vyama kumbuka Ulaya ni tajiri kwa sababu ilijengwa na Wafalme ambao walikuwa hawabadilshwi!

Hivyo mimi bado naamini kabisa kwamba kama TanZania tunaweza kutoka hapa kimaendeleo basi ni ndani ya CCM na si kwingineko waache Upinzani watumike kama vile sasa hivi kuishtua CCM ili iamke kama ilivyofanya sasa hivi kwa kujivua gamba na sasa tuko ready for take off!

Umekosea kitu kimoja gamba,nchi zote ulizosema hazijabadilisha vyama zina kitu kikubwa sana cha kuonyesha(namaanisha maendeleo makubwa katika nyanja zote) halafu bahati nzuri umesema miaka 50 hawajabadilisha.Je sisi kwa hiyo miaka 50 tuna nini?zaidi ya kuambiwa nchi bado changa.
 
Aisee acha kuongea ujinga!! Una utafiti uliofanya usiongee mambo ambayo yanausisha utafiti! Ccm mnapumzika imetosha, kutowachagua nyie tutaokoa ata maisha ya wanyama wetu, kama tembo simba na nk.

Unataka utafiti gani? Nimekwambia hakuna nchi iliyoendelea ambayo ilibadilisha Chama wakati wa kuendelea kwake na mifano nimekupa sasa kama unapinga unaweza pia kuweka mifano badlaya tu kusema wacha kuongea sijui nini...
 
Back
Top Bottom